Cheyo ni 'mlaini' mno kuongoza kamati | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Cheyo ni 'mlaini' mno kuongoza kamati

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tuko, Apr 4, 2011.

 1. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #1
  Apr 4, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 395
  Trophy Points: 180
  Wakati viongozi wenzake wa kamati za watch dogs, Zitto na Mrema wakiungana na maelfu ya Watanzania kupendekeza sheria za kudhibiti ubadhirifu wa fedha za umma, ikiwemo kuzipa kamati hizo uwezo wa 'kuarrest' na kushitaki, Cheyo anaonekana bado ana 'huruma' na wabadhirifu.

  Msimamo wa Cheyo alioubainisha asubuhi ya leo Channel ten ni kuwa utaratibu wa sasa kuwa wabadhirifu wanaitwa na kuhojiwa tu na kamati hizo, ni 'mzuri sana'. Anatoa ushuhusa kuwa waliwahi kumbana mhasibu mmoja hadi akaanguka akafa!

  Anasema kuwa kazi ya bunge ni kutunga sheria na kuisimamia serikali, so lisijihusushe na kukamata na kushitaki watu.

  Cheyo anashindwa kufahamu kuwa kati ya sababu kubwa zinazowafanya watanzania kuwa masikini (ambapo Pinda na Kikwete walishakiri kuwa hawazifahamu) ni matumizi mabaya ya fedha za umma, hivyo ashiriki kuhakikisha sheria za udhibiti zinabana pande zote, kuanzia serikali yenyewe (Takukuru na Polisi), CAG na kamati za bunge.

  Nilijiuliza hivi Cheyo amewaona Waganda kuwa Wendawazimu pale walipoweka sheria kuwawezesha kamati za bunge kearrest na kushitaki?

  Cheyo is too soft to lead a watch dog committee...
   
 2. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #2
  Apr 4, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Huo ulaini ndiyo sifa kuu iliyoifanya serikali kupindisha kanuni za bunge ili Cheyo aendelee kubakia kuwa mwenyekiti wa kamati hiyo ya matumizi ya serikali. Pengine ni vema ikaeleweka ya kuwa Cheyo kwa hulka yake siyo mtu laini kama inavyofikiliwa; ukweli ni kwamba Cheyo wa hivi sasa amelainishwa na fadhila anazopewa ili kulinda ufisadi serikalini. Ikumbukwe huko nyuma mheshimiwa huyo alikuwa na kauli mbiu ya kuwajaza watu mapeza, wabaya wetu wametumia hiyo kauli mbiu yake kumjaza mapesa yeye, ili waweze kumlainisha.
   
Loading...