mgogoone
JF-Expert Member
- Dec 28, 2015
- 2,900
- 2,100
Making Tanzania Great AgainMAKE AMERICA GREAT AGAIN
MTGA #hapa ni kazi tu.
Making Tanzania Great AgainMAKE AMERICA GREAT AGAIN
Making Tanzania Great Again
MTGA #hapa ni kazi tu.
Kwani Tanzania ilikuwa great? kama ilikuwa great ni lini na watu wake walinufaika na huo ugreat?Making Tanzania Great Again
MTGA #hapa ni kazi tu.
Hawa jamaa wanajikuta wana Strong Democracy kuliko nchi yoyote duniani ila wakati huu wameingia cha kike Donald Trump anawaonesha the real Meaning of democracy walizoea watu wanaowapenda wao ndio wanapata support ya wananch saiv upepo umegeuka..bado marekani haijakomaa kidemokrasia.. inchi iliyokomaa kidemokrasia inafanya maamuzi kupitia sanduku la kura. Sasa hawa wanaoleta vurugu kumpinga Trump inaonyesha jinsi gani Marekani haijakomaa kidemokeasia.
Hawa wachache wanampinga ila wengi wanamkubali ndo maana anaongoza majimbo mengi, naona wamesahau kanuni muhimu ya demokrasia inayosema wengi wape. Wengine wakaiita demokrasia ni udikteta wa watu wengi.
Jambo la pili tunalojifunza ni mpasuko wa chama cha Republican.Hii inavipa funzo vyama vya siasa nchini kuhakikisha vinakuwa na mshikamano wakati wa kampeni za ndani (kura ya maoni) wakati wa kuchagua mgombea urais kupitia vyama vyao. Mipasuko huku Afrika inapelekea kuongezeka kwa vyama vya siasa ambavyo si vishindani bali vinaishia kuwa vioinzani kwa vyama pinzani na sio kwa chama tawala pia inapelekea kuipa serikali mzigo mkubwa wa kuvipa ruzuku vyama hivyo . Sio kama kwa wenzetu Wazungu wao wanahubiri mfumo wa siasa ya vyama vingi ikiwa wao wanavyama vichache tuu (U.S wana viwili. ie Republican & Democratic) UK ie Labour, Conservative & Liberal Democrats) German ie CDU, SPD & CSU na vingine vidogo ambavyo vinatengeneza coalition na vyama vikubwa)
kura ndo mwamuzi, sio waandamane halafu kura wasipige
[emoji106] [emoji106] [emoji106] [emoji106]Hizo fujo niza kuchonga tu, ma neocon wanaogopa sana kupoteza ulaji wao waliozoea kupigia debe viwanda vya kuhunda silaha, mabenki ya kinyonyaji na lobbying za Wayahudi, group hilo ni la hatari sana - ndio wachochezi wakubwa wa vita visivyo kwisha Duniani, kila siku wanabuni adui wapya ili wapate kisingizio cha kuhunda silaha mpya zosizo za lazima lengo lao wanataka Serikali ya Merikani iwe inatenga budget kubwa kwa lengo la ulinzi, kumbe lengo lao.ni kunufaisha makampuni ya kuhunda silaha.
Trump amesema ana pesa nyingi hivyo hakuna kumpuni yoyote ya kuhunda silaha au ma lobbyists wowote wanaweza kumuweka mfukoni na kufanya wapendalo chini ya uongozi wakr, amesema ujinga huo ataufutilia mbali na kutafuta amani ya kudumu Duniani, ataelewana na Wachina, Warusi, Iran nk.
Msimamo huo wa Trump ma neocon hawaupendi hata kidogo, wamefikia hatua ya kutishia kumpigia kura Clinton kama Trump atapata tiketi ya kuongoza chama cha Republican!! Vitisho hivyo sioni kama vinaweza kubadirisha chochote kwa kuwa Trump ana wafuasi wengi, kama ni suala la u racism hata Clinton anao she is even worse, linapokuja suala siasa ya mambo ya nje yeye ana msimamo mkali na anapendelea sana vita na fujo katika azma yake ya kufikia malengo yake katija foreign policy, halafu kampein zake zinagharimiwa na wenye viwanda vya silaha,mabenki nk. hao ndio wabataka kumuendesha kama robot afanye watakayo wao na sio wapiga kura wa Merikani.
Kusema kweli Wamerika wakifanya makosa wakam-damp Trump watakuja kujuta hapo baadae, chini ya Clinton kuna uwekano mkubwa vita ya III ya Dunia kulipuka chini ya utawala wake.
Kipi hcho ni kikundi cha propaganda cha obama??
Khaa !!!! Kumbe haya mambo yakuzomea yapo hadi marekani nilijua ni kwa akina zitto tukura ndo mwamuzi, sio waandamane halafu kura wasipige
Erijo hivi kweli huwezi kuona nchi yetu ilivyo Na utajiri wa kila aina?Kwani Tanzania ilikuwa great? kama ilikuwa great ni lini na watu wake walinufaika na huo ugreat?
