Chenge kufuru tupu, amiliki bilioni 25 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chenge kufuru tupu, amiliki bilioni 25

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Venant Ben, Jan 14, 2011.

 1. Venant Ben

  Venant Ben Senior Member

  #1
  Jan 14, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 155
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Aliyekuwa WAZIRI wa Miundombinu, Andrew Chenge anaogelea katika utajiri wa zaidi ya Sh. 25 bilioni zenye utata huku Rais Jakaya Kikwete akiendelea kumkumbatia, MwanaHALISI limegundua.Chenge amekuwa mfanyakazi serikalini kwa karibu miaka 30 na hafahamiki kuwa mfanyabiashara.

  Kiwango kinachotajwa ni pamoja na fedha zilizogunduliwa na makachero wa Uingereza katika akaunti zake za nchi za nje. Fedha zilizoko kwenye akaunti yake ya nchini, Na. 011101006950 katika benki ya NBC Limited, ni Sh. 25,794,805.89 za Tanzania hadi Ijumaa iliyopita, tarehe 11 Aprili 2008.

  Katika akaunti yake ya Uswisi, ambako ana akaunti ya fedha za kigeni, Chenge amehamishia dola za Marekani 467,000, sawa na zaidi ya nusu bilioni kwa fedha za Tanzania.Fedha za Uswisi zimelimbikizwa katika akaunti Na. 030105000364. Zilihamishwa kutoka akaunti Na. 011105011782 ya kampuni ya TANGOLD Limited, tangu 22 Februari 2006 kupitia NBC Limited.

  Taarifa za kuaminika ambazo MwanaHALISI imezipata zinasema Chenge ni Mkurugenzi wa kampuni ya TANGOLD Limited ambayo ina dola 12,997,950.84 sawa na Sh. 15 bilioni za Tanzania katika NBC Limited tawi la Makao Makuu. Aidha, kampuni hiyo inahifadhi Sh. 1,379, 359,367.39 katika akaunti Na. 011103024852 tawi hilohilo la NBC Limited.

  Habari tulizopata wakati tukienda mitamboni, zinasema kwamba makachero wa Uingereza wanafuatilia uhalali wa Euro 3 milioni (sawa na zaidi ya Sh. 8 bilioni za Tanzania) zinazodaiwa kuwa Chenge alizipeleka kwenye akaunti zake nje ya nchi.Taarifa nyingine ambazo hatukuweza kuzithibitisha haraka, zinasema Chenge alihamisha kwa mkupuo dola 600,000 za Marekani kwenda kwenye akaunti ya ofisa mwandamizi mmoja aliyekuwa Benki Kuu miaka kadhaa iliyopita, na ambaye kwa sasa anaongoza shirika la umma nchini.

  TANGOLD ni kampuni ambayo inadaiwa kumilikiwa na serikali kwa asilimia 100 na ambayo inadaiwa pia kuwa ndiyo imerithi mali na madeni ya kampuni ya Meremeta Limited iliyokuwa ikijihusisha na uchimbaji madini, Buhemba, mkoani Mara.Hata hivyo, kuna utata juu ya lini kampuni hiyo ilianzishwa nchini. Wakati aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini Nazir Karamagi aliuambia Mkutano wa Tisa wa Bunge kuwa TANGOLD iliundwa mwaka 2006 kupitia Task Force maalum ya serikali, kumbukumbu zinaonyesha kuwa kampuni ilianzishwa mapema 2000 au kabla.

  Hiyo inathibitishwa na ukweli kwamba tarehe 1 Januari 2000 walikuwa na akaunti ambayo haikuwa hata na senti moja katika akaunti zake mbili hadi 29 Desemba 2005 zilipoingizwa dola 13,340,168.37.Fedha hizo zilikuwa zinatoka Hazina kupitia Benki Kuu (BoT).

  Kwa akaunti ya fedha za Tanzania, tarehe 1 Agosti 2005, TANGOLD Limited ilichota kutoka Hazina kupitia BoT, Sh. 4,703,221,229.08 kwa hundi Na. 241741 na kufanyiwa uhamisho wa haraka (special clearance).Chenge, akiwa mkurugenzi, anahusika na uhamishaji, ulimbikizaji na ulipaji wa fedha kutoka akaunti za TANGOLD.

  Wakurugenzi na waidhinishaji malipo wengine wa kampuni hiyo ni, Daudi Ballali, Gray Mgonja, Vincent Mrisho na Patrick Rutabanzibwa.Ballali alikuwa gavana wa BoT, Mgonja akiwa Katibu Mkuu Hazina, Mrisho akiwa Ofisi ya Waziri Mkuu na Rutabanzibwa akiwa Katibu Mkuu Maji na Umwagiliaji.Matumizi ya fedha kutoka akaunti hizi ambako kuna mkono wa Chenge ndiyo yanaongeza utata.

