Chenge: Jeuri yake ni kaburi la CCM

Tatizo liko hapo. Waafrika hatuna utamaduni huo wa kuachia. Kumbuka wakati unashutumu kuna watu wnanamsifu; yeye anachagua asikilize lipi Na mara nyingi anachagua linalompendeza. Ingekuwa hivyo unavyosema Museveni, Mugabe wangeshaachia. Nyoka wa makengeza ni msemo maarufu huko kwao usukumani - chonji - yeye anatafuta fursa na kuvitumia effectively. Wakati wote tusisahau pia kuwa tuko kwenye mfumo tofauti na wa ujamaa tuliokuwa nao! Ni mfumo wa kutafuta fursa na kujilimbikizia mali na wala hii si dhambi.
 

Very contradictory
Please try again & make your argument clear!
 
Mtoa mada au ndg msanii. Mada yako ni nzuri sana ila naomba nikukosoe sehemu moja kuwa ujambazi wa Chenge ni kaburi la CCM . Siyo kweli Bali chama hiki ndo kinajichimbia hilo kaburi. Ndo utendaji wake unalea ujambazi ndani ya chama . Ujambambazi huu ni ngumu kuutenganisha na chama .kwani kina manyangumi wanaonyonya watanzania wangapi na bado wanadunda ndani ya chama??? Wana wafuasi lukuki ndani ya chama? Jambazi Chenge si peke Yake anaenuka ujambazi ndani ya hilo li chama . Leo ni ngumu kutafuta mtu ndani ya chama asiyeguswa na ujambazi. Chenge analaumuwa tu kwa kuwa ni jambazi Sugu ndani ya chama ila ma jambazi ni mengi sana na yanareflect chama hivyo chama ndo kinajichimbia kaburi chenyewe. Ni dhahri kuwa chama kimekuwa na nafasi kubwa mno ya kutubu na kubatizwa tena kwa maji mengi ila usugu umekuwa muthiri ya vile vidole vinavyikataa mashine ya mpiga kura .
 
Tatizo mnasukumwa na hisia kuliko ukweli na sheria. Je umeshajiuliza ikiwa kweli ni mchafu kiasi hicho mbona hajafukuzwa katika Chama na pia hajafikishwa mahakamani?

Chama chenyewe kichafu nani sasa amfukuze? Chama ndo kina mtegemea kwenye dili sasa nani atamfunga paka kengele?
 
Mkuu
Nashukuru kwa kudadavua vyema mada yangu, lakini ninasimama katika msimamo niliouweka hapo juu kwa sababu zifuatazo.
1. Pamoja na kuwepo kwa majambazi ya mali za umma ndani ya CCM na ieleweke wapo katika upinzani pia. Lakini mtu kama Chenge amemulikwa waziwazi kuwa ndiye kubwa la majizi hayo kwa kuwa uhuni wake anaufanya wazi na hakuna wa kumgusa wala kumkemea. Inawezekana ukawa unawafahamu wengine ila aliyejipambanua hata kwa tambo zake ni huyu chifu.
2. Kama Chama kingemshughulikia bila kusubiri Bunge kutoa mapendekezo yake, heshima ingejengeka kuwa at least CCM inarudi kwenye misingi yake. Ila kwa kuwa kimekuwa kinasubiri mtu ahusishwe na ubadhirifu ndipo kijisuesue kushughulika naye hivyo kinajipeleka kwenye kitanzi kwa hiyari yake
3.Chenge halaumiwi bali anatuhumiwa na ieleweke kwamba vyombo muhimu vya serikali vimethibitisha kwamba si msafi, hata majizi wanaojiita wafadhili wamemtaja kwamba ni mkwapuaji hasa kupitia lile deal la RADAR.

I rest my case
 
Sawa Mkuu ila ieleweke tu Kuwa katika mji wa vipofu mwenye Chongo ni mfalme. Tunahitaji kuuchukia ujambazi bila kujali dhambi imekuwa nyekundu kiasi gani.
 
jeuri ya chama -yeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeba
 
Someni in between the lines sakata hili la Hon Chenge, mimi naona huyu bwana ataondolewa katika Chama kuonesha ukomavu.Na kama CCM ikishika madaraka tena atasamehewa na kurudi kundini na kumfanya MBUNGE wa Bariadi amuachie kiti.
 
Sijui kwanini hajafa mpaka now. ..aliua watu kwa ajali akachoropoka ....siku akifa itakua ni sherehe kubwa
 
Chenge ndiye mtunzi wa katiba ya mwaka 1977 na ni mwandishi wa katiba inyopendekezwa. Katiba ni msingi wa nchi hivyo watu kama hawa lazima wajenge msingi unao favour mafisadi na si taifa kwa ujumla. Movie inaendelea. ..watanzania amkeni
 
Sisi wananchi ni sungura wajanja wasio na makengeza, hatutaki nyoka, tutakutana na mwenye nyoka/ chama cha wafuga manyoka October 2015

Ni zamu yako!! Amka kajiandikishe kupiga kura
 
Umeshahau

Na ni chenge aliyetunga katiba iliyoondoa maadili kama tunu ya taifa

Katiba hiyo inaitwa "Katiba bora" na MaCCM

Sasa hebu fikiri zaidi hapo

Hayo ndio maajabu ya dunia!!Kwa aina ya Watanzania sisi chenge anakuwa Mbunge awamu ijayo na hasirani hatapelekwa mahakamani nafikiri kunahaja ya wao wananchi kichukua hatua bila kusubiri serikali inayoshangilia wizi wake!
 
Hebu tuanze na sakata la rada (BAE) ambapo vyombo vya uchunguzi vya Uingereza vimemhusisha na rushwa aliyopokea na kuificha kwenye offshore account....
Naomba unitoe tongotongo kuhusu usafi wake hapo ili tusonge mbele na tuhuma zingine


Bora umeuliza kwa ustaarabu na huyu nyoka mtoto asiyejua ujambazi wa baba nyoka ajibu kny ya babake . Akimaliza ya BAE, tutampa dozi nyingine tusonge mbele maana orodha ni ndefu.
 
Bora umeuliza kwa ustaarabu na huyu nyoka mtoto asiyejua ujambazi wa baba nyoka ajibu kny ya babake . Akimaliza ya BAE, tutampa dozi nyingine tusonge mbele maana orodha ni ndefu.
Amekimbia.
Kutetea uozo inahitaji uwe jasiri kama uozo wenyewe ndani na nje ya ngozi.

Kinachonisikitisha ni kuwa Wana wa uovu hawaendi likizo na kila siku wanakuja na mbinu mpya ya kufanya uovu zaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…