Usinukuu nukuu za watu zilizo irreverent kwa Tanzania, Donald John Trump anaona America imepoteza ukuu na ushawishi wake kama taifa kubwa duniani sasa anajinadi kuwa atarudisha heshima na ukuu wa taifa lao.
Obama anahusika vipi hapo? Sijaelewa kabisa. Kwanza yeye hagombei tena. Amewaachia watu wa chama chake wachuane. Vurugu limetokea kwenye kampeni za Trump. Trump amekuwa mshari siku zote tunamwona. Mtu akionekana tu si wa kumsapoti anawaambia watu wake "fanyeni mnavyoona inafaa. mwondoeni" Badala ya kuzungumza na watu na kuwaelewesha. Huoni mambo kama hayo kwenye kampeni za Sanders, kwa mfano. Anapalilia shari, na ndiyo inamtafuna mwenyewe sasa.Wangemkataa kwa sanduku la kura na si kufanya vurugu. Hicho ni kikundi cha propaganda za Obama!
Ubaguzi gan mkuu??Obama anahusika vipi hapo? Sijaelewa kabisa. Kwanza yeye hagombei tena. Amewaachia watu wa chama chake wachuane. Vurugu limetokea kwenye kampeni za Trump. Trump amekuwa mshari siku zote tunamwona. Mtu akionekana tu si wa kumsapoti anawaambia watu wake "fanyeni mnavyoona inafaa. mwondoeni" Badala ya kuzungumza na watu na kuwaelewesha. Huoni mambo kama hayo kwenye kampeni za Sanders, kwa mfano. Anapalilia shari, na ndiyo inamtafuna mwenyewe sasa.
Naona kampeni za republicans zinaingia mpaka kwenye JF. Republicans wameanza kumlaumu Obama ati ndiyo chanzo cha mfarakano katika chama cha Republicans. Lakini kwa hakika ni dhambi ya ubaguzi ambayo ndiyo inawatafuna wenyewe.
Enhee! Sasa ndugu yangu fungua macho na masikio. Je, unajua kwamba Obama alipochaguliwa tu mara ya kwanza, viongozi wa Senate walitangaza kwamba ajenda yao ya kwanza ni kuhakikisha Obama hachaguliwi kwa muhula wa pili? walitangaza kabisa wanataka kuhakikisha kwamba Obama anashindwa ktk kazi. Sikutaniij. Sen. Mitch McConnell alitamka wazi wazi bila kificho. Hebu fikiria tu hapo. Ajenda yao si kutatua matatizo ya Marekani. Na kama unakumbuka 2008 ulikuwa mwaka ambapo matatizo ya kiuchumi na kifedha yalifikia kilele. Sasa, hakuna raisi mwingine amewahi kuwekewa mizengwe ya namna hii toka wameanza mfumo wa maraisi. Kwa nini? Raisi wa kwanza mweusi.Ubaguzi gan mkuu??
Nakubaliana nawe kwamba fujo nyingi ni za kutengeneza duniani. Lakini Trump si wa kuleta amani duniani. Amesema atamwaga mabomu na kuchukua mafuta yao, ataua familia za magaidi. Kauli hizi ni za kibabe na kijambazi. Ni kwamba kama alivyofanya Bush atakuwa anachokoza nyuki tu. Hawezi kuleta amani. Huoni anavyochochea shari katika mikutano yao?Hizi fujo ni za kutengeneza na hakika wala hakuna fujo kama tunavyoonyeshwa nimeangalia ni wahuni tu wachache wametengenezwa na wale Matajiiri wauaji ili wafanye fujo na kupewa attention kwenye media...hawa wazungu wauaji ni hatari walichukua maandamano ya India wakaweka kuonyesha ni Libya hawa ni wauaji walaishazoea uongo na kunywa damu za watu...huyu Trump anasema kwann Sadam aliuawawa?? Kwann Ghadafi auliuwawa?? Walikosa nn na je baada ya kuwaua Dunia imekua salama?? Lakini ujinga huo huo Obama na wenzie wauaji wanaufanya Syria ni vita ya pesa tu..na biashara hawa watu wabaya sna sana...Trump ataifanya Dunia iwe na amani
Watakuwa wanao support ugaidi,maana kuna dini fulani fulani kwao ugaidi ni imani ya kumpeleka mtu mbinguni
Hukumundo afadhali umemjibu.Obama anahusika vipi hapo? Sijaelewa kabisa. Kwanza yeye hagombei tena. Amewaachia watu wa chama chake wachuane. Vurugu limetokea kwenye kampeni za Trump. Trump amekuwa mshari siku zote tunamwona. Mtu akionekana tu si wa kumsapoti anawaambia watu wake "fanyeni mnavyoona inafaa. mwondoeni" Badala ya kuzungumza na watu na kuwaelewesha. Huoni mambo kama hayo kwenye kampeni za Sanders, kwa mfano. Anapalilia shari, na ndiyo inamtafuna mwenyewe sasa.
Naona kampeni za republicans zinaingia mpaka kwenye JF. Republicans wameanza kumlaumu Obama ati ndiyo chanzo cha mfarakano katika chama cha Republicans. Lakini kwa hakika ni dhambi ya ubaguzi ambayo ndiyo inawatafuna wenyewe.