Chenge: Jeuri yake ni kaburi la CCM

Chenge: Jeuri yake ni kaburi la CCM

Tatizo mnasukumwa na hisia kuliko ukweli na sheria. Je umeshajiuliza ikiwa kweli ni mchafu kiasi hicho mbona hajafukuzwa katika Chama na pia hajafikishwa mahakamani?
we unaota mchana kweupe! Nani mwenye ubavu kumkamata na kumshitaki chenge? Unakumbuka hata sakata la vua gamba?
 
He is slwowly becoming a hero and a model to many.
Kitaa kumezuka kamsemo "Nina jeuri ka Chenge"
 
Hawa CCM hawasomi historia?

Yule malkia wa Ufaransa aliyedhihaki watu wasio na uwezo wa kununua mikate wanunue keki, kilimkuta kitu gani?

SMH
 
Hahahaha. Joka lenye makengeza hi nchi hii iahajifia tangu lini mzaramo akawa raisi
 
Tangu mzaramo alipochukua madaraka nilijua kuwa ndo mwisho wa hii nchi iliyo jaa mijitu mijinga na mizembe
 
kama ndani ya ccm hakuna wa kumkemea Chenge utawezaje kumpata kiongozi bora? ndio maana sisi kina gogo la shamba tunasema kwa sasa ndani ya ccm uwezi kumpata kiongozi bora<br><div style="display:none;" id="__if72ru4sdfsdfrkjahiuyi_once"></div><div style="display:none;" id="__if72ru4sdfsdfruh7fewui_once"></div><div style="display:none;" id="__hggasdgjhsagd_once"></div>
 
View attachment 230264
Chenge ana jeuri kwa sababu anajua ccm hawawezi kumfanya lolote kama waliweza kumpa madaraka ya kuandika katiba wakati wakijua ni mchafu unategemea nini hapo kwenye tume ya maadili kuna mchezo unachezwa hili asihojiwe kwa sababu anajua ana makosa makubwa hujaona mwenzake Tibaijuka jana anaongea kama amechanyingikiwa eti millioni 10 ni pesa ya kununua mboga .
 
Halafu eti, mkuu wanchi anaisifia nakuikubali katiba yamtu mchs na mbinasfsi kiihivyo. Hivi unakulaje namtumchafu mikono...
 
Hakuna mwenye uwezo wa kumwajibisha chenge serikalini wala kwenye chama kamwe! Katiba pendekezwa imetungwa na kuandikwa na fisadi chenge, ndiyo katiba ambayo jk anasema ni katiba bora afrika. Ndani ya ccm wote wameoza, kilichobaki ni kugawana vyeo kama njugu tu. Period!

Pamoja na ufisadi wake bado anaonekana mwenye akili nyingi kuliko watendaji wote wa serikali pamoja na bunge.Tukumbuke wabunge walishndwa kuframe maazimio kuwa kwenye mpangilio unaoleta mant&#305;ki,n CHENGE aliyeibuka na modelity iliyoungwa mkono na wabunge hata wapinzani.Wakat&#305; wa BMK chenge alikuwa mwenyek&#305;ti wa kamati ya uandishi, alibishana na Asha Rose kuhusu swala la Rais wa Zanzibar kuwa makamu wa Kwanza wa Ra&#305;s, Chenge alikataa na akajenga hoja ikaungwa mkono na wajumbe wote kuwa wakifanya hvyo na baadaye CUF wakashnda Urais Zanzibar maana yake akifa Rais wa Muungano ambaye atakuwa CCM, CUF wanakaimu Ura&#305;s.Hakuna aliyekuwa ameona hlo.Walibishana hadi ngita z&#305;kawatoka lakn Chenge akasema Ng'o na kama hamtaki najiondoa nyie endelea.Rose hakuwa ameona hilo na udaktari wake,anatafuta kuwar&#305;dhsha Wazanzbar.Iweje Rais aliyechaguliwa na watu laki2 awe wa JMT?Chenge genius na wale jamaa wa maadili anawaona vihio tu ndo mana hataki hata wamuhoji.
 
sasa nyinyi vikoroboi mtu akituhumiwa haruhusiwi kujitetea akubali eti sababu mbunge wa ccm
 
Na hii katiba inayopendekezwa ipigiwe kura na haohao viongozi waliopo madarakan wanawashawishi wananchi waikubali ametunga huyo huyo Mwiz CHENGE hv kwel hii CCM inawatakia mema wananchi, na huyu bwana mkubwa mzigo tu.
 
