VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,004
Huu ni mwaka wa uchaguzi mkuu wa Rais,Wabunge na Madiwani. Wakati wa uchaguzi mkuu kama huu,chama kinapaswa kuwa safi na imara kama chuma cha pua. Chama cha Mapinduzi kitaathiriwa vya kutosha na sarakasi za Andrew John Chenge na Anna Kajumulo Tibaijuka juu ya sakata la Escrow. Sarakasi wanazozicheza mbele ya Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma chini ya Jaji Kiongozi Mstaafu,Hamisi Msumi.
CCM iliamua vyema.Ilipokea ubunifu/ushauri toka kitengo cha Itikadi/Propaganda kwamba ni vyema Chenge na Tibaijuka 'washughulikiwe' ili kukisafisha na kukinusuru chama kuelekea Oktoba. Lengo lilikuwa zuri.Ni kuwaaminisha watanzania kwa CCM hailei wakiuka maadili ya chama na kiuongozi wa nchi. Kushughulikiwa kwa Chenge na Tibaijuka kungekuwa msaada mkubwa kwa chama.
Mpango wa chama unaelekea kubuma. Kukwama hadi kiama. Matendo na maneno ya Chenge na Tibaijuka mbele ya Tume ya Jaji Msumi yanadhihirisha kukwama kwa mpango huo. Ijulikane kuwa CCM ina faili la kila mmoja wao lenye nyaraka zote. Tume ya Jaji Msumi itaishia kutoa mapendekezo ya siri kwa mamlaka za kiserikali juu ya Chenge na Tibajuka ambayo pia si msaada kwa chama.
Bado Ngeleja!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam