Chifu Wanzagi amemkabidhi Makongoro Nyerere kifimbo cha Mwalimu kama ishara ya uongozi

Swali linakuja je ameshawahi kuongoza ai kusaidia jamii yoyote?

Swissme
 
Hata wampe kifimbo hawezi kushinda watanzania tumechafuka hatuwezi kuongozwa na kifimbo sisi sio man,gombe
 
Ukiujua ukweli utakaa katika hilo,ila kwa sasa macho yamefungwa sababu aidha ya vipesa nk. Na yeyote aliye wa ukweli haachi kuuutafuta ukweli. Na daima atachukiwa na wale wasiopenda ukweli. Qn ukweli ni kitu gani? Tough Qn in the contemporary arena.
 
  • Thanks
Reactions: DSN
Hivi kifimbo hiki kina sifa zaidi ya urembo?ndio nguzo ya utawala?Au ndio utawala wenyewe?
 
Swali linakuja je ameshawahi kuongoza ai kusaidia jamii yoyote?

Swissme

Nafasi za Uongozi alizopita
1: Kiongozi Jeshini Ngazi ya Luteni.
2: Mbunge Wa Kuchaguliwa Jimbo La Arusha Mjini Tiketi Ya NCCR
3: Mwenyekiti Wa CCM Mkoa Wa Mara
5: Mbunge Wa East Africa-Tanzania


Historia yake
Makongoro Nyerere ni mtoto wa tatu wa Rais wa kwanza wa Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na kwa sasa ni Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (Eala).
Makongoro alizaliwa Januari 30, 1956 (Amefikisha miaka 59 Januari mwaka huu).
Alisoma katika shule za msingi Bunge na Isika zote za Arusha kati ya mwaka 1964–1972 na akajiunga na shule sekondari ya Wavulana Tabora alikohitimu kidato cha nne.

Mwaka 1979 alijiunga na Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) na alipelekwa mstari wa mbele kwenye vita ya Uganda, kikosi cha Mizinga na baada ya vita yeye ni mmoja wa askari waliobakizwa ili kulinda amani ya wananchi wa Uganda lakini pia kufundisha askari wapya raia wa Uganda kwa ajili ya mipango ya baadaye ya kuilinda nchi yao wao wenyewe.
Aliporejea nchini kutoka vitani Uganda aliendelea kutumia jeshi kwa muda mfupi kabla ya kupelekwa katika Chuo cha Mafunzo ya Maofisa wa Jeshi (TMA), Monduli–Arusha na alishiriki na kufuzu mafunzo ya Ofisa Kadeti na akawa Ofisa wa Jeshi la Tanzania rasmi hadi alipostaafu rasmi mwaka 1990 akiwa na nyota mbili “Luteni”.

Baada ya kujiunga na kushiriki katika siasa kwa miaka mitano, aliamua kwenda nchini Scotland ambako alisoma Shahada ya Masuala ya Mikakati katika Chuo Kikuu cha Aberdeen, hii ilikuwa mwaka 2001 – 2003.
Makongoro ameshika nyadhifa mbalimbali ndani ya CCM na wadhifa mkubwa aliowahi kushika ni uenyekiti wa chama hicho katika Mkoa wa Mara 2007–2012, lakini pia Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, moja ya vikao muhimu ndani ya chama hicho.
Makongoro amemuoa Jaji Aisha Nyerere na wamepata watoto watatu, wa kwanza anaitwa Julius Kambarage Nyerere, wa pili ni Daudi Nyerere na wa tatu ni Prince Nyerere.

Mbio za ubunge

Mwaka 1995, Makongoro Nyerere aliwashangaza Watanzania na hasa wanachama wa CCM baada ya kufanya uamuzi wa kukihama chama hicho na kujiunga na chama kilichokuwa maarufu sana wakati huo, NCCR Mageuzi.
Baada ya kujiunga NCCR, Makongoro alitangaza kuwa anagombea ubunge katika jimbo la Arusha Mjini kupitia NCCR. CCM ilifanya kila iwezalo lakini nguvu ya Makongoro ikawa kubwa, akapata asilimia 41.6 na kumshinda Felix Christopher Mrema wa CCM (Aliyewahi kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali) aliyenyakua asilimia 39.9, huku Mzee Edwin Mtei (Waziri Mstaafu wa Fedha na kiongozi wa Chadema wakati huo) akipata asilimia 13.5 ya kura zote.

