Cheni za English Gold na kutokwa vipele vingi shingoni

Enny

JF-Expert Member
May 26, 2009
962
130
Kuna baadhi ya watu wakivaa cheni za English Gold hata kwa masaa mawili tu wanawashwa sana na kutokwa vipele vingi shingoni ambavyo ukiona utadhani ugonjwa wa ngozi. Je kuna uhusiano gani hapo?
 
Uhusiano upo, hii maana yake kuwa ana aleji na hivyo vitu hivyo ili kuepusha madhara zaidi ni bora akaviacha kabisa. Nimeishaona watu wengu wenye aleji na hiyo gold ya kuchovya lakini mara tu baada ya kuacha na tatizo linakwisha lenyewe ila kuendelea kung'ang'ana navyo kisa urembo ataja rembeka asivyopenda.

Nina rafiki yangu mmoja yeye alikuwa na tatizo kwenye masikio yalivimba vile vinundu mara tu baada ya kutobo. akafanyiwa operation wakavikata akafikiri tatizo nalo limekwisha akawa anavaa hizi hereni za kuchovya na nyinginezo na akaja toboa tena vitundu vingine viwili kwenye masikio muda si mrefu alikotoboa, alikofanyiwa operation kote vinundu vikavimba kama ndio alitia mbolea. Bahati nzuri alimpata daktari mzuri akamfanyika operation nyingine ila akamwambia kama atakuwa ana uwezo wa kuvaa pure gold masikio yakipona baada ya operation aende akamtoboe na awe anavaa pure gold akaona hatakuwa na huo uwezo uwezo wa kuvaa pure gold. hivyo baada ya kupona hakutoba tena masikio ila siku hizi ameamua kuvaa hereni za kubana naona hizo hazimzuru.
 
Tatizo ni allergy. Suluhisho ni kutovaa hivyo vidani

Hiyo ndio tiba sahihi...nimeshaona wengi tu wenye tatizo la allergy kwa sababu ya cheni 'feki' za gold, kwani wantumia sana synthetic materials ambazo watu wengine huwa na allergy nazo.
 
Mshukuru Mungu maana kakuokoa na gharama za gold
hiyo siyo gold ndugu yangu na bei za hizo cheni ni ndogo sana hata wamachinga wanauza. Hivyo mtu kama ana allergy ya hizo cheni inabidi avae pure gold ambayo ni ghali. Hivyo hajaokolewa na gharama
 
Hizo english gold products ni mchango wa vitu ving hasa hiz za pande zetu za DRC, Ukijipaka na mavipodozi reaction yake ndo hyo upele. Solution acha au angalia ni product ya wapi !kama fasi ya congo na west africa mmmh.
 
Kuna baadhi ya watu wakivaa cheni za English Gold hata kwa masaa mawili tu wanawashwa sana na kutokwa vipele vingi shingoni ambavyo ukiona utadhani ugonjwa wa ngozi. Je kuna uhusiano gani hapo?

English gold ni nini? As far as i understand chain au earing ya gold haiwezi kuwa pure gold,it needs other elements ili iweze kuwa moulded into a chain or earing.Only GOLD BARS are pure gold
 
Back
Top Bottom