Chenge na Tibaijuka wataigharimu CCM

Chenge na Tibaijuka wataigharimu CCM

...sheria za nchi hii ni dhaifu au halifu kama uzi wa buibui ambao hukatwa na nzi mkubwa na kunasa nzi mdogo tu...

Kuwa na sheria ni jambo moja na kusimamia matumizi yake ni kitu kingine. Kinachokusekana ni usimamizi, matumizi na tafsiri sahihi ya sheria kwa maslahi ya uma. Siyo kupindishapindisha sheria kwa kuangalia nani anatuhumiwa!
Kwa sheria hizi hizi, tukipata viongozi wazuri, mambo yatakwenda vizuri kabisa.
Tukiwa na viongozi waovu, hata ubadilishe sheria iwe kali kiasi chochote, bado watapindisha kwa maslahi yao!
 
Mkuu nadhani upo sawa,
Na mimi naomba kuongezea kwamba ccm si mara ya kwanza kushindwa.
kumbuka dhana ya kujivua gamba, na hawa wanaamini itashindikana kama ilivyoshindikana
ile ya kwanza.
Mimi kama mtanzania nimejifunza kuwa mh.Chhenge siyo msafi
kama wengi walivyodhani na kumpa nafasi za uongozi wa kamati
za bunge hata na ubunge,kwa sababu.
Nafasi hii ya kuhojiwa ilikuwa fursa muhimu ya kujisafisha
kama hayo makandokando yanayomkabili ni ya kusingiziwa.

Ikumbukwe kwamba Chennge ni mwanasheria aliyebobea
Hawezi kuogopa kuhojiwa kwa mantiki ya hofu ya kukabiliana na majaji.
Kukataa kwake kuhojiwa kwa kuzitumia mahakama zetu
kunaonyesha anajua jinsi alivyovuruga na hawezi kuukwepa mkono
wa sheria,maana anaijua kwamba ni msumeno hivyo anaamua
kupiga danadana ilimradi muda uende na litatokea jingine kama
lile la amboni na watanzania watasahahu na maisha yataendelea kama kawaida

Nawaomba wananchi tuone umuhimu wa kufanya maamuzi magumu
maana tuliowaamini hawaaminiki tena,tuchukue hatua ya kubadilisha
uongozi si serikali tu bali na mahakama mfumo wake ufumuliwe
na kuundwa upya.
 
Ni wazi kuwa pengo la kipato miongoni mwa Watanzania ni kubwa sana sasa. Ninachofikiri ni kuwa mtumishi wa umma inatakiwa maisha yake yaakisi (reflect) hali halisi ya nchi na wananchi anaowatumikia. Sisi mtaani kuna jamaa ambaye ni miongoni mwa watu wenye maisha mazuri sana maana anafanya kazi kwenye taasisi za serikali, nilivyofuatilia kwa wajuzi wa mambo ya mishahara ya umma walisema mshahara wake analipwa kama TSh. 850,000/- kwa mwezi.

Hoja yangu hapa ni Prof. Tibaijuka kusema kuwa "10,000,000/- ni pesa ya mboga", jamani wajuzi wa mambo hii mboga inayogharimu kiasi hiki ni mboga gani hapa dar es Salaam/Tanzania au hata Afrika Mashariki kama sio duniani!?

Sikuelewa pale JK alivyoahidi kutengeneza mamilionea kwamba wangelikuwa katika sura hizi!
 
Ijulikane kuwa CCM ina faili la kila mmoja wao lenye nyaraka zote.

Acheni unafiki wa kumfanya kila mtanzania ni zuzu, hayo mafaili ni mapambo huko kwenye shelves zenu? Ama kilichomo humo kimtaja bwana Andrea kwa sifa za malaika?

Mbona pamoja na hayo mafaili ni mbunge kupitia chama chenu? Tena come october atakuwa huko bariadi ya mashariki akipeperusha bendera yenu kama mgombea. Mbona pia mlimpa wadhifa kuwa kiongozi wenu wa maadili(sijui maadili gani), bungeni huko mkampa nafasi nyeti ya kuongoza kamati ya budget na hata ndani ya BMK mkamtunuku ile tunu ya kuichora Tanzania aitakayo/muitakayo?

Ni kipi hasa unachojaribu kutuambia juu ya hayo mafaili? Come on mzee!!!!
 
Chenge na Tibaijuka wako sahihi kabisa,na waendelee kufanya hivyo..hawezi kuendelea kufanywa kafala wakati wengine walipiga hela ndefu kabisa wameachwa,waitwe wote mpaka wale wa STANBIC,waitwe wapwa na wakwee,,sio kumuonea mama wa watu na Chenge,,,Chenge mwaga ugali ,,wao si wanataka kumwaga mboga
 
Na kwa tabia za huyu Binti yako usitegemee kupata kitu kinaitwa mahari hapo! Nani atakubali kuoa binti wa aina hiyo? Huyo acha akacheze kigodoro tuu. Pole mzee wetu, watoto wengine sio riziki.

Mabinti kama laki si pesa kwa taarifa yako huwa wana figure za kuua mtu, wanaume lazima tupange foleni.
 
Last edited by a moderator:
sakata zima linatokana na udhaifu wa sheria zetu na muundo wa utawala wa nchi yetu. Wananchi tulipendekeza kuweko na mgawanyo wa madaraka kati ya Wananchi wanowakilishwa na Bunge, na serikali inayokabidhiwa uendeshaji wa nchi. CCM mkakataa mgawanyiko huo. Mnataka serikali iwe sehemu ya Bunge. Ni panya gani amfunge paka kengele? Hicho ndicho kitandawili ambacho katiba pendekezwa inataka na wajukuu wetu wakikute!
 
Baada ya miaka hamsini watakaokuwepo watashangaa sana jinsi tunavyofanya maamuzi yetu na aina ya viongozi waliokuwepo,watashangaa zaidi pale watapoona jina la Chenge kama mwenyekiti wa kamati za bunge hasa ya uandishi wa katiba!!
 
Chama tawala wengi wameshakugharimu hao wametolewa kama muhanga tu...
 
Iwagharimu mara ngapi huyu mmoja anajiita nyoka mjanja mwenye makengeza na huyu mwingine anasema milioni kumi ni hela ya mboga si matusi haya kwa watanzania.wacha tusubiri hiyo mwezi oktoba itajulikana tu.
 
Huu ni mwaka wa uchaguzi mkuu wa Rais,Wabunge na Madiwani. Wakati wa uchaguzi mkuu kama huu,chama kinapaswa kuwa safi na imara kama chuma cha pua. Chama cha Mapinduzi kitaathiriwa vya kutosha na sarakasi za Andrew John Chenge na Anna Kajumulo Tibaijuka juu ya sakata la Escrow. Sarakasi wanazozicheza mbele ya Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma chini ya Jaji Kiongozi Mstaafu,Hamisi Msumi.

CCM iliamua vyema.Ilipokea ubunifu/ushauri toka kitengo cha Itikadi/Propaganda kwamba ni vyema Chenge na Tibaijuka 'washughulikiwe' ili kukisafisha na kukinusuru chama kuelekea Oktoba. Lengo lilikuwa zuri.Ni kuwaaminisha watanzania kwa CCM hailei wakiuka maadili ya chama na kiuongozi wa nchi. Kushughulikiwa kwa Chenge na Tibaijuka kungekuwa msaada mkubwa kwa chama.

Mpango wa chama unaelekea kubuma. Kukwama hadi kiama. Matendo na maneno ya Chenge na Tibaijuka mbele ya Tume ya Jaji Msumi yanadhihirisha kukwama kwa mpango huo. Ijulikane kuwa CCM ina faili la kila mmoja wao lenye nyaraka zote. Tume ya Jaji Msumi itaishia kutoa mapendekezo ya siri kwa mamlaka za kiserikali juu ya Chenge na Tibajuka ambayo pia si msaada kwa chama.

Bado Ngeleja!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
na makundi ya waasi yalitokea kwa mtindo huo walionacho na waliokosa ss majibu ya hela za mboga million kumi waliolala na njaa wanajisikiaje wakisikia hayo kama mtu anachezea ten million wanahatarisha taifa letu kuingia ktk machafuko
 
Na kwa tabia za huyu Binti yako usitegemee kupata kitu kinaitwa mahari hapo! Nani atakubali kuoa binti wa aina hiyo? Huyo acha akacheze kigodoro tuu. Pole mzee wetu, watoto wengine sio riziki.

Hahahaaaaaaaaaaaaa,duh nilikuwa stressed kweli na hili likazi la leo.Lakini umenifanya na usingizi unitoke kwa kucheka.Asante sana kuniongezea siku:msela:
 
Huu ni mwaka wa uchaguzi mkuu wa Rais,Wabunge na Madiwani. Wakati wa uchaguzi mkuu kama huu,chama kinapaswa kuwa safi na imara kama chuma cha pua. Chama cha Mapinduzi kitaathiriwa vya kutosha na sarakasi za Andrew John Chenge na Anna Kajumulo Tibaijuka juu ya sakata la Escrow. Sarakasi wanazozicheza mbele ya Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma chini ya Jaji Kiongozi Mstaafu,Hamisi Msumi.

