tanga kwetu
JF-Expert Member
- May 12, 2010
- 2,193
- 1,437
Miaka yangu michache ya utumishi wa umma (miaka nane) nilikuwa nikishuhudia ofisi za serikali ifikapo June mwishoni huwa zinarejesha pesa iliyobaki hazina. Yaani kama hazikutumika kwa sababu yoyote ile. Niliona ipo maantiki kuzirejesha hazina maana ndipo zilipotokea.
Sasa naona kumezuka mtindo wa baadhi ya ofisi za umma (so far ni bunge na Tume ya Taifa ya Uchaguzi,NEC) kurejesha fedha Ikulu pesa iliyobaki hata kabla ya mwaka wa fedha hujaisha i.e 31/6/2016.
Hapa sipingi "chenji" kurejeshwa, bali nashangaa ni vipi zinarejeshwa Ikulu. Sijaona waraka wa hazina unaoelezea haya mabadiliko.
Naomba mwenye kujua anijuze juu ya haya mabadiliko kama yapo.