Kudo
JF-Expert Member
- Nov 2, 2017
- 1,809
- 6,081
RIWAYA; CHELEWA UZIKWE!
NA; BAHATI K MWAMBA
SIMU; 0758573660/0624155629.
DAR ES SALAAM….
Kelele za muito wa simu zilimuamsha katikati ya usiku mnene. Alijivuta kivivu huku akijaribu kushindana na uzito wa macho yake. Aliifikia simu yake na kutazama mpigaji.
Haraka alinyanyuka kitandani na kukaa kitako, huku akibonyeza kitufe cha kupokelea na usingizi ukiwa umempaa.
Masikio yake yalinasa sauti za hekaheka na mihemo ya hofu kutoka kwa mtu aliyepiga simu usiku huo. Licha ya kusikia hekaheka hizo, lakini aliamua kukaa kimya kama alivyokuwa amefanya mpigaji.
Udadisi mwingi kuhusu kilichokuwa kikiendelea upande wa pili, ulimfanya atulie kama aliyekuwa amepigwa na shoti ya umeme usingizini, hata mapigo yake ya moyo yalipunguza kasi ya kudunda, ili mradi aweze kusikia kila kilichokuwa kinaendelea.
Licha ya kusikia purukushani nyingi, lakini hakuweza kuelewa ni tukio gani hasa, lililokuwa linaendelea.
Alijikuta akisimama bila kupenda, huku tamaa ya kutaka kuelewa, ikizidi kuichota nafsi yake.
“Nipo matatizoni bwana Zuki!” Hatimae sauti ya mtu upande wa pili ilisema kwa kitetemeshi.
“Unaweza kunieleza kwa uchache?” Zuki aliuliza huku akijaribu kuweka umakini mkubwa, ili aweze kusikia jambo.
“Nimevamiwa nyumbani usiku huu, walinzi wangu wameuawa, familia yangu ipo matatizoni Zuki!” Sauti upande wa pili ilisikika kwa mbali sana, dhahiri muongeaji alikuwa hataki kuongea kwa sauti.
Kuvamiwa kwa yule mtu aliyepiga simu, kulimfanya Zuki Gado p.a.k Miguu ya kuku, apigwe na ganzi kwa sekunde kadhaa.
Kwa nini?
Kwa sababu alimfahamu vema mtu huyo, alifahamu ulinzi mkali aliyokuwa nao pia alifahamu nyumba yake ililindwa saa ishirini na nne tena kwa ulinzi wa kisasa kabisa. Ilikuwa ni ajabu kusