chemchem zimekauka kilimanjaro | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

chemchem zimekauka kilimanjaro

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by rosemarie, Jul 21, 2012.

 1. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #1
  Jul 21, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  Ajabu na kweli, tumeshangazwa sana na baadhi ya chem chem muhimu sana hapa kilimanjaro kukauka na kuwa kavu kabisa,

  Nimekulia hapa moshi machame na tangu kuzaliwa kwangu tumekuwa tukitumia maji ya chem chem yanayopatikana sehemu mbali mbali hasa hapa mto weru weru, cha kushangaza zote zimekauka na hazitoi maji kabisa,

  Inashangaza kweli kweli na inaonyesha kuna hatari kubwa inakuja,

  Jamani jiandaeni na makubwa yanayotujia kwani hii ni ishara mbaya kabisa
   
 2. Vmark.

  Vmark. JF-Expert Member

  #2
  Jul 21, 2012
  Joined: Aug 2, 2011
  Messages: 1,361
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 0
  Kuna miti ya eucalyptus ambayo imeoteshwa kwa wingi sana maeneo yua Rombo na ina absorb maji kwa wingi sana so i think that can be a reason...........correct me from the wrong.......
   
 3. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #3
  Jul 21, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,224
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  you are wrong, eucalyptus spp gani unayodhani inanyonya maji?!, its a wrong conception.
   
 4. L

  Luluka JF-Expert Member

  #4
  Jul 21, 2012
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ni mabadiliko ya hali za hewa kutokana na uharibifu wa mazingira uliokithiri!kwani huoni hata hali ya hewa k'njaro imebadilika ukilinganisha na zamani??ndo hali halisi iliyopo na mengi yanakuja!!poor k'njr.
   
 5. SWEEPER

  SWEEPER JF-Expert Member

  #5
  Jul 21, 2012
  Joined: Jul 16, 2012
  Messages: 265
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Climate change @work. The worst is still to come
   
 6. malema 1989

  malema 1989 JF-Expert Member

  #6
  Jul 21, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 848
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  wakazi wengi wa kilimanjaro wanajitahidi sana kutunza mazingira hasa kwa kuotesha miti na kulinda uoto wa asili. Tatizo kubwa la chemchem kukauka kilimanjaro ni uchafuzi wa mazingira unaofanywa na mataifa makubwa ya magharibi kupitia viwanda vyao vinavyozalisha hewa ya ukaa kwa kiasi kikubwa. Suluhu hapa naona ni mataifa machanga kuendelea kwa umoja kuyabana mataifa makubwa ili kupunguza uzalishaji wa "green house gases" hadi kufikia kiwango kile kilichokubalika kwenye itifaki ya kyoto kwa kuanzia bila unafiki na kusalitiana.
   
 7. Lyamungo

  Lyamungo Member

  #7
  Jul 22, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 91
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  nouma mbe
   
 8. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #8
  Jul 22, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,354
  Trophy Points: 280
  pia ukataji miti na mioto ya milimani imekuwa deal baad aya kuondoa kahawa kipindi kile watu walikuwa wamekasirika ,KNCU ilipofilisika.Kilimanjaro sasa hivi ina joto kali sana na kwa vile hakuna water body karibu hakuna evaporation na pepo za kutokea pwani zimebadili muelekeo,sasa hivi kilimnjaro inategemea mvua za mistu ya congo ambazo ni kidogo sana kuweza fikwa kwa wingi.

  Pia zoezi la kutanua mabomb aya maji kuelekea Moshi mjini lilifanyika kibaguzi ili kulazimisha watu wachukue maji ya kulipia na si yale ya kijiji toka katika chemichemi ndogondogo ambazo piazilikuwa zikitirisha mifereji ambayo ilitumika kunyeshea mashamba ya migomba, mbogboga na mambo mengine.Sasa sehemu nyingi za tambarare za mteremko wa mlima kilimnjaro hazina miti wana cover za kulinda ardhi isikauke.

