Cheza mbali na IT HACKERS wa N/KOREA.

hakufai kule
sijataka hata kujaribu mkuu, ila nilisikia kwa kufanyia marketing ni pazuri sana nadhani freemasons na illuminat wanapatumia kule, ila niliogopa, kuna mtu alishawahi toa uzi kuhusu hii dark web, nikaona wala sigusi
 
Anayebeza wa North Korea huenda hana information za kutosha kuhusu wao.

Leo tujikumbushe matukio yafuatayo ambayo N/korea cyber army wameyafanya.

1. Ransomware attack(wanna cry-2017), katika shambulio hili walikuwa wakiomba fedha kutoka kwa watumiaji wa compyuta walizovamia.

Hata hivyo kuna nadharia kadha wa kadha kuhusu shambulio hili ila makampuni makubwa mawili ya IT, ambayo ni KASPERSKY ya Urusi na kampuni nyingine ya Marekani ambapo zilifanya uchunguzi na kubaini kuwa code za hackers wa Ransomware zilikuwa na mfanano na code za hackers wa N/korea waliohack SONY PICTURES mwaka 2014.

Hakuna ajuaye walipata hard cash ngapi katika ransomware attack ila waliharibu kompyuta nyingi sana duniani.

2. South korea bitcoin hacking.
Hapa wazee wa kazi walivamia mfumo wa bitcoin nchini South Korea na kuondoka na fedha kiasi fulani kwa ajili ya maendeleo yao.

3. BBC RADIO JAMMING(2017).
Hii ni ya juzi juzi tu tena mwezi wa 9 mwaka 2017, ilifanyika baada ya BBC kufungua kituo cha matangazo yao ya redio nchini korea kusini ambayo yalilenga kutoa ufahamu wa demokrasia na jinsi ya kutorokea Korea kusini kwa wananchi wa N/korea.

4. Implanting of Digital sleeper cells in south korean infrastructures.

Katika hili Ushahidi upo ila bado haujatolewa wazi wazi ila wizara ya mambo ya Ndani ya Korea kusini imebaini hivi karibuni kuwa hackers wa N/korea wamevamia mfumo wao wa mawasiliano na kupandikiza vitu ambavyo vitaharibu mawasiliano ya nchi nzima yakiwemo na ya jeshi ktk wakati wa vita.

5. New york federal reserve hacking (hapa waliondoka na milioni 81 za kimarekani baada ya kuhack na kujifanyisha kuwa wao ni Bangladesh Central Bank)

Imeandikwa mahali fulani kwenye makala moja matata, kuwa walitaka kuchukua $1 billion ila walikosea tu herufi moja wakashtukiwa na mfumo wa benki hiyo. Waliandika neno 'fandation' badala ya 'foundation'.

6. BBC TELEVISION NETWORK HACKING(kuna mdau kaielezea hii kwenye thread moja humu jf, itafute)

7. SONY PICTURES HACKING IN 2014.(Na hii pia kuna mdau alielezea humu jf, itafute uisome)

Source: makala hii nimeiandika kutoka vyanzo mbalimbali ila waweza pia itafuta hapa www.independent.co.uk
Hela lazima itawale, ukiona wanakudharau pambana wakuheshimu
 
15 Reactions
Reply
Back
Top Bottom