pierre buyoya
JF-Expert Member
- Dec 6, 2015
- 476
- 163
Usiku wa Jana ijumaa ya Tarehe 11 Machi ulikuwa mgumu kwa Mgombea urais wa Marekani kupitia Chama cha Republican, Mfanyabiashara Donald Trump mara baada ya fujo kuibuka mji wa chicago ambapo alitakiwa akafanye kampeni.
Katika hali ya kushangaza maelfu ya wafuasi wa Donald Trump wengi wao wakiwa wazungu walikutana na kundi kubwa la wapinzani wa Mgombea huyo (mchanganyiko wa wazungu na wamarekani weusi) wakiwa tayari kumfanyia fujo akiwasili kuhutubia katika ukumbi wa chuo kikuu cha illinois.
Kutokana na hali hiyo ziliibuka vurugu kubwa kati ya Wafuasi na wapinzani wa Trump pamoja na polisi kitu kilichopelekea kuahirishwa kwa mkutano huo wa kampeni na mgombea huyo kutoweka kusikojulikana.
Kuna kampeni ya chini kwa chini za kumfanyia vurugu mgombea huyo katika majimbo yaliyobaki.