Asante matusi ya ni ninI wakati mimi sijakutukana?Uwe unafikiri kwa kutumia kichwa achana na makalio!
Asante matusi ya ni ninI wakati mimi sijakutukana?Uwe unafikiri kwa kutumia kichwa achana na makalio!
Tatizo liko hapo. Waafrika hatuna utamaduni huo wa kuachia. Kumbuka wakati unashutumu kuna watu wnanamsifu; yeye anachagua asikilize lipi Na mara nyingi anachagua linalompendeza. Ingekuwa hivyo unavyosema Museveni, Mugabe wangeshaachia. Nyoka wa makengeza ni msemo maarufu huko kwao usukumani - chonji - yeye anatafuta fursa na kuvitumia effectively. Wakati wote tusisahau pia kuwa tuko kwenye mfumo tofauti na wa ujamaa tuliokuwa nao! Ni mfumo wa kutafuta fursa na kujilimbikizia mali na wala hii si dhambi.Ni mtizamo tu wa Watanzania maskini, lakini kwa kiongozi makini tuhuma zikizidi anaachia ngazi, hachezi na mapungufu yaliyomo kwenye sheria ambazo kwa kiasi kikubwa alishiriki kuziasisi. Wala hang'ang'anii utolewe ushahidi, anaacha nafazi yake na kukaa pembeni. Ile tu kiongozi kujiita nyoka mwenye makengeza ni ukosefu wa maadili mema, nyoka mwenye makengeza maana yake ni nini. Haiingii akilini kwa kiongozi kuhusishwa katika kashfa zote kubwa na yeye akaona anaonewa. Lakini naamini safari hii watu jinsi hiyo hakika wataigharimu CCM.
Tatizo liko hapo. Waafrika hatuna utamaduni huo wa kuachia. Kumbuka wakati unashutumu kuna watu wnanamsifu; yeye anachagua asikilize lipi Na mara nyingi anachagua linalompendeza. Ingekuwa hivyo unavyosema Museveni, Mugabe wangeshaachia. Nyoka wa makengeza ni msemo maarufu huko kwao usukumani - chonji - yeye anatafuta fursa na kuvitumia effectively. Wakati wote tusisahau pia kuwa tuko kwenye mfumo tofauti na wa ujamaa tuliokuwa nao! Ni mfumo wa kutafuta fursa na kujilimbikizia mali na wala hii si dhambi.
Asante matusi ya ni ninI wakati mimi sijakutukana?
Then you should not insult someone because s/he has written what in your opinion is shit. a civilised person will respect other people's opinion not insult.The reason is: YOU Are writing SHIT
Use your brains!!
Mtoa mada au ndg msanii. Mada yako ni nzuri sana ila naomba nikukosoe sehemu moja kuwa ujambazi wa Chenge ni kaburi la CCM . Siyo kweli Bali chama hiki ndo kinajichimbia hilo kaburi. Ndo utendaji wake unalea ujambazi ndani ya chama . Ujambambazi huu ni ngumu kuutenganisha na chama .kwani kina manyangumi wanaonyonya watanzania wangapi na bado wanadunda ndani ya chama??? Wana wafuasi lukuki ndani ya chama? Jambazi Chenge si peke Yake anaenuka ujambazi ndani ya hilo li chama . Leo ni ngumu kutafuta mtu ndani ya chama asiyeguswa na ujambazi. Chenge analaumuwa tu kwa kuwa ni jambazi Sugu ndani ya chama ila ma jambazi ni mengi sana na yanareflect chama hivyo chama ndo kinajichimbia kaburi chenyewe. Ni dhahri kuwa chama kimekuwa na nafasi kubwa mno ya kutubu na kubatizwa tena kwa maji mengi ila usugu umekuwa muthiri ya vile vidole vinavyikataa mashine ya mpiga kura .View attachment 230242
Hatimaye nyoka mwenye makengeza ameweza kupuruchuka kuwekwa kikaangoni kwa kukiuka maadili ya Uongozi wa Umma.
