Chenge si jasiri wala smart, anadekezwa na kutengenezewa upenyo

Mtu smart hawezi kutoa kauli kama ile ya "vijisenti tu" kwa nchi masikini na hela kama ile.

Nawalaumu sana majambazi wa Tanzania kwa kushindwa kazi yao, wameshindwa kwenda kwa Chenge kuiba hata baada ya kualikwa kwamba huyu mtu ana mipesa ningi sana - malaki ya dola za Marekani- na zile hela zilikuwa vijisenti tu.

Nchi nyingine ukijitapa vile unatekwa nyara mpaka familia yako itoe hela.
 
Hili lapoti kweli linateleza kama mafuta, ila watalipata tu, lakini si lingestaafu tu litafune midola yake! Linapokuwepo mle CMM lachafuwa na kuleta harufu mbaya, liende likavinjari na totoz sasa kabla ya kukosa meno ya kuvunja mfupa...
 
mkuu hili joka likitembea linavuta kenge,mamba na madudu mengi mengine hakika hakuna wa kuligusa...na likipigiwa sana kelelee linaenda zake state linajitangazsia msiba over
 
Hata Mgombea kiti cha Urais CCM alipokwenda SIMIYU hakumpa hata mkono wala kumnadi lakini wana Bariadi/simiyu walimpa kura zote, huyu kwenye nyoka wa makengeza
 
Namjua Andrew John Chenge vya kutosha. Ingawa sikumkuta pale UDSM, nilimkuta chamani CCM tangu katikati ya 1980's nilipojiunga na CCM na kuendelea kuwa naye hadi leo. Kaka yangu Chenge nimewahi kufa nya naye kazi mbalimbali za kisheria wakati huo nikiwa Serikalini, yeye akiwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Hata kazi za kichama, tuliwahi mara kadhaa kufanya kazi pamoja ili kufanikisha hili au lile. Kwa nimjuavyo, Chenge ni mtu wa kawaida. Ni muoga kama wengi wetu. Hachelewi kujaa mashaka juu ya hatua za kisheria na kinidhamu juu yake na kadhalika. Chenge hana ushupavu, uhodari, usmart wala uthubutu anaopewa kwenye media.

Kwa Serikali, Chenge ni mdogo kama chembe ya haradari. Chenge, kama alivyo Lowassa na Rostam ni wazito midomoni lakini wepesi kisiasa, kisheria na kimaisha. Chenge anadekezwa na kupewa upenyo tu. Nitawapa mfano mdogo. Katika mambo anayohusishwa nayo ya makinikia, Chenge anayatoka kirahisi kwakuwa kuna upenyo.

Mambo yanayomhusisha ni mambo yaliyotokana na Uanasheria wake Mkuu wa Serikali. Alikuwa Mshauri. Alikuwa akitoa ushauri juu ya mambo hayo ya madini. Hivi, ushauri ni jambo la lazima kukubaliwa? Hivi, aliyeshauriwa hakuwa katika nafasi ya kukataa? Huu ndiyo upenyo ninaousema. Kwanini yasingetafutwa mambo direct yaliyomhusu na kumhusisha nayo?

Amini nawaambia, Chenge ni mwepesi kama unyoya. Mbele ya Serikali, na vyombo vyake, hakuna mbishi,jasiri wala smart. Lakini, Chenge anadekezwa, anabebwa na anatengenezewa upenyo kila mara anapotajwa kwenye kashfa za kifisadi. Hana upekee wowote wala si nyoka kama anavyotamba kila mara.

Bastola ya nini tena jamani!?

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
Acha uongo wewe sio ccm ni chadema ila ni kweli wewe ni mwanasheria ila hujawahi fanya kazi serikalini.acha uongo mbona kama unamjua mbona huko unakofanya wewe bado ni junior lawyer ?
 
CHENGE anakamatika vema ila anasema hatuwezi kumfunga kwa kutusainisha mikataba feki.Sasa JIULIZE anajivunia nini!!!???
Ni kweli anakamatika, hofu yangu wasukuma watakuelewa? Inaweza kuzalisha kitu kingine, bashite kulindwa Vs chenge and company. Stop there kulinda Chama hususan usukumani.
 
Hivi hawa jamaa wanoshtukiza kule mkuranga wapo wapi? Kwanini wanadili na watendaji badala ya kudili na watu kama chenge? Hili nchi tuna laana kwa kweli
 
Namjua Andrew John Chenge vya kutosha. Ingawa sikumkuta pale UDSM, nilimkuta chamani CCM tangu katikati ya 1980's nilipojiunga na CCM na kuendelea kuwa naye hadi leo. Kaka yangu Chenge nimewahi kufa nya naye kazi mbalimbali za kisheria wakati huo nikiwa Serikalini, yeye akiwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Hata kazi za kichama, tuliwahi mara kadhaa kufanya kazi pamoja ili kufanikisha hili au lile. Kwa nimjuavyo, Chenge ni mtu wa kawaida. Ni muoga kama wengi wetu. Hachelewi kujaa mashaka juu ya hatua za kisheria na kinidhamu juu yake na kadhalika. Chenge hana ushupavu, uhodari, usmart wala uthubutu anaopewa kwenye media.

Kwa Serikali, Chenge ni mdogo kama chembe ya haradari. Chenge, kama alivyo Lowassa na Rostam ni wazito midomoni lakini wepesi kisiasa, kisheria na kimaisha. Chenge anadekezwa na kupewa upenyo tu. Nitawapa mfano mdogo. Katika mambo anayohusishwa nayo ya makinikia, Chenge anayatoka kirahisi kwakuwa kuna upenyo.

Mambo yanayomhusisha ni mambo yaliyotokana na Uanasheria wake Mkuu wa Serikali. Alikuwa Mshauri. Alikuwa akitoa ushauri juu ya mambo hayo ya madini. Hivi, ushauri ni jambo la lazima kukubaliwa? Hivi, aliyeshauriwa hakuwa katika nafasi ya kukataa? Huu ndiyo upenyo ninaousema. Kwanini yasingetafutwa mambo direct yaliyomhusu na kumhusisha nayo?

Amini nawaambia, Chenge ni mwepesi kama unyoya. Mbele ya Serikali, na vyombo vyake, hakuna mbishi,jasiri wala smart. Lakini, Chenge anadekezwa, anabebwa na anatengenezewa upenyo kila mara anapotajwa kwenye kashfa za kifisadi. Hana upekee wowote wala si nyoka kama anavyotamba kila mara.

Bastola ya nini tena jamani!?

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
Mzee naona povu linakutoka kwa nyoka wa makengeza.
 
gz9.jpg
 
Mkuu naomba uache kumfananisha chenge na vikashfa vyako vya kitoto hivi hujui kuwa kashfa yoyote dhid yake inapoteza umaarufu haraka sana !! acha kucheza na role model wangu mzee Chenge huyu ni untouchable kwenye ishu za kitoto km hizo km huamini endelea kusubiri.
 
Back
Top Bottom