Nimefurahishwa sana na jamaa wa Maadili(au madili?) kumchokoza Mbunge wa Bariadi Magharibi Andrew Chenge kuhusu mambo ya IPTL/ESCROW.Na nimefurahishwa sana na mgomo wake,kukubali tu kuonewa onewa si jambo zuri,na Chenge anajitambua.

Kama kweli watu wa maadili wanao ubavu wa kushughulika na ishu za mkataba wa IPTL na kashfa zilizofuatia za kupiga km vile ishu ya ESCROW,basi wamwite na Kikwete maana ndo Waziri hasa wa IPTL,na Rugemalira ni mtu aliyetoa fedha ya kutosha tu kumsaidia Kikwete kuupata Urais wa JMT mwaka 2005.Kwanini Kikwete anafichwafichwa?

Namwunga mkono Mtemi Chenge asilegeze kamba,aweke ngumu tu hadi kieleweke!
 
Yote yaliandikwa, lakini kiukweli ni kuwa yalibaki hisia tu. Kungekuwa na uthibitisho wa kumhusisha yeye na sakata hilo kijinai angepelekwa mahakamani. Kuwa na Account nje na pesa hizo siyo kosa kwa mujibu wa sheria zetu mpaka sasa ikiwa tu unaweza kuelezea zimepatikanaje. Nina hakika Mh alieleza kwa ufasaha alizipataje na zikaonekana ni za halali ndiyo maana hakupelekwa kwa Pilato.

Ni mtizamo tu wa Watanzania maskini, lakini kwa kiongozi makini tuhuma zikizidi anaachia ngazi, hachezi na mapungufu yaliyomo kwenye sheria ambazo kwa kiasi kikubwa alishiriki kuziasisi. Wala hang'ang'anii utolewe ushahidi, anaacha nafazi yake na kukaa pembeni. Ile tu kiongozi kujiita nyoka mwenye makengeza ni ukosefu wa maadili mema, nyoka mwenye makengeza maana yake ni nini. Haiingii akilini kwa kiongozi kuhusishwa katika kashfa zote kubwa na yeye akaona anaonewa. Lakini naamini safari hii watu jinsi hiyo hakika wataigharimu CCM.
 
Kama mtu ni msafi kwanini uogope kuhojiwa?hapo ndio anatia shaka uadilifu wake,angekuwa msafi wala usingekimbilia kuweka zuio,huyu ni sawa na mwenye makosa anavyoogopa hata kupita kituo cha polisi ,ni sawa na mhalifu anapomuona askari hukimbia au huanza kujitetea hata kabla polisi hajafungua kinywa chake.Ukiwa mwizi hata ukisikia sauti za mwizi mwizi nawe huanza kukimbia au kusema au mimi sio mwizi bila hata ya kuulizwa.Ni aibu kwa watu wa Bariadi kuwa na mbunge kama Chenge halafu anawadanganya kwa kuwapa fedha za wizi nao kwa ujinga wao wanapokea na kumpigia makofi,anayeshiriki kupokea vitu vya wizi naye ni mwizi au anayepokea rushwa naye ni mla rushwa,huwezi mbunge na msomikama Chenge kujifanya eti kutoa hivyo vijisenti eti ndio kuwaletea maendeleo watu wake wa Bariadi,hawa wezi wakiiba hukimbilia majimboni mwao na kutoa hizo hela za wizi eti huko ndio kuwaletea maendeleo watu wao,akina Prof Tibaijuka nao walifanya vivyo hivyo,walipotimuliwa wakakimbilia majimboni mwao eti kuwaletea maendeleo wananchi wao.Ndugu zangu maendeleo hayaletwi na mbunge au mtu moja mmoja maendeleo huletwa na wananchi wenyewe,tuache ujinga,hayo maendeleo ndio wanayaona leo karibu na uchaguzi,watu wa Bariadi mungemuuliza Chenge hizo hela kazipata wapi na kwa biashara gani anayoifanya?mlivyofanya ni sawa na mzazi anayepokea fedha au msaada kutoka kwa mtoto wake wakati akijua mtoto wake hana kazi yoyote ya kuleta mabilioni hapo nyumbani.
 
Back
Top Bottom