Mwalimu Nyerere mwenyewe aliwahi kusikika akitoa ‘kijembe’ kuhusu familia yake kuwa “…familia yangu iko mstari wa mbele mabadiliko. Nina wafuasi wa CCM, CUF na NCCR…” Nyerere alikuwa anasema hivyo kwa sababu, Leticia Nyerere (mke wa kijana wa Nyerere) ni mtoto wa Mzee Musobi Mageni aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi CUF (miaka ya 1990).
Felix Christopher Mrema wa CCM alikata rufaa katika Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, akilalamikia ushindi wa Makongoro Nyerere. Felix alisisitiza kwenye rufaa yake kuwa Msimamizi wa Uchaguzi hakuhesabu kura za vituo kadhaa na pia kulikuwa na kura hewa zaidi ya 5,246.

Mahakama Kuu ilitupilia mbali maombi ya Felix, lakini akakata rufaa kwenda Mahakama ya Rufaa ambayo ilijiridhisha kuwa Makongoro alishinda isivyo halali. Ubunge wa Makongoro ukatenguliwa na uchaguzi mdogo ukaitishwa lakini yeye (Makongoro) hakushiriki.
Aliamua kupumzika masuala ya siasa na kujiendeleza kielimu. Alikwenda nchini Urusi na baadaye Uskochi na mwaka 2000 alijiunga tena CCM na baada ya mwaka 2003 akarejea nchini kutoka masomoni ambapo Rais Mkapa alimteua kuwa Mbunge mwaka 2004 – 2005.
Makongoro alirejea tena katika siasa kwa nguvu alipokuwa akisaka ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki. Hii ilikuwa mwaka 2012 na alichaguliwa kwa kura 123 na kuwa mbunge wa Bunge hilo hadi muda wake utakapokamilika mwaka 2017.

Mbio za urais

Vyombo mbalimbali vya habari vimekuwa vikimuuliza Makongoro Nyerere kujua kama yumo kwenye kinyang’anyiro cha kuomba ridhaa ya urais kupitia CCM, hakuwahi kukubali au kukataa na mara ya mwisho amehojiwa na gazeti la kila siku linaloheshimika sana nchini Tanzania, bado akawa hakubali au hakatai. Lakini vyanzo vyangu ndani ya CCM na hata watu wa karibu na Makongoro, wamenithibitishia kuwa milango ikishafunguliwa atachukua fomu. Nimesisitizwa kuwa tayari Makongoro amekwishafunga safari na kuonana na viongozi wengi wa juu waliowahi kuongoza nchi hii wakiwemo marais wastaafu, mawaziri wakuu wastaafu, majaji wakuu wastaafu na wakuu wastaafu wa vyombo vya ulinzi na usalama. Inaonekana Makongoro hataki kuanza kutajwatajwa sana lakini ana mipango thabiti. Nilipomuuliza juu ya nia hii, hakukubali wala kukataa kwa hiyo mimi nimehitimisha kuwa “yumo kwenye mtanange”.

Nguvu yake

Makongoro ni mtu wa kujitolea sana, siyo kwa kutoa fedha, lah! Kujitolea kufanya mambo ambayo yatawasaidia watu wengine na hata taifa lake. Mwaka 1979 alijiunga jeshini kama mmoja wa vijana waliohitaji kulinda taifa lao dhidi ya nduli Idd Amin. Tunajua kuwa watoto wengi tu wa vigogo wakati huo walikwepa wajibu huo, Makongoro hakuwa mmoja wao.
Lakini Makongoro anapewa nguvu na mtazamo wa jamii kumhusu. Anatazamwa kama mtu wa kawaida tu. Hakuwahi kuthubutu kujijengea tabia za “Unyerere” kwa maana ya taswira ya baba yake. Ni mtu ambaye ukikaa naye chini siku nzima, kama hujaambiwa na mtu wa jirani kuwa huyu ni kijana wa Baba wa Taifa, hutaweza kugundua. Anaishi maisha ya Utanzania zaidi kuliko ya “kuwa mtoto wa Rais wa Kwanza wa Taifa hili”. Leo hii tunashuhudia watoto wangapi wa marais wetu ambao hawawezi kupanda “bajaji au daladala”? Makongoro hachagui nini avae, nini ale na nini apande. Watu wake wa karibu wananiambia kuwa amefaulu kabisa kujijenga yeye kama yeye na si yeye kama mtoto wa Nyerere.

