CHEZEA MACCM wewee!

CHEZEA MACCM wewee!

CHIBUKU

Member
Joined
Nov 3, 2013
Posts
13
Reaction score
1
Hakuna shaka sasa kuwa Chama kikuu cha upinzani nchini (Chadema),kinapitia wakati mgumu sana katika historia ya chama hiki. Jambo moja sina hakika nalo ni kama watavuka salama! Tuwaombee wavuke salama kwa faida ya demokrasia nchini.

Lakini haya yalitabiriwa na viongozi kadhaa wa CCM akiwemo mzee Wasira na Nape. Walisema CDM itasambaratika soon! Nilistuka kidogo niliposikia hawa majabali wakijitapa hadharani, kwa uzoefu wangewastukiza badala ya kutangaza hadharani. Baada ya matamko yao nkaanza kuhisi upinzani nchini una udhaifu mkubwa kiasi kwamba jamaa wanapanga kuubomoa na wanatangaza hadharani wakijiamini Kuwa hakuna kitakachobadilika zaidi ya kipigo tu!

Lakini kubwa hapa kwasasa ni hili linaloendelea wakati CDM wakivuana nguo Ma CCM ynaendelea na ziara zao mikoani tena bila kuongelea lolote linalotokea kwa mahasimu wao!!!!! Wamewapuuza?? Au kwa kujua na kushiriki vurugu hizo ndio maana wamekaa kimya??!!! Au ukimya huu hasa wa Nape na Kinana tafisiri yake nini??!

WASIJE WAKAWA NI WALE MBWA WANAOUMA KIMYAKIMYA!!
 
Chadema siyo vile vyama walivyofanikiwa kuviendesha/kuviua watakavyo,msimu huu wamefeli,mapandikizi yenu yanafukuzwa na Chadema itasonga mbele kwani kama mimi ndiyo kwanza nimechukua kadi,niwe mwanachama kabisa,.
 
Ccm ni wauaji wa demokrasia nchi hii.tunajua kitu alichofanya nyerere uchaguzi wa zanzibar 1995.pia walichokifanya kwa cuf bara na hata hili la cdm ndio wachawi na kwa kukaa kwao kimya ni kujidanganya kuwa adui wa kuchukiwa kwao ni upinzani.ccm haipendwi tena kwa sababu nyingi ikiwepo wizi uongo na ahadi hewa huku kundi kubwa la vijana likiwa mitaani na mwisho wa ccm ni tume huru na uandikwaji upya wa daftari la kudumu la wapiga kura.
 
Chadema haitasambaratika, bali ni chuma kinachopita katika tanuri/tanuru la moto mkali ili kukiimarisha! Haitakufa ni mapito tu! Watanzania wa leo si wale wa enzi za NCCR-MAGEUZI na mzee Mrema! Tujipe muda kuthibitisha haya.
 
Zitto Kabwe Akerwa na Siasa za Majungu CHADEMA


Posted by Jewajua Kweli at 31 October, at 08 : 51 AMPrint
[Translate]


NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Zitto Kabwe, ameelezea kukerwa na siasa za majungu na vikao vinavyoishia kupigana ndani ya chama chake na badala yake amewataka viongozi wenzake kuelekeza nguvu kwa wanachama, kwani malumbano hayatakijenga chama.
Zitto, ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, alitoa kauli hiyo jana, baada ya RAI Jumatano kutaka kujua msimamo wake kutokana na kuhusishwa kuwa nyuma ya usaliti anaodaiwa kuufanya Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba.
Katika majibu yake hayo aliyoyatoa kwa njia ya mtandao, Zitto alisema wanaojaribu kumhusisha na suala la Mwigamba ni kawaida yao kupenda kumhusisha na mambo yasiyomhusu.
"Mwigamba ni Mwenyekiti wa chama wa Mkoa mwenye utashi wake wa kisiasa. Ana uwezo wa kusimama mwenyewe. Siyo kila mtu mwenye mawazo yake anatumika. Sasa hao wanaomtuhumu Mwigamba wao wanatumiwa na nani?" alihoji Zitto.
Kuhusu hoja kwamba sakata hilo la Mwigamba chanzo chake ni msuguano wa kuwania nafasi ya uenyekiti kati yake na Mbowe, Zitto alisema uchaguzi ndani ya chama haujatangazwa, kwa hiyo yeyote anayezungumzia kugombea au la anavunja kanuni za uchaguzi.
Katika hilo, Zitto alisema hahitaji mtu wa kumsemea, kwamba akihitaji uenyekiti wa chama atasema yeye mwenyewe.
"Nina sifa zote, siyo tu za kuongoza chama, bali kuongoza nchi. Nina elimu ya kutosha, nina rekodi ya kazi za kibunge kubwa kuliko wabunge takribani wote wa sasa, kwa miswada binafsi, hoja binafsi na hata kuibua masuala nyeti ya nchi.
"Uadilifu wangu hauna shaka, uzalendo wangu kwa nchi yangu ni wa kupigiwa mfano. Zaidi ya yote, najua kero za wananchi na changamoto zao. Sihitaji kusemewa na mtu. Nikitaka uenyekiti nitasimama mwenyewe," alisema Zitto.
Zitto alisema kitendo cha kutaka kumhusisha na masuala yanayoendelea ndani ya Chadema na kuhusu sakata zima la Mwigamba, ni kutaka kuhamisha mjadala na kumtoa kwenye ajenda ya kuwafuatilia watu wanaodaiwa kuficha mamilioni ya fedha nje ya nchi.
"Kwa sasa nina kazi ya kuhakikisha mafisadi na wahuni ‘criminals' walioficha fedha na mali nje ya nchi wanaibuliwa na kurejesha fedha hizo," alisisitiza Zitto.
Kuhusu madai ya kuchunguzwa na chama chake kama na yeye ni mmoja wa wasaliti, Zitto alisema kuwa hizo ni mbinu za kumuondoa kwenye kazi anayofanya ya kupambana na ufisadi.
"Wanajua nikishika jambo siachi mpaka mwisho, hivyo wanajaribu kutengeneza uongo wanaouita uchunguzi. Watanzania wasipumbazwe na vituko vya siasa vinavyoendelea. Tuendelee kudai Katiba Mpya na kupambana na ufisadi. Kwa Wanachadema tuendelee kujenga chama kwenye kanda zetu. Chama kitakachochukua dola ni kile chenye mtandao mpana kwenda vijijini," alisema.
Zitto aliwataka viongozi wenzake na wanachama wa Chadema kupunguza vikao vya majungu vinavyoishia kupigana na badala yake waende kwa wananchi wakafanye kazi, kwamba malumbano hayajengi chama.
Kwa upande mwingine, chama hicho kimeendelea kusisitiza kuwa madai yote yaliyotolewa na Mwigamba dhidi ya chama chao ni ya upotoshaji, uongo na ya kichonganishi.
Kwa mujibu wa tarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Ofisa Habari Mwandamizi wa chama hicho, Tumaini Makene, wameshangazwa na hatua ya Mwigamba kuendelea kuvunja katiba ya chama kwa kutunga mambo yasiyokuwepo, badala ya kuwasilisha hoja zake kupitia vikao halali vya chama.
Alisema kwa kuwa Mwigamba amekiri mbele ya waandishi wa habari kuwa amevunja katiba ya chama na kukubali kuwa aliandika kwa kutumia jina bandia waraka na kuuweka kwenye mitandao ya kijamii, ni wazi hana lengo zuri na chama chao, hivyo apuuzwe.
Chanzo – Ra
 
Chadema haitasambaratika, bali ni chuma kinachopita katika tanuri/tanuru la moto mkali ili kukiimarisha! Haitakufa ni mapito tu! Watanzania wa leo si wale wa enzi za NCCR-MAGEUZI na mzee Mrema! Tujipe muda kuthibitisha haya.
Marehemu chadema, rest in peace
 
Ccm ni wauaji wa demokrasia nchi hii.tunajua kitu alichofanya nyerere uchaguzi wa zanzibar 1995.pia walichokifanya kwa cuf bara na hata hili la cdm ndio wachawi na kwa kukaa kwao kimya ni kujidanganya kuwa adui wa kuchukiwa kwao ni upinzani.ccm haipendwi tena kwa sababu nyingi ikiwepo wizi uongo na ahadi hewa huku kundi kubwa la vijana likiwa mitaani na mwisho wa ccm ni tume huru na uandikwaji upya wa daftari la kudumu la wapiga kura.

Chadema ni watoa roho kwa tindikali, sumu na mabomu. Walaaniwe daima
 
Chadema siyo vile vyama walivyofanikiwa kuviendesha/kuviua watakavyo,msimu huu wamefeli,mapandikizi yenu yanafukuzwa na Chadema itasonga mbele kwani kama mimi ndiyo kwanza nimechukua kadi,niwe mwanachama kabisa,.
Chadema ni ya kaskaxini, viongozi wanachaguliwa na mtei, tumechoka - makam mwenyekiti, said Amour arf
 
Marehemu chadema, rest in peace

Hayo ni matamanio yako na wenzako. Na yataendelea kubaki matamanio kama fisi amsindikizavyo mwanadamu akidhani mikono yake (binadamu) itadondoka wakati wowote kwa jinsi inavyocheza kwa kadiri anavyotembea. Kumbe ndio anaenda hivyo na hatimaye hufika salama aendako huku fisi akisindikiza........
 
Back
Top Bottom