Chenge apata pigo jingine Nec | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chenge apata pigo jingine Nec

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Zak Malang, Nov 11, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Nov 11, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Chenge apata pigo jingine NEC

  Fredy Azzah


  TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imetoa ufafanuzi wa viti sita vinavyosubiri uchaguzi wa majimbo saba unaotarajiwa kufanyika Jumapili ijayo, huku majina ya wanawake na watoto wa vigogo yakiachwa.

  Kwa mujibu wa Nec, viti hivyo vimegawanywa kwa vyama vitatu; CCM, Chadema na CUF kila chama kikipewa viti viwili na kwamba, hali hiyo inaweza kubadilishwa na tofauti ya kura za uchaguzi huo.

  Kulingana na taarifa hiyo, CCM ina viti 67, Chadema 25 na CUF 10 na kuongeza kuwa, idadi ya wabunge wa viti maalum wa CUF iliyotangazwa juzi ilikosewa hivi sasa watapata viti vinane wakisubiri matokeo ya Jumapili.

  Baadhi ya wanawake wa CCM ambao walipitishwa na orodha ya Nec imewatupa ni mke wa Mbunge wa Bariadi Mashariki, Andrew Chenge, Tinner, Kaslida Mgeni, Mboni Mhita na Janet Masaburi. Kwa mujibu wa Mwanasheria wa Nec, Venosa Mkwizu, kwa sasa CCM imepewa wabunge 65, Chadema 23 na CUF vinane, huku viti viwili kwa kila chama vikiachwa wazi kusubiri matokeo ya majimbo saba ambayo uchaguzi wake iliahirishwa kutokana na kasoro mbalimbali zilizokuwa kwenye karatasi za kupiga kura.

  "Majina mawili kwa kila chama, hatujayatoa kwa sababu tunasubiri matokeo ya majimbo hayo, tumefanya hivyo kwa sababu inawezakana kura zikabadilisha hesabu zetu…lakini kama haitoathiri basi, kila chama kitapata hao wabunge niliowaambia," alisema Mkwizu. Wabunge kutoka CCM ambao wametangazwa na Nec ni Lucy Owenya, Esther Matiko, Muhonga Ruhwanya, Anna Mallac, Paulina Gekul na Conjesta Rwamlaza. Wengine ni Suzan Kiwanga, Grace Kiwelu, Suzan Lyimo, Regia Mtema, Christowaja Mtinda, Anna Komu, Mwanamrisho Abama, Joyce Mukya, Leticia Nyerere na Naomi Kaihula.

  Majina mengine ni Chiku Abwao, Rose Kamili, Christina Lissu, Raya Ibrahim Hamis, Philipa Mturano, Mariam Msabaha na Rachel Mashishanga. Nec iliwataja wabunge wa CCM kuwa ni viongozi wakuu wawili wa Jumuiya ya Wanawake wa chama hicho (UWT), Sophia Simba na katibu wake, Amina Nassoro Makilagi. Wengine ni Gaudentia Mugosi Kabaka, Ummi Ally Mwalimu, Agnes Elias Hokororo, Martha Jachi Umbulla, Lucy Thomas Mayenga na Faida Mohamed Bakari.

  Walioteuliwa wengine ni Felista Bura, Kidawa Hamid Saleh, Stellah Manyanya, Maria Hewa, Hilda Cynthia Ngoye, Josephine Genzabuke na Esther Midimu. Wengine ni Maida Hamad Abdallah, Asha Mshimba Jecha, Zarina Madabida, Namalok Edward Sokoine, Munde Tambwe Abdallah, Benardetha Mushashu, Vicky Kamata, Pindi Chana, Fatuma Mikidadi, Gertrude Rwakatare, Betty Machangu, Diana Chilolo, Fakharia Shomari Khamis, Zaynabu Vulu, Abia Muhama Nyabakari, Pudenciana Kikwembe na Lediana Mng'ong'o.

  Wengine ni Sarah Msafiri, Catherine Magige, Ester Bulaya, Neema Hamid, Tauhida Cassian, Asha Mohamed Omari, Rita Mlaki, Anna Abdallah, Fenella Mukangara, Terezya Huvisa, Al-Shaymaa Kwegir na Margreth Mkanga. Angellah Kairuki, Zainab Kawawa, Mwanakhamis Kassim Said, Riziki Lulida, Devotha Likokola, Christina Ishengoma, Mariam Mfaki, Margreth Sitta, Subira Mgalu, Rita Kabati, Martha Mlata, Maua Daftari na Elizabeth Batenga. Wamo pia, Azza Hillal Hamad, Mary Mwanjelwa, Josephine Chengula, Bahati Ali Abeid, Kumbwa Makame Mbaraka, Rosweeter Kasikila, Anastazia Wambura na Mary Chatanda.
  Chanzo: Mwananchi
   
 2. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #2
  Nov 11, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,594
  Likes Received: 18,589
  Trophy Points: 280
  Nadhani mwandishi alikosea waiotajwa mwanzo sio kutoka CCM.
   
 3. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #3
  Nov 11, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,945
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  Tume ya Uchaguzi ya Taifa ni horrible - kwa maana hii kabla hata ya kura kupigwa na wananchi wao tayari wamekwisha panga matokeo. Kwa nini wasisubiri mpaka kura zihesabiwe na kuachana na ubashiri wao. Ni sawa na referee kutabiri mshindi wa mechi atakayochezesha yeye mwenyewe!
   
Loading...