Uthubutu ni nguvu ya tatu ya Makongoro. Kiongozi yeyote yule anayejiandaa kuongoza dola lazima awe na uwezo wa kuthubutu kufanya mambo fulani fulani ili kujenga mustakabali mwema mbele ya safari. Mwaka 1995 alipohamia NCCR huku baba yake akiwa ni muasisi wa mwanzo wa Tanu na CCM, wengi walimshangaa sana lakini hakutishwa na kivuli cha “mishangao” hiyo, alipigana na kushinda ubunge Arusha bila kusaidiwa na kivuli cha baba yake? Watoto wangapi wa marais wengine wanaweza kuthubutu kuhamia upinzani na wakagombea na kuishinda nguvu kubwa ya dola za wazazi wao?

Lakini jambo la mwisho kwa hapa ni kufahamika. Makongoro Nyerere ni mtoto wa Nyerere anayefahamika, kutajwa na kuonekana sana kuliko watoto wengine wote. Walau kwa kizazi cha Mwalimu Nyerere, unaweza kusema kuwa Makongoro ndiye amewapita wenzake wote katika ushiriki wa juu wa masuala ya siasa na hata uongozi ndani ya CCM. Kufahamika ni karata muhimu kwake katika mbio hizi.

Udhaifu wake

Udhaifu mkubwa wa Makongoro ni “kufanya maamuzi ya haraka”. Watu wa karibu yake, waliofanya kazi naye bungeni na kwingineko wanasema yeye ni mtu wa kufanya maamuzi na si kulaza viporo. Mbunge mmoja wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka Tanzania alinidokeza kuwa yeye hutaka mambo yajadiliwe na kumalizwa na hapendi hata kidogo kulaza masuala ambayo yalihitaji kukamilishwa kwa wakati.

Pamoja na kuwa nchi inahitaji kiongozi anayefanya maamuzi haraka lakini yanapaswa kuwa maamuzi makini. Hadi sasa sijapata ushahidi wa maamuzi yapi Makongoro aliwahi kuyasimamia kwa haraka lakini yakawa na tija kubwa.
Udhaifu mwingine mkubwa wa Makongoro ni kutokuwa na visheni ya kudumu katika siasa. Makongoro tofauti na wanasiasa wengi wa Afrika anachukulia siasa kama suala la wakati na kipindi fulani. Ndiyo maana alipoenguliwa katika nafasi ya ubunge mwaka 1997 pale Arusha, akaamua kutogombea tena akarudi kusoma na baadaye kati ya mwaka 2005–2012 hakugombea nyadhifa zingine za kiuwakilishi kabla ya Eala.

Tabia hii ya kugombea miaka kadhaa na kuacha na tena kurudi baada ya miaka mingine imemfanya Makongoro asijijengee uhakika wa kisiasa na imemnyima fursa ya kusimamia masuala makubwa ambayo leo angewaonyesha Watanzania kuwa aliwahi kutulia mahali fulani na akasimamia masuala hayo. Watu wake wa karibu pia, wameutaja huu kama udhaifu mkubwa.

Nini kinaweza kumfanya apitishwe

Mambo kama matano hivi yanaweza kumfanya Makongoro avuke mchujo na kuwa mgombea wa CCM:
Jambo la kwanza ni historia yake ya kulitumikia taifa jeshini hadi alipoamua kustaafu mwenyewe lakini pia uzoefu wake ndani ya uongozi na katika kusimamia masuala ya kikanda (Afrika Mshariki). Makongoro ni mmoja wa wabunge wa kutegemewa katika Bunge la Afrika Mashariki akiisaidia Tanzania na ana bahati ya kukubalika hata kwa viongozi wa nchi jirani kama Kenya na Uganda.

Kama CCM itamvusha Makongoro, pia ni kwa sababu ya maadili. Yeye ni mtu mwenye msimamo na kusimamia maadili. Ndiyo maana wakati wa vikao vya Halmashauri Kuu ya CCM ni Makongoro ndiye alisimama kidete na kuwanyooshea vidole makada kadhaa ambao walikuwa wanatuhumiwa kukipatia chama hicho taswira mbaya. Makada hao ni watu wenye uwezo mkubwa wa kifedha na wanaogopwa hasa ndani ya CCM, lakini Makongoro alichukua msimamo mzito mno. CCM ya sasa inaweza kuhitaji mgombea wa namna hii ili kuinusuru na kuirudishia heshima.

