Chezea vyote ila sio kupokea majibu ya HIV

Chezea vyote ila sio kupokea majibu ya HIV

Sazira kwetu

Senior Member
Joined
Aug 23, 2015
Posts
155
Reaction score
104
Habri za leo wana jukwaa?

Nilejee kwenye mada, mwaka jana nilibahatika kupata msichana ambae nilianzisha nae mahusiano ktk harakati za kukoleza mahusiano yetu akadai hawezi nipa tunda mpaka atakapojua hari ya afya yangu, hivyo akapendekeza twende tukapime kama tuna maambukizi ya virus vya UKIMWI ama la.

Nami nikaona jambo jema na la kupendeza ila kabla ya kwenda kupima kaniomba hela ya kusikia nami nikatoa na tukapanga siku ya kwenda kupima.

Siku ya kupima tukaongozana wote mpaka angaza tukafika tukapewa namba na kusubili kuitwa kwenda kupimwa huku tukiangalia tv yenye vipindi vya kuonye adhari na madhara ya UKIMWI.

Mda wa kupima ukafika tukaitwa mmoja baada ya mwingine kufuatana na namba yako uliyopewa.

Wakati wa kupokea majibu ndio ulikuwa mtihan mkubwa kwa bibie, ile tunaitwa tulipofika tukaulizwa je mnataka kuchukua majibu kwa pamoja?
Jibu alilolitoa bibie likaniduwaza na hata mshauri nasaha akastaaju akasema kila mmoja apewe majibu yake, kiukweli nilichukia na kuamua kuondoka.

Mahusiano yakaishia hapo.
 
sasa we ulitaka upokee ya mwenzio kwani wakati wa kupima alikupa damu yake?
 
sasa we ulitaka upokee ya mwenzio kwani wakati wa kupima alikupa damu yake?

Hapana sio hivyo miss chaga,tumeondoka tukiwa na nia moja lengo moja na tena yeye ndiye initiater wa wazo sasa kama tungechukua majibu kila mmoja yake kulikuwa na ulazima gani wa kwenda kupima wote?
Si kila mmoja angeenda kivyake na kurudi na majibu yake.
 
Kwahiyo ushaanza dose za ARV mkuu?

Mkuu mimi sikuwa na tatizo lolote na ndio maana sikutaka kupata majibu ya peke yangu ila yeye sijui alipata status gani ktk majibu hayo,na hata mshauri nasaha akasema kama alijijua anawasiwasi na mienendo yake angepima kwanza then siku hiyo akawa na ujasiri wa kupokea majibu
 
Mkuu yaani toka mwaka jana ndo unakuja kutusimulia leo?

Bora tu alivyokataa.
 
Mwanaume una gubu wewe, susa salama, ukisusa jirani atakula
 
Naona unatafuta huruma yetu baada a kukimbia majibu

anyway idadi ya nilizokimbia majibu ni nyingi kuliko niliyochukua nishawahi hadi kuishia mlangoni
 
Mwanaume una gubu wewe, susa salama, ukisusa jirani atakula

Bora kususa kuliko kufanyiwa yale niliyofanyiwa,eti baby hakuna ku do mpaka kupime haya sasa mwanaume nikasema mwanamke ndiye huyu anayejipenda na anayeipenda afya yake kumbe alitaka kunizingua sasa mim nikaamua kumpotezea na namba yake nikafutilia mbali.
 
Naona unatafuta huruma yetu baada a kukimbia majibu

anyway idadi ya nilizokimbia majibu ni nyingi kuliko niliyochukua nishawahi hadi kuishia mlangoni

Mim sio kwamba natafta huruma la hasha,ila nimeeza tukio lililonipata lkn pia natoa fundisho kuwa kama unasema unataka kupima ukimwi na uwe wa kwanza kupokea ili hata uliyemshawishi ashawishike na aone ni swala la kawaida na ni jema
 
Hapana sio hivyo miss chaga,tumeondoka tukiwa na nia moja lengo moja na tena yeye ndiye initiater wa wazo sasa kama tungechukua majibu kila mmoja yake kulikuwa na ulazima gani wa kwenda kupima wote?
Si kila mmoja angeenda kivyake na kurudi na majibu yake.
khee basi pole aisee......
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom