Chenge: Mafisadi Wadhibitiwe

Chenge: Mafisadi Wadhibitiwe

Filipo Lubua

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2011
Posts
339
Reaction score
579
Ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni

LICHA ya tuhuma mbalimbali za ufisadi ambazo zimekuwa zikimkabili aliyewahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Andrew Chenge, ametaka Katiba mpya iipe meno Tume ya Maadili ili kuwadhibiti wala rushwa.

Chenge ambaye kabla Rais Jakaya Kikwete hajamsafisha, kwa muda mrefu pia alikuwa akitajwa ndani na nje ya chama chake kuhusika na kashfa ya ununuzi wa rada kutoka Kampuni ya BAE- System.

Hiyo ilimfanya awekwe kwenye orodha ya vigogo wanaodaiwa kuficha fedha nje ya nchi.

Licha ya tuhuma hizo zote jana wakati akitoa maoni yake kwenye Tume ya Mabadiliko ya Katiba, alitaka Katiba mpya iipe madaraka Tume ya Maadili ili rushwa iondoke.

Alisema tume hiyo lazima ipewe meno na kufanya kazi kwa uchunguzi bila kuingiliwa wala kuwa na woga wa mtu au kiongozi yeyote ili kutoa weledi kwa taifa.

Mchakato wa ununuzi wa rada, ambao uliwahusisha watu wa madaraka na kada mbalimbali akiwamo aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza, Tony Blair, ulimuacha Chenge kwenye tuhuma nzito za rushwa.

Kuhusika kwa Chenge kulitokana na nafasi ya uanasheria mkuu wa serikali aliyokuwa akiishikilia, hivyo kutajwa kuwa kiungo muhimu aliyefanikisha ununuzi wa rada hiyo kwa gharama kubwa kupita kiasi ya shilingi bil. 40.

Chanzo: Tanzania Daima, Jumapili 27 Jan. 2013
 
CCM (Panya) wanajiuliza, nani atamfungia Paka Kengele Kwanza?....lol Hii Kali
Chenge has the guts and moral authority to question or even make comments on Corruption. Honestly, Nchi hii haina Kiongozi. Tunaye Fastjet/Mtalii au some lunatic at Magogoni. this is an insult to our senses
 
Hapana mkuu. Chenge kafungua njia ya kumuhukumu Jakaya. Anataka ashitakiwe kunyongwa then aseme ni Jakaya ndiye aliyemtuma kuiba, hivyo kosa si lake bali ni la raisi. Kwa kifupi, anataka Jakaya anyongwe!
 
"Ikulu ni mzigo mzito......kuna biashara gani ikulu?"
 
Hapana mkuu. Chenge kafungua njia ya kumuhukumu Jakaya. Anataka ashitakiwe kunyongwa then aseme ni Jakaya ndiye aliyemtuma kuiba, hivyo kosa si lake bali ni la raisi. Kwa kifupi, anataka Jakaya anyongwe!

Basi watajane ili wanyongwe.... Who cares if they all get hanged.
 
Sina shaka na kauli yake naamini anawajua na wapo, yeye alipiga dili la 1Mil Usd. Lakini kuna watu wana 300Mil Usd peke yao huko Uswiss unategemea nini?
 
Nchi hii kila mtu yupo against na mafisadi kumbe inawezeka hakuna mafisadi au nchi nzima ni mafisadi.

Ana maana kwenye kundi la MASHETANI yapo Mashetani ambayo ni bora zaidi ambayo kati yao ni yeye na EL ambao wote wamelizungumza hilo la MAFISADI liingizwe kwwenye Katiba. Huko ni kuweweseka
 
chenge alishatamka kuwa Mwenye ushahidi juu ya ufisadi wa chenge apeleke mahakamani, mbona twalalama tuu mitandaoni?
 
chenge alishatamka kuwa Mwenye ushahidi juu ya ufisadi wa chenge apeleke mahakamani, mbona twalalama tuu mitandaoni?

Ushahidi gani tena zaidi ya ule uliotolewa na serikali ya Uingereza? Nani ampeleke mahakamani zaidi ya Takukuru? Edward Hossea na wafanyakazi wake wote Tanzania nzima, tunawalipa ili wawashughulikie watu kama Chenge, sasa nani tena mwingine ampeleke Chenge mahakamani zaidi yao?
 
Mwenzake aliibuka na Maoni kwenye katiba mpya eti watoe defination ya Fisadi na ufisadi Tanzania home of Maigizo
 
Sina shaka na kauli yake naamini anawajua na wapo, yeye alipiga dili la 1Mil Usd. Lakini kuna watu wana 300Mil Usd peke yao huko Uswiss unategemea nini?
Ndio maana akatuambia kua hizo zake ni "vijisenti" tu, aki-relate na hizo $300mil za wenzie
 
Back
Top Bottom