Jambo la tatu linaloweza kumvusha ni kuifahamu vizuri CCM ikiwa ni pamoja na kutoharibu taswira ya baba yake. Nyerere alichukia rushwa na Makongoro anachukia sana rushwa. Nilipomuuliza jambo gani analolichukia kwenye ukurasa wake wa facebook, alinijibu kuwa la kwanza ni rushwa, nilipomuuliza la pili alisisitiza “rushwa” na la tatu… rushwa. Kwa sababu anakifahamu vizuri chama chake na ameweza kubeba taswira ya baba yake, huenda akawa mwarobaini ndani ya CCM na hivyo akavushwa.
Jambo la nne linaloweza kumvusha Makongoro ni dhana ya kuua nguvu ya makundi yanayoshindana na yaliyojipanga muda mrefu sana. Kama CCM itahofia kuparaganyika vibaya na inahitaji kurejea kwenye heshima. Makongoro anaweza kuwa mtu muhimu wa kubeba dhamana hiyo na labda kukiacha chama hicho salama.

Gazeti moja la kila siku la Kiingereza, limewahi kuandika kuwa:“Marketing Mr Makongoro is every easy because of the enduring legacy his father left behind to ordinary Tanzanians as well as the elite, many would empathise with him during the election.” (Tafsiri yangu – “Kumuuza Makongoro ni rahisi sana kwa sababu ya heshima ambayo baba yake aliiacha kwa Watanzania wa kawaida pamoja na watu wa kati, watu wengi wataungana naye kwenye uchaguzi”). Hakika, kama CCM inahitaji mtu anayeuzika katika uchaguzi wa mwaka huu, huenda Makongoro ni mmoja wa mtu wa aina hiyo.

Nini kinaweza kumwangusha?

Mambo matatu makubwa yanaweza kumwangusha Makongoro:
La kwanza ni makundi yenye fedha na yaliyojipanga kunyakua urais kupitia CCM, na yameshafanya hivyo kwa kipindi kirefu sana na hivyo kuingia kwake katika hesabu kunaweza kuyafanya makundi hayo yatumie kila mbinu kummaliza kisiasa kwanza ili wakosekane watu mbadala wa kufikiriwa na chama hicho.

Jambo la pili ni uamuzi wake wa kuhama CCM mwaka 1995 na baadaye kurejea mwaka 2000. Chama hicho kinaweza kuwa bado kina hofu na tabia yake ya kufanya maamuzi ya namna hiyo na kwa sababu katika rekodi za marais waliotokana na CCM na kuongoza Tanzania, hakuna mmoja wao ambaye aliwahi kuhamia upinzani kisha akarejea CCM, huenda “zengwe” hili likatumika kummaliza.

Jambo la mwisho ni kukosa ufuasi mkubwa sana ndani ya CCM. Kama CCM itataka kumpitisha mgombea urais wake kwa kutazama nani ana wafuasi wengi ndani ya chama hicho kwa sasa, huenda Makongoro asiwe chaguo. Makongoro hana ufuasi mkubwa ndani ya CCM kwa sababu ufuasi ndani ya chama hicho unajengwa sana na nguvu ya fedha na mitandao, mambo ambayo yeye aliniambia kuwa hawezi kujihusisha nayo.

Asipopitishwa (mpango B)

Namuona Makongoro akijielekeza katika mipango miwili na kufanikiwa, iwapo hatapitishwa kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mpango wa kwanza ni kuendelea kutumikia ubunge wake wa Bunge la Afrika Mashariki na kisha atakapomaliza kipindi cha kwanza aombe kingine na kuendelea kuwakilisha huko.
Mpango wa pili ni kujipanga na kugombea ubunge wa jimbo la Musoma Vijijini.

Mpango wa mwisho unaweza kuwa Kuendeleza kazi za Baba wa Taifa katika maeneo ya haki, umoja na amani. Ikumbukwe kuwa pamoja na taifa hili kupata mchango mkubwa kwa wazee wengi akiwamo Mwalimu Nyerere, historia na kazi za wazee hao hazijatangazwa kitaifa na kimataifa. Huenda Makongoro akaamua kuachana na siasa na kuanza kutangaza juhudi za watu waliopigania taifa hili akiwamo baba yake huku akihamasisha mshikamano katika taifa, umoja, haki na udugu.

