mukizahp2
JF-Expert Member
- Jul 28, 2012
- 705
- 378
SPIKA wa Bunge, Anne Makinda, anaweza kukutana na hoja ya kupigiwa kura ya kutokuwa na imani bungeni na hatimaye kung'olewa kama sehemu ya wabunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wataunganisha nguvu na wabunge wa Upinzani, hususan wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Raia Mwema limeelezwa.
Tayari namna ya kuendesha mpango huo imekwishaafikiwa kati ya wabunge. Hoja zinazodaiwa kuweza kutumika, kwa mujibu wa vyanzo vya habari vya gazeti hili, ni pamoja na Spika Makinda kudaiwa kutumia mabadiliko ya kanuni za Bunge bila idhini ya Bunge.
"Spika ameunda kamati hizi za Bunge na uamuzi huu aliutangaza bungeni, lakini kuna kasoro nyingine ya hivi karibuni. Amemteua Andrew Chenge kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti ya Bunge kwa kutumia mabadiliko ya kanuni ambayo hayajaidhinishwa na Bunge, haya ni makosa," anaeleza mmoja wa wabunge walioko tayari kumpigia kura ya kutokuwa na imani Spika Makinda.
Mbunge huyo (jina linahifadhiwa) anafafanua ya kwamba mabadiliko ya Spika kupewa uamuzi wa kuteua mwenyekiti wa kamati badala ya mfumo rasmi wa wenyeviti wa kamati kuchaguliwa ni jambo jipya na ni uamuzi mkubwa ambao unapaswa kuhusisha mabadiliko kamili ya kanuni yanayopaswa kuidhinishwa na Bunge, kabla ya kutumika.
Inadaiwa ya kwamba, Spika alifuata na kuheshimu taratibu za awali za kufanikisha mabadiliko hayo ya kanuni, kwa mfano, kuhakikisha mabadiliko hayo yanapitia katika kamati ya kanuni za Bunge lakini hoja inajengwa kwamba hatua ya mwisho aliyopaswa kuipitia ni kuhakikisha mabadiliko hayo ya kanuni yanaidhinishwa na Bunge na si kamati ya kanuni pekee.
Lakini wakati harakati hizo zikiendelea, tayari Raia Mwema limethibitishiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa wa Bunge, Jossey Mwakasyuka kwamba, Spika hakucheza rafu zozote na hiyo haiwezi kuwa sababu ya kumng'oa.
"Alichokifanya Spika ni kwa mujibu wa kanuni ya 152 ya kanuni za Bunge, inayompa mamlaka ya kufanya mabadiliko na kanuni hiyo ya 152 fasili ya tatu inaeleza, Spika kwa kushauriana na Kamati ya Kanuni za Bunge, atakuwa na madaraka ya kuzifanyia marekebisho au mabadiliko ya nyongeza kanuni hizi, kulingana na mahitaji ya wakati, kadiri atakavyoona inafaa," alisema Mwakasyuka katika mazungumzo yake kwa njia ya simu na mwandishi wetu.
Lakini wakati ufafanuzi kwa upande wa Bunge ukiwa hivyo, mbunge mwingine aliyeko kwenye harakati kuhakikisha Spika Makinda anaadhibiwa anasema; "Ni sawa kutumia kamati ya kanuni za Bunge lakini, kanuni ya 153, fasili ya kwanza inasema mabadiliko yaliyopitishwa hayataanza kutumika mpaka yatakapochapishwa na kuingizwa katika toleo la kanuni za Bunge litakalofuata. Kwa hiyo kuna makosa hapa, uamuzi wa Spika kujipa mamlaka ya kuteua mwenyekiti wa kamati mojawapo wakati wenyeviti wengine wanachaguliwa ni uamuzi unaogusa mabadiliko ya kanuni yanayopaswa kuzingatia taratibu zote."