  Wawekezaji wa maua na kahawa na viwanda (vya maji, bia,madawa,etc )wameteka maji yote kwa ajili ya matumizi yao.Siku hizi hata vimifereji vilivyokuwa vikipita kila mitaa na kupendwa na watu kiasi ch akuweka ulinzi kwa mifereji katika mitaa inayopitwa na hivi vifereji.Maji yalikuwa yakisafiri umbali mrefu yakiwa safi na baridi bil akuchafuliwa.tukitoka shule palikuw na mashamba mengi tuliyoweza kula miwa, mapera, maparachini, maembe ,zambarau ,ngoda, vidoo ,matopetope, etc .Tulikuwa tunapita katika kivuli kwa umbalia mrefu huku tukigombana na wenye mashamba kwa jinsi tulivyokuwa tukijihudumia katik mashamba yao.Wengi wa wanafamilia zenye mshamba walitukimbiza tuu ili kutuonyesha kuwa hatukupashwa haribu matunda ila kuchuma na kula vyema.now maneeo yamekuwa kipara kama dodma, haydom, mbulu, kondoa etc.

  Pia mashamba ya maua yamekuwa yakipiga mabomu kuzuia mvua kijnaja usiku.
   
 9. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #9
  Jul 22, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,684
  Likes Received: 641
  Trophy Points: 280
  globulus
   
 10. georgeallen

  georgeallen JF-Expert Member

  #10
  Jul 22, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 3,758
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Sasa ndiyo mtajua pesa au uhai (maji) ndiyo muhimu. Tuliwakataza /tuliwaonya/tuliwaelimisha madhara ya kukata miti mkatuona sisi mafala. Kila aina ya mti na hata miembe, mifuruanje, misesewe, mififina, mieresi, etc mlikata kwa ajili ya mbao na chapaa ya kununulia kisusio na wari.
   
 11. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #11
  Jul 22, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,289
  Likes Received: 22,057
  Trophy Points: 280
  Mazingira mmehariu wenyewe>
  Kule Narumu hadi Lyamungo sinde mmefyeka hovyo misitu kwa kisingizio cha kuanzisha mashamba ya kahawa.
  Mbaya zaidi kahawa yenyewe hamlimi tena
   
 12. Msalagambwe

  Msalagambwe JF-Expert Member

  #12
  Jul 22, 2012
  Joined: Jul 11, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Kuna aina 7000 za Eucalyptus aina zilizo nyingi ni miti ya kawaida chache hufyonza maji na kukausha visima.
  Si kweli kwamba aina yote ya miti hii hukausha maji,
  vilevile si kweli kwamba aina yote ya miti hii haikaushi maji.

  "While the Eucalyptus tree offers a great deal of benefits, it's also known to severely impact the environment. The thirsty roots of the Eucalyptus tree lower the water table, dry up streams, deplete soil moisture, and exhaust soil nutrients and fertility.
  "
   
 13. malema 1989

  malema 1989 JF-Expert Member

  #13
  Jul 22, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 848
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  acha majungu! na tuendelee kusaidiana ni nini tufanye ili kuokoa hili jahazi, sasa si wakati wa lawama. Hali ni ya kutisha kwelikweli Mifongo yote ya umwagiliaji na matumizi mengine ya kifamilia kwisha habari yake. Tusipoangalia kizazi kijacho kitabakia na historia tu ambayo haitatusaidia chochote.
   
 14. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #14
  Jul 22, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Bila kulaumu waliotufikisha hapa, itakuwa vigumu kufahamu kilichotufikisha hapa. Hivyo acha tulaumiane na hiyo itasaidia kupata ufumbuzi
   
 15. Ulimate4

  Ulimate4 Member

  #15
  Jul 22, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kaa chini mtafute njia m-badala ,pia kuondoa fikra kuwa kila kitu unaweza kukigeuza fedha, ukianza na wewe mtoa hoja anza kuonesha mabadiliko na uhamasishaji juu ya hilo, utunzaji wa vyanzo vya maji na mazingira kwa ujumla.
   
 16. babe S

  babe S JF-Expert Member

  #16
  Jul 22, 2012
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 3,703
  Likes Received: 19,819
  Trophy Points: 280
  Matunda ya uharibifu wa mazingira hayo
   
 17. Vmark.

  Vmark. JF-Expert Member

  #17
  Jul 22, 2012
  Joined: Aug 2, 2011
  Messages: 1,361
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 0
  Put the correct one then..........
   
Loading...