Hitimisho

Kujitokeza kwa Makongoro Nyerere katika kusaka urais wa Tanzania kupitia CCM kuna maana kubwa sana, lakini ni kitisho kikubwa kwa kambi zilizojipanga muda mrefu uliopita. Nchi nyingi duniani pia zinaongozwa na vijana ambao wazazi wao walikuwa viongozi wakuu wa mataifa hayo. Mimi huwa sielewi maana ya falsafa hiyo na nilipofuatilia katika nchi zingine nimegundua kuwa vijana wa marais wanapoanza safari ya kutaka ukuu, watu wengi huwachukulia kama wanafanya masihara lakini mwisho wa siku huwa viongozi. Na kwa namna CCM ilivyozidiwa na mpasuko, nina uhakika kuwa watu kama Makongoro Nyerere wana turufu muhimu sana mkononi. Namtakia ndugu huyu ‘kama alivyoomba nimuite’ kila la heri katika nia hii ya urais.

Julius Mtatiro: Ni Mchambuzi wa Masuala ya Kisiasa na Kijamii; ana uzoefu mkubwa wa uongozi wa kisiasa hapa Tanzania. Ana Cheti cha Juu cha Sarufi na Lugha, Shahada ya Sanaa (B.A) katika Elimu (Lugha, Siasa na Utawala), Shahada ya Uzamili ya Utawala na Uongozi (M.A) na ni mwanafunzi wa fani ya sheria (LLB) – Anapatikana kupitia +255787536759.

Uchambuzi huu unatokana na utafiti na maoni yake binafsi.
 
Hata wampe kifimbo hawezi kushinda watanzania tumechafuka hatuwezi kuongozwa na kifimbo sisi sio man,gombe

Hivyo vifimbo maasai wanavyo pamoja na marungu kama ya mzee pembe long time.Hakuna mabadiliko
Sio muda wa kuongozwa na vifimbo . vote for ukawa
 
Ndo rais huyo watanzania wanamtaka mzalendo nyie Team Mafisadi imekula kwenu...mlikua mnataka mkapange ikulu?mtuuze vizuri?...anzeni tu kutema pesa za watu mlizokula yani mnataka pesa mle nyie afu waje walipe watanzania wote?ikulu sio pango la walarushwa ....Makongoro Up...go shine bright mafisadi washaanza kupoteana
 
huyu jamaa atawasumbua sana wapinzani mwaka huu kwenye uchaguzi mkuu.huyu ndiye chaguo la ccm.time will tell.
 
  • Thanks
Reactions: DSN
Maakongoro anafaa sana kwani anayajua maisha ya aina zote na siasa zote,kakutana na shughuri pevu ya kagera war,kazaliwa ukoo wa kichief làkini kaishi kama mie na wewe,kajiweni na mtaani(site)anapaelewa nje ndani,

siasa zote mpaka za wapinzani kazifanya,huyu ndo anayetufahaa,real man.Ni sawa na unapompata waziri Wa elimu ambaye kasoma kote,private na public,day na boarding n.k.Utamficha nini,utamzunguka vipi? ...a.k.a mzee Wa falsafa.
 
  • Thanks
Reactions: DSN
huyu jamaa atawasumbua sana wapinzani mwaka huu kwenye uchaguzi mkuu.huyu ndiye chaguo la ccm.time will tell.

Mkuu nakwambia huyu jamaa siyo tu kubebwa ila siasa anayo tena ya kutosha na kuongea pia anajua,tena kwa hoja.Mwaka huu kama anapitishwa huyu binafsi kwa uraisi CCM wana chukua kura yangu,true.
 
Maakongoro anafaa sana kwani anayajua maisha ya aina zote na siasa zote,kakutana na shughuri pevu ya kagera war,kazaliwa ukoo wa kichief làkini kaishi kama mie na wewe,kajiweni na mtaani(site)anapaelewa nje ndani,

siasa zote mpaka za wapinzani kazifanya,huyu ndo anayetufahaa,real man.Ni sawa na unapompata waziri Wa elimu ambaye kasoma kote,private na public,day na boarding n.k.Utamficha nini,utamzunguka vipi? ...a.k.a mzee Wa falsafa.


Kikwete ni mjanja sana, na kama atafanikiwa kumkabidhi nchi Mako yeye na familia yake watakuwa salama zaidi na pia atakuwa na heshima zote. Kaucheza mchezo siku nyingi kimyakimya bila kumshirikisha mtu mpaka vuuuuu!...yaani naweza faninisha na ule ugonjwa alomficha mother mpaka pale alipotakiwa kufanyiwa upasuaji huko nje.. Kikwete ni mwana mikakati aloiva.
 
  • Thanks
Reactions: DSN
Back
Top Bottom