Malalamiko dhidi yake yalikuwa yasikilizwe tangu juzi tarehe 24/2/2015 ambapo aliibuka barazani akiwa na court injuction kulizuia Baraza la Maadili kumhoji kwa kuwa kesi yake ipo mahakamani hivyo asihojiwe katika Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma hadi kesi yake itakapotolewa uamuzi na mahakama inayosikiliza kesi ya awali kuhusu ESCROW. Kama haitoshi huku akijua Baraza linaweza kuja na maamuzi ya kutupilia mbali ZUIO lake ameamua kukata rufaa Mahakama Kuu kuhusu ufafanuzi wa yeye kuhojiwa na Baraza la Maadili kuhusu ESCROW.
Fafanuzi nyingi zilizotolewa na weledi wa Sheria ni kwamba, kimsingi Baraza lilanolisikiza malalamiko dhidi ya Chenge na wenzake haliingilii kesi za msingi ama zinazoendelea kwenye mahakama. Kwani hakuna kesi inayohusu kukiukwa maadili ya Uongozi ambayo imewahi kufunguliwa mahakamani kuhusiana na sakata la ujambazi wa pesa kutoka ESCROW Account. Hivyo pia Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi haina penal code zaidi sana inaishia kutoa ushauri kwa mamlaka husika kuhusu uthibitisho wa malalamiko dhidi ya mlalamikiwaji ili hatua stahiki zichukuliwe ambazo inawezekana mtu akaondolewa ktk nafasi yake ya uongozi, kushtakiwa mahakamani, kufilisiwa ama hatua zingine zozote za kinidhamu.
Chenge, ametia aibu kubwa taaluma ya Wanasheria nchini, siyo tu kutajwa bali kwa ushahidi ameshiriki matukio mengi kama siyo yote makubwa ya kijambazi dhidi ya pesa za umma, mikataba yenye utata na hata kufikia uhalifu wa kuficha pesa nje ya nchi ambazo yeye anaziita vijisenti. Inawezekana anayafanya haya akijua ukweli wa ndani kabisa kuwa hakuna wa kumchukulia hatua kwani aliwahi kuwa Mwanasheria Mkuu na anajua wapi abane na wapi ajifiche kupitia sheria ambazo amewahi kuwa msimamizi wake mkuu. Mchezo uliochezwa mbele ya Baraza la Sekretarieti ya Maadili hauvumiliki na haupendezi hata kidogo.
Narejea maneno ya Baba wa Taifa aliposema "Bila CCM IMARA nchi itayumba" hii kauli ni fupi lakini nzito na ina mantiki kubwa sana. Tukiamua leo kuandika historia ya uimara wa CCM itakuja kugundulika kwamba ilishakwenda na Nyerere.
Kuvumilia uozo imekuwa hulka yetu sisi Watanzania wa leo. Ukiwaacha viongozi ambao kwao uozo ni godoro la sufi la kulalia, sisi wananchi tumefikia mahala kuwaenzi wahuni wanaowajibishwa kwa kukiuka miiko ya uongozi na tunawapokea majimboni kama washindi na wafalme, ndiyo maana mtu kama Chenge amepewa hadhi ya Uchifu huko kwao, Siyo kwa sababu ya uongozi wake bali kwa sababu ya wingi wa pesa alizoiba na ubabe wa kipuuzi dhidi ya dola na watu hivyo ameonekana ni shujaa.
Leo tunaendelea kuwaita waheshimiwa wale wote wanaotukejeli na kutupuuza na tunaendelea kuwapa kura kwa kishindo eti Chama kisianguke. Tunashindwa kuwawajibisha majizi na hatimaye tunawapa another round for the road wakati tunajua ni madereva wanaopaswa kutuendesha bila ulevi wa madaraka....
