Chezea First Day!

Wengine wanalalaga wakiwa wameoga kabisa na kuvaa nguo!!!!...Siku tamu sana hii..!!
 
Kuna siku niliambiwa napelekwa nje ya jiji mbali sana aisee na ndio mara ya kwanza kupanda basi sikulala na nilikuwa nimevaa kabisa
 
Hapo mmenikumbusha enzi zangu Miaka hiyo Christmas inaheshima sana,bila nguo Mpya haijawa sikukuu na utahuzunika sana,ukinunuliwa nguo mpya utaificha wasiione washkaji, na unakuwa unaona siku na masaa hayaendi kabisa,yaani usingizi unakuwa wa mang'amng'am kinoma yaani ilikuwa balaa
 
Hahaha kudadeki. Kumbe hiii kitu tumefanya wengi.
 
Usiombe,
Nilipoambiwa nasafiri toka mikoani kuja darisalama kwa gogo. Sikulala, nikamwamsha dingi saa 4 usiku ati tutachelewa gogo lililokuwa linapita saa 12 jioni.
Siisahau siku hiyo
 
Usiombe,
Nilipoambiwa nasafiri toka mikoani kuja darisalama kwa gogo. Sikulala, nikamwamsha dingi saa 4 usiku ati tutachelewa gogo lililokuwa linapita saa 12 jioni.
Siisahau siku hiyo

Hahahaa, eti gogo. Umenikumbusha mbali sana. Enzi hizo advance pande za magharibi mwa TZ. Ilikuwa ni mwendo wa kuzamia tuu gogo.
 
Siku ya kwanza kuja dar (2001) kusoma MUHAS sikupata usingizi kabisa nalala kidogo mara naamka naenda kukagua begi langu.kweli ushamba mzigo
 
Ndoto zinakuwa kibao.....yaani....da!!!
 
Hahahaa, eti gogo. Umenikumbusha mbali sana. Enzi hizo advance pande za magharibi mwa TZ. Ilikuwa ni mwendo wa kuzamia tuu gogo.


Complex;
Kila aliyepanda gogo anazikumbuka raha zake. Haswa kuwakwepa wale ma-tii tii. Mtu unasogea ukihesabu station. Unashuka ghafla na kuwahi kule alikotoka tii tii. Halafu halijai, ni rahaaa
 
Complex;
Kila aliyepanda gogo anazikumbuka raha zake. Haswa kuwakwepa wale ma-tii tii. Mtu unasogea ukihesabu station. Unashuka ghafla na kuwahi kule alikotoka tii tii. Halafu halijai, ni rahaaa


Hahahaaa, ila ilikuwa inatulazimu kuzamia. Maana kipindi kile ndo ilikuwa mambo ya kubook tiketi wiki kabla. Kishuleshule wiki kabla ya shule kufungwa nyumbani unakuwa hujatumiwa nauli ya kurudi. Nauli nilikuwa natumiwagwa siku ya kufunga shule. Sasa shule ushafunga ukae tena wiki kisa tiketi. Huku ukiangalia nauli uliyotumiwa haitoshi kupanda basi, na hata kama inatosha basi ilikuwa ghali sana na ilikuwa inahatarisha kukosa pocket money likizo time.

Lilikuwa ni jambo gumu sana kusubiri, na kulikuwa hakuna namna zaidi ya kuzamia gogo mpaka home.

hahahhaaa, Ila it was sooo funny.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…