Lakini Mwakasyuka anazungumzia hilo akisema; "Kilichopo ni kwamba, Spika amefanya mabadiliko katika nyongeza ya mabadiliko ya Kanuni za Bunge. Tayari kulikuwa na nyongeza ya mabadiliko ya kanuni ambayo yalifanyika kupitia Kamati ya Kanuni za Bunge, na hayo ni sehemu ya majukumu yake...hayahitaji moja kwa moja kupitishwa na Bunge, yaani Kamati ya Kanuni inafanya kazi hiyo kwa niaba ya Bunge."
Vyanzo vingine vya habari vinaeleza ya kwamba, hatari ya Spika kung'olewa bado ni kubwa si tu kutokana na rafu anazodaiwa kufanya katika kujipatia mamlaka ya kuteua mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti, bali pia ni kutokana na baadhi ya wabunge kuamini ya kwamba haongozi vema Bunge.
Tayari kumetokea mzozo kati ya uongozi wa Bunge na Kambi ya Upinzani Bungeni kuhusu mwenendo wa Bunge chini ya Spika, ambaye naye, hata hivyo anaamini hadhi ya Bunge inashushwa na mwenendo mbovu wa baadhi ya wabunge, huku Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu akitajwa kuwa mfano wa vinara wa ‘vurugu' bungeni.
Kupungua kwa imani dhidi ya Spika Makinda miongoni mwa wabunge kunatajwa kuchangiwa zaidi na uamuzi wake huo wa ‘kujipa' mamlaka ya kumteua mwenyekiti wa kamati ya bajeti na kisha, moja kwa moja kumteua Andrew Chenge.
Mbunge mmoja alimweleza mwandishi wetu: "...ukiondoa hili suala la mabadiliko ya kanuni kufanyika na kutekelezwa bila kwanza kuidhinishwa na Bunge ndipo yaanze kutumika, jambo baya zaidi kwangu amemteua Chenge kuwa Mwenyekiti wa hii kamati na anasema amemteua kwa sababu eti ana high intergrity (ni mwadilifu). Hatuwezi kukubali kwa sababu hizo nchi wafadhili ndio wenye rekodi ya Chenge, kwa mfano katika suala la rada hadi chenji imerudishwa nchini.
" Uingereza ni mchangiaji mkubwa wa Bajeti ya Tanzania, leo hii Bunge linampa uongozi wa Kamati ya Bajeti mtu ambaye wanajua alikuwa na nafasi kubwa ya kushauri ili nchi isinunue rada kwa bei kubwa, kazi ambayo ilifanywa kwa niaba yake bila mafanikio ya Waziri wa Uingereza Clare Short.
"Nadhani Tanzania ndiyo nchi ya kwanza au ya pili katika kupewa msaada mnono wa bajeti yake na Uingereza, leo hii unawaeleza Chenge huyo huyo aliyesimama katikati ya sakata la rada, ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, hii ni dosari. Kwa hiyo, kwanza uteuzi wake umefanyika kupitia kanuni ambazo hazijaidhinishwa na Bunge lakini pili, Bunge linajitia aibu mbele ya wananchi na Jumuiya ya Kimataifa," alisema mbunge huyo (jina linahifadhiwa).
Hata hivyo, kwa upande mwingine, mwandishi ameelezwa na baadhi ya wabunge wanaomuunga mkono Spika kwamba; "hata kama Chenge akiachwa agombee uenyekiti kwa kupigiwa kura atashinda tena nafasi hiyo."
Chenge mwenyewe hakuweza kupatikana kuzungumzia uteuzi wake huo lakini gazeti hili liliwahi kuripoti ya kuwa, Spika aliwahi kuunda kamati ya siri iliyopaswa kumshauri kuhusu namna bora ya kufuatilia bajeti ya serikali na katika kamati hiyo, Chenge ndiye aliyekuwa mwenyekiti, baadhi ya wajumbe waliokuwa naye ni pamoja na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Freeman Mbowe, Mbunge wa kuteuliwa na Rais, James Mbatia na Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed.
Source: RAIA MWEMA