CCM iliamua vyema.Ilipokea ubunifu/ushauri toka kitengo cha Itikadi/Propaganda kwamba ni vyema Chenge na Tibaijuka 'washughulikiwe' ili kukisafisha na kukinusuru chama kuelekea Oktoba. Lengo lilikuwa zuri.Ni kuwaaminisha watanzania kwa CCM hailei wakiuka maadili ya chama na kiuongozi wa nchi. Kushughulikiwa kwa Chenge na Tibaijuka kungekuwa msaada mkubwa kwa chama.

Mpango wa chama unaelekea kubuma. Kukwama hadi kiama. Matendo na maneno ya Chenge na Tibaijuka mbele ya Tume ya Jaji Msumi yanadhihirisha kukwama kwa mpango huo. Ijulikane kuwa CCM ina faili la kila mmoja wao lenye nyaraka zote. Tume ya Jaji Msumi itaishia kutoa mapendekezo ya siri kwa mamlaka za kiserikali juu ya Chenge na Tibajuka ambayo pia si msaada kwa chama.

Bado Ngeleja!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

Kukinusuru CHAMA CHETU CHA MAFISADI,basi japo mnong'onezeni kidogo kidogo kwamba ile SHOMBO ya KATIBA ya FISADI Chenge au Nyoka Mwenye Makengeza,basi aipotezee tu,hiyo ndiyo itakayowagharimu Mzee wangu Tupatupa.Maana kiburi cha jamaa yenu ni sababu ya Katiba isiyokuwa na meno sasa na imagine hii aliyoitengeneza FISADI mwenyewe itakuwaje?
 
CCM bado Tuko imara sana hasa tukimchagua huyu Tanzania itakuwa nchi ya neema maana watoto wetu watakuwa wanavimbiwa kwa kunywa maziwa , mikate na siaji

11009850_792272034188319_6833047830999452455_n.jpg
 
Huu ni mwaka wa uchaguzi mkuu wa Rais,Wabunge na Madiwani. Wakati wa uchaguzi mkuu kama huu,chama kinapaswa kuwa safi na imara kama chuma cha pua. Chama cha Mapinduzi kitaathiriwa vya kutosha na sarakasi za Andrew John Chenge na Anna Kajumulo Tibaijuka juu ya sakata la Escrow. Sarakasi wanazozicheza mbele ya Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma chini ya Jaji Kiongozi Mstaafu,Hamisi Msumi.

CCM iliamua vyema.Ilipokea ubunifu/ushauri toka kitengo cha Itikadi/Propaganda kwamba ni vyema Chenge na Tibaijuka 'washughulikiwe' ili kukisafisha na kukinusuru chama kuelekea Oktoba. Lengo lilikuwa zuri.Ni kuwaaminisha watanzania kwa CCM hailei wakiuka maadili ya chama na kiuongozi wa nchi. Kushughulikiwa kwa Chenge na Tibaijuka kungekuwa msaada mkubwa kwa chama.

Mpango wa chama unaelekea kubuma. Kukwama hadi kiama. Matendo na maneno ya Chenge na Tibaijuka mbele ya Tume ya Jaji Msumi yanadhihirisha kukwama kwa mpango huo. Ijulikane kuwa CCM ina faili la kila mmoja wao lenye nyaraka zote. Tume ya Jaji Msumi itaishia kutoa mapendekezo ya siri kwa mamlaka za kiserikali juu ya Chenge na Tibajuka ambayo pia si msaada kwa chama.

Bado Ngeleja!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
Hiko chama sasa hivi kimekuwa 'kipofu' na 'kiziwi' wa kusikiliza ushauri wa hekima, kama huo ulioutoa mzee Tupa Tupa.

Jaribu kuimagine hao masisiem jinsi walivyokuwa na ujasiri, pamoja na kujua kashfa lukuki alizonazo NYOKA MWENYE MAKENGEZA MSAKA PESA aka Mzee wa vijisenti, bado waliweza kumkabidhi jukumu muhimu kabisa kwenye BMK la kuwa Mwenyekiti wa kamati ya uandishi wa Katiba pendekezwa.

Sasa tumejua kwa nini walimkabidhi jukumu la uandishi wa Katiba mpya, Andrew Chenge, lengo lao kubwa ni kuwafanya watawala wa nchi hii wawe na impunity na kuwa 'untouchables' ya vitume vinavyojiita vya maadili ya uongozi wa Umma.

Kwa hiyo waTz tusidhanii kuwa CCM itaathirika na hizi sarakasi za akina Chenge na mama Tibaijuka, aliyedai shilingi milioni 10 za Escrow, yeye alizitumia kununulia kitoweo cha siku moja tu nyumbani kwakwe!

Kwa kuwa kila 'sarakasi' unayoona inaendelea ya akina Chenge na mama Tiba, zina all the blessings from our highest office of Magogoni TZ!
 
Uliyosema ni kweli mkuu bora wangekaa kimya kuliko hizo sarakasi zao!
 
Back
Top Bottom