Jeuri ya Chenge kusema kwamba yeye ni NYOKA mwenye makengeza anayeangalia mahala pesa ilipo si ya kuichekea hata kidogo. Hivi tangu lini uongozi ukawa ni mtaji wa biashara? Je sanduku la kura ndilo linaloamua nani awe tajiri na nani awe maskini? Inawezekana hii kasumba imeanza kutulevya Watanzania na tukafikia kuona kwamba hayo ndiyo majaliwa yetu. Tukatae kabisa upuuzi, wizi na uozo kwenye maongozi ya nchi. Hii jeuri anayoendelea kuionyesha Chenge ni dalili mbaya sana kwa CCM.
Ikumbukwe kwamba Chenge ndiye mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Chama kitaifa, yeye ameonyesha mfano mbaya kimaadili na bado hakuna mtu ndani ya chama anayestuka na biashara inaendelea kama kawaida. Ina maana bila Chenge nchi itayumba? Uimara wa CCM umepukutika na nchi inayumba sana. Muda bado ungalipo ili chama kijisafishe kiingie ktk ngwe ya uchaguzi kikiwa kimetakata. Watanzania wanazidi kufunguka fahamu zao na sasa wanaelekea kuchoshwa na mwenendo wa kulindana na kuoneana haya katika masuala ya msingi ya kitaifa.
Katika msahafu wa Wakristo imetajwa kwamba Mungu ni baba yetu, na pia shetani ni baba wa waovu. Sisi watanzania tulimchagua mioyoni mwetu kuwa Nyerere awe Baba wa Taifa, hivyo napendekeza sasa Chenge aitwe baba wa UFISADI nchini.
Tatizo mnasukumwa na hisia kuliko ukweli na sheria. Je umeshajiuliza ikiwa kweli ni mchafu kiasi hicho mbona hajafukuzwa katika Chama na pia hajafikishwa mahakamani?
MkuuMtoa mada au ndg msanii. Mada yako ni nzuri sana ila naomba nikukosoe sehemu moja kuwa ujambazi wa Chenge ni kaburi la CCM . Siyo kweli Bali chama hiki ndo kinajichimbia hilo kaburi. Ndo utendaji wake unalea ujambazi ndani ya chama . Ujambambazi huu ni ngumu kuutenganisha na chama .kwani kina manyangumi wanaonyonya watanzania wangapi na bado wanadunda ndani ya chama??? Wana wafuasi lukuki ndani ya chama? Jambazi Chenge si peke Yake anaenuka ujambazi ndani ya hilo li chama . Leo ni ngumu kutafuta mtu ndani ya chama asiyeguswa na ujambazi. Chenge analaumuwa tu kwa kuwa ni jambazi Sugu ndani ya chama ila ma jambazi ni mengi sana na yanareflect chama hivyo chama ndo kinajichimbia kaburi chenyewe. Ni dhahri kuwa chama kimekuwa na nafasi kubwa mno ya kutubu na kubatizwa tena kwa maji mengi ila usugu umekuwa muthiri ya vile vidole vinavyikataa mashine ya mpiga kura .
Umeshahau
Na ni chenge aliyetunga katiba iliyoondoa maadili kama tunu ya taifa
Katiba hiyo inaitwa "Katiba bora" na MaCCM
Sasa hebu fikiri zaidi hapo
Hebu tuanze na sakata la rada (BAE) ambapo vyombo vya uchunguzi vya Uingereza vimemhusisha na rushwa aliyopokea na kuificha kwenye offshore account....
Naomba unitoe tongotongo kuhusu usafi wake hapo ili tusonge mbele na tuhuma zingine
Amekimbia.Bora umeuliza kwa ustaarabu na huyu nyoka mtoto asiyejua ujambazi wa baba nyoka ajibu kny ya babake . Akimaliza ya BAE, tutampa dozi nyingine tusonge mbele maana orodha ni ndefu.