  Kutoka kwenye akaunti ya binafsi ya Chenge, mamilioni ya shilingi yamelipwa kwa watu mbalimbali wakiwa ni pamoja na Janet Mashale, Mary Nchimbi, Mary Chitanda na Livingstone Ruhere.Wengine ni Getrude Mtiga, Hawa Kiama, Leocardia Kalumuna, Athumani Sheha na David Sanga.

  Miongoni mwa waliolipwa ni viongozi wa CCM, waandishi wa habari na wengine ambao hawakuweza kutambulika. Muhimu ni kwamba karibu fedha hizo zote zililipwa wakati uchaguzi wa CCM mwaka jana ambapo Chenge aliwania ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC). Alishinda kwa kura nyingi. Akaunti ya TANGOLD inaonyesha kutoingiza kiasi chochote cha fedha kwa miaka mitano, kati ya Januari 2000 na Desemba 2005.
  Source : Mwanahalisi
   

  Attached Files:

 2. Monstgala

  Monstgala JF-Expert Member

  #2
  Jan 14, 2011
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 1,082
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Wow!!!! Then 1 billion from radar issue was definitely kijisenti for this guy!
   
 3. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #3
  Jan 15, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mmmmhhhh!!!!!!!!!!!!!
   
 4. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #4
  Jan 15, 2011
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  "Kutoka kwenye akaunti ya binafsi ya Chenge, mamilioni ya shilingi yamelipwa kwa watu mbalimbali wakiwa ni pamoja na Janet Mashale, Mary Nchimbi, MARY CHITANDA na Livingstone Ruhere.Wengine ni Getrude Mtiga, Hawa Kiama, Leocardia Kalumuna, Athumani Sheha na David Sanga."

  Wakuu, ktk nukuu hapo juu, naomba kuhighlight majina haya hususan jina la Mary Chitanda... nawasilisha
   
 5. shanature

  shanature JF-Expert Member

  #5
  Jan 15, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 718
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  mh atadaai ni urithi wa ng'ombe kule bariadi
   
 6. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #6
  Jan 15, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  kuna kuna viwanda sola-maswa, rugulu-bariadi na marampaka vya kuchambua pamba kuna mtu kani dokeza kuwa ni za kwake na kikwete pamoja na shule moja kubwa sana yenye chekechea mpaka kidato cha 6 inayojulikana kwa savvanah spring..kwalio huko mnaweza kutujuza zaidi juu ya ukweli huu
   
 7. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #7
  Jan 15, 2011
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  vijisent tu ivyo
   
 8. Not_Yet_Uhuru

  Not_Yet_Uhuru JF-Expert Member

  #8
  Jan 15, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hiyo ndiye Chenge, vijisent vingine hivyo.

  ndio maana hata akiua kwa magari yake, wahanga wanadharaulika kama kuku, serikali ni mali yake. Ukizingatia kampuni ya TANGOLD inamilikiwa na serikali ka 100%, na mkurugenzi ni yeye pekee, then tuna kazi kubwa kwa future ya JK na ukizingatia mwenye uamuzi wa mwisho ni Rostam, je nani atamuwajibisha nani?
   
 9. HeartBreak

  HeartBreak JF-Expert Member

  #9
  Jan 15, 2011
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 346
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  nchi hii...amefulia sana.....hakuna kiongozi wa ccm aliyenauchungu na watanzania kama yuko lazima atapigwa chini faster!!!!
   
 10. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #10
  Jan 15, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,134
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Halafu JK mpaka leo hajui kwanini watanzania ni maskini wa kutupwa mpaka leo TOBAA!
   
 11. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #11
  Jan 15, 2011
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  mkuu habari hii ni ya siku nyingi sana kwenye gazeti la mwanahalisi na imeshaletwa hapa jamvini nadhani ni punde tu baada ya kujiuzulu au siku chache baada ya kutajwa kwenye sakata la rada.
   
 12. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #12
  Jan 15, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Akiamua kutoa pesa zake zote Bank hakika bank zinaweza filisika duh
   
 13. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #13
  Jan 15, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Hili waziri mkuu pinda alishawahi kusema mafisadi yananguvu yana weza kuitetemesha nchi kiuchumi..
   
 14. musmyl

  musmyl Member

  #14
  Jan 15, 2011
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 38
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  :coffee:C.c.m -chukua chako mapema sasa yeye ameshachukua jamani tatizo liko wapi na wewe ingia ubebe chako
  mapinduzi daima:coffee:
   
 15. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #15
  Jan 15, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  sijui unatania, sijui ndiyo uwezo wako wa kufikiri....
   
Loading...