Chenge: Mafisadi Wadhibitiwe

Chenge: Mafisadi Wadhibitiwe

apimwe masaburi nadhani ametumia masaburi kuzungumzia hili
 
Tanzania yangu inaongozwa kwa maigizo hii!!!! Mungu tusaidie"
 
mmmh......nilizaliwa katika kipindi cha laaana....jamani the imminent of judjement is on our foot.
 
mpaka chenge amepata jeuri ya kusema hivi, basi tunapaswa kujua kuwa ufisadi hautashuhulikiwa milele hapa tanzania.
 
mhe. Lowassa amekuwa akitamka kwamba Viongozi wa Serikali hadi yule no. 1 na watendaji wakuu wa serikali wameshindwa kuchukua maamuzi magumu badala yake wanalia lia tu! kwa hiyo ndio matokeo yake...ktk kundi la mamba, kenge anaweza akawa jasiri bila hofu kama mamba hawajui wajibu wao au ni waoga!
 
kuna siri nzito juu ya UFISADI wa nchii hii, kwa kauli hii ya chenge basi mafisadi wanajuana.
 
Kama Chenge kasema hilo basi nafikiri sijui ufisadi ni nini.
unajua yale madeal alishindwa kuyakataa maana katiba, ina mpa nguvu nyingi saana Raisi, na yeye akiwa pekee yake asingeweza kuwashinda jamaa kama walivyo fanya watu wa ntwara, lakini sasa akiangalia yale mashimo yaliochiwa ndugu zake huwa analia saana. lol
 
Mhhhhh, ama kweli hakuna mafisadi nchi hii...chenge ni mwalimu wao na anawakanya pia wengine waache kufisadi nchi hii. Gud..katiba mpya itamke mwalimu na mwanafunzi wa fisadi/mhujumu uchumi wote wanyongwe hadharani
 
Kuna watu sasa hivi wapo kama wamenyeshewa na mvua.
Baada ya 2015 tutasikia mengi!
 
Nyani hawezi kuona makalio yake.Asubiri ukombozi waja watatajana!
 
Ufisadi ni msamiati ambao sasa hautenganishwi na siasa za Tanzania. Kwa hiyo mmoja kutaka tafsiri sahihi katika Katiba na mwingine kutaka tume ipewe madaraka kamili kushughulikia nahisi ni mkakati wa kisiasa lakini pia ni ujumbe kwa wapinzani wao. No one will dare to touch them unless he/she is absolutely clean.
 
Ana maana kwamba kama yy anatajwa katika ufisadi na hajachukuliwa hatua ina maana tasisi husika hazina meno na ametaka katiba mpya iwape meno.hajakosea...

Kuna uwezekano ameshajipanga vya kutosha, kisheria. Ngoja aendelee kujidanganya, siku yake itafika tu hata kama ni miaka ishirini ijayo
 
Chenge anataka KATIBA idhibiti MAFISADI, Lowasa anataka KATIBA ieleze maana ya RUSHWA, kazi ipo kwa hiyo Katiba mpya....
 
nchi hii kila mtu yupo against na mafisadi kumbe inawezeka hakuna mafisadi au nchi nzima ni mafisadi.

kwani hata wezi kwenye mahakama si huwa hawakubali kuwa wao ni wezi,je twaweza sema hatuna wezi nchini?.mihimili ya dola yote ina mafisadi.
 
Back
Top Bottom