Chenge na Tibaijuka wataigharimu CCM

Chenge na Tibaijuka wataigharimu CCM

Ukweli ndiyo huo,zile hela walipiga wengi, chenge na mwenzie tibaijuka Hilo wanalijua na ndiyo maana wanakomaa.hela zilizopigwa stanbic bank mpaka Leo hakuna majina yaliyowekwa hadharani na ndiyo noma,Tunafahamu tu wa mkombozi bank
 
Huu ni mwaka wa uchaguzi mkuu wa Rais,Wabunge na Madiwani. Wakati wa uchaguzi mkuu kama huu,chama kinapaswa kuwa safi na imara kama chuma cha pua. Chama cha Mapinduzi kitaathiriwa vya kutosha na sarakasi za Andrew John Chenge na Anna Kajumulo Tibaijuka juu ya sakata la Escrow. Sarakasi wanazozicheza mbele ya Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma chini ya Jaji Kiongozi Mstaafu,Hamisi Msumi.

CCM iliamua vyema.Ilipokea ubunifu/ushauri toka kitengo cha Itikadi/Propaganda kwamba ni vyema Chenge na Tibaijuka 'washughulikiwe' ili kukisafisha na kukinusuru chama kuelekea Oktoba. Lengo lilikuwa zuri.Ni kuwaaminisha watanzania kwa CCM hailei wakiuka maadili ya chama na kiuongozi wa nchi. Kushughulikiwa kwa Chenge na Tibaijuka kungekuwa msaada mkubwa kwa chama.

Mpango wa chama unaelekea kubuma. Kukwama hadi kiama. Matendo na maneno ya Chenge na Tibaijuka mbele ya Tume ya Jaji Msumi yanadhihirisha kukwama kwa mpango huo. Ijulikane kuwa CCM ina faili la kila mmoja wao lenye nyaraka zote. Tume ya Jaji Msumi itaishia kutoa mapendekezo ya siri kwa mamlaka za kiserikali juu ya Chenge na Tibajuka ambayo pia si msaada kwa chama.

Bado Ngeleja!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

You are absolutely right; Chenge na Anna watakigharimu Chama; nionavyo mimi hayo yatakuwa malipo sahihi kwa Chama chenu kutokana na tabia, mila na desturi ya CHAMA ya kulindana; kufumbia macho maovu; kukosa uthubutu wa kukemea maovu na kuchukua maamuzi magumu na wanachama wote kujihusisha na uovu; kwa kuwa hakuna aliye msafi wa kuweza kumfunga paka mwenzie kengele shingoni; ndio maana Anna na Chenge wanafanya wanayoyafanya kwenye tume!
 
Tatizo viongozi wetu si wasikivu

Mzee Tupatupa
 
  • Thanks
Reactions: MTK
Tatizo viongozi wetu si wasikivu)
Mzee Tupatupa

Kama sio wasikivu; Then they should get ready to bear the consequences; Choices have consequences; kama wamechagua kufanya ufisadi na kufumbia macho uovu, athari zake ndio kama hizo ulizosema Vuta; Hivyo ndivyo maisha yalivyo; Adhabu fulani fulani ziko ndani ya kitendo chenyewe kama mtoto kung'ang'ania kuchezea moto; anaadhibiwa pale pale; moto unamuunguza mara moja!
 
Hakuna athari yeyote kwa sababu majimboni kwao wananchi wamejaa tongotongo..nlikuwepo jimbon kwa chenge(Bariadi Magharibi) kule jamaa ni nyoka kweli kweli..mikutano yake ya hadhara ni kufuru,watu wanamshangilia mwanzo mwisho hata alipotoa kauli ya nyoka msaka pesa wasukuma wamemsifu na kumshangilia wanasema ubunge ni mali yake hadi atakapoamua kuacha mwenyewe

Aliewaloga wananchi jimboni kwa chenge alikufa bila kuacha dawa
 
Ukweli ndiyo huo,zile hela walipiga wengi, chenge na mwenzie tibaijuka Hilo wanalijua na ndiyo maana wanakomaa.hela zilizopigwa stanbic bank mpaka Leo hakuna majina yaliyowekwa hadharani na ndiyo noma,Tunafahamu tu wa mkombozi bank

majina ya stanbic yanalikana inasubiriwa tu wakati kampeni zinaenda ngwe ya lala salaam video (footage) toka CCTV za stanbic zirushwe live humu!
 
Chenge na Tibaijuka wako sahihi kabisa,na waendelee kufanya hivyo..hawezi kuendelea kufanywa kafala wakati wengine walipiga hela ndefu kabisa wameachwa,waitwe wote mpaka wale wa STANBIC,waitwe wapwa na wakwee,,sio kumuonea mama wa watu na Chenge,,,Chenge mwaga ugali ,,wao si wanataka kumwaga mboga
Mkuu hapa cchenge hamwagi ugali bali anatumia sheria mbovu walizozitunga wao kujilinda,ili
kuwalinda wenzake,angelikubali kuhojiwa na kusema au kuhoji wengine wako wapi? tungesema anamwaga
mboga.Huyu ameishajitaja kuwa ni joka lenye makengeza anatumia ujanja wa nyoka
kujiokoa na kuokoa wenzake.
Ni afadhali mama Tibaijuka ameanza vizuri kwa kusema milioni kumi ni hela ya
mboga,kwa wanafasihi watamwelewa kwamba kama hiyo ni ya mboga basi
kuna waliochukua za kununua nyumba mbona hawapo hapa?
Huyu wakimhoji vizuri ndo anaweza kumwaga ugali,
Huyo mwenzake anayekataa kuhojiwa anatumia dhana ya ''Ni upepo tu utapita''.
 
mkuu uko sahihi, lakini Mzee wa Joka lenye makengeza anawasumbua kwa sababu anaona utani tena wa kifedhuli,,aliyewatuma wamhoji ndio aliepata mgao mkubwa...aliyewapa hela wala hajatumiwa hata message kuulizwa,sasa si kiini macho hiki,Chenge muache aendelee kudinda ili hili sakata lisiishe,na mwisho wataumbuana tu hata kama itakuwa ni serikali ijayo
 
Sakata la escrow Chenge,Tibaijuka na Ngeleja wamevuliwa ujumbe wa Halmashauri kuu CCM.Source taarifa ya habari ITV.
 
CCM haiwezi kumwadhibu Chenge kwa sababu huyo ndiyo mfano mzuri kwa CCM. Umoja, mshikamano na nguvu ya CCM imejengwa katika uovu. Aliye muovu zaidi ndiye hustahili kuwa mfano na kiongozi wa walio na uovu mdogo.

CHENGE NI MWENYEKITI WA KAMATI YA MAADILI YA CCM. UNADHANI KWA NINI ALIPEWA NA KUAMINIWA NA CCM KUONGOZA KAMATI YA MAADILI YA CHAMA? UKITAKA KUJUA MAADILI YA CCM MTAZAME CHENGE, MAANA HUYO NDIYE KIOO CHA CCM KATIKA MAADILI.

Huu ni mwaka wa uchaguzi mkuu wa Rais,Wabunge na Madiwani. Wakati wa uchaguzi mkuu kama huu,chama kinapaswa kuwa safi na imara kama chuma cha pua. Chama cha Mapinduzi kitaathiriwa vya kutosha na sarakasi za Andrew John Chenge na Anna Kajumulo Tibaijuka juu ya sakata la Escrow. Sarakasi wanazozicheza mbele ya Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma chini ya Jaji Kiongozi Mstaafu,Hamisi Msumi.

CCM iliamua vyema.Ilipokea ubunifu/ushauri toka kitengo cha Itikadi/Propaganda kwamba ni vyema Chenge na Tibaijuka 'washughulikiwe' ili kukisafisha na kukinusuru chama kuelekea Oktoba. Lengo lilikuwa zuri.Ni kuwaaminisha watanzania kwa CCM hailei wakiuka maadili ya chama na kiuongozi wa nchi. Kushughulikiwa kwa Chenge na Tibaijuka kungekuwa msaada mkubwa kwa chama.

Mpango wa chama unaelekea kubuma. Kukwama hadi kiama. Matendo na maneno ya Chenge na Tibaijuka mbele ya Tume ya Jaji Msumi yanadhihirisha kukwama kwa mpango huo. Ijulikane kuwa CCM ina faili la kila mmoja wao lenye nyaraka zote. Tume ya Jaji Msumi itaishia kutoa mapendekezo ya siri kwa mamlaka za kiserikali juu ya Chenge na Tibajuka ambayo pia si msaada kwa chama.

Bado Ngeleja!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
 
CCM bado Tuko imara sana hasa tukimchagua huyu Tanzania itakuwa nchi ya neema maana watoto wetu watakuwa wanavimbiwa kwa kunywa maziwa , mikate na siaji

11009850_792272034188319_6833047830999452455_n.jpg
Wassira ana uwezo mkubwa kuliko Lowasa,Dr Slaa,Mbowe na Lipumba. Akipewa Nchi leo ataiweka sawa. hakuna Ufisadi wala lelemama.
.View attachment 230793
 
Msikubali,wamezidi kunyanyasa watu na kutoa makafara kwa uonevu wakati wao ndio wezi wakubwa,msikubali waburuzeni wasiwanyanyase na this time wakiwauwa tutajua tu na sisi na wao.

Wamesha zoea kuua watu na kutoa makafara wakakti wao ndio wacheza dili wakubwa na wanajificha nyuma yenu

haiwezekani tupige kelele kwa billion 7 alizo gawa rugemalila tena kwa kulipa kodi kubwa billion 37 wakati kuna mtu aligawa billion 73 tena kwa pesa ambayo haikulipiwa kodi na mpaka sasa ivi hakuna anaye sema chochote juu ya hili,kwangu mimi namwona ruge bonge la mzalendo.

Mimi naomba nyie ngereja,chenge,tibaijuka msikubali kuburuzwa waaibisheni hao,fichueni maovu yao wamezoea,najua mnajua mengi hasa chenge ,walipueni tu kama noma na iwe noma
 
joharry Unawaonea huruma? 'Wote' hao ni wezi na hawatakiwi kuwa na nafasi yoyote katika jamii!
 
Last edited by a moderator:
Nonesense... Fisadi aliyejulikana Kumlipua Fisadi asiyejulikana. Wanaojulikana Mpaka sasa Washughulikiwe na wakipatikana wengine Wapewe haki pia.
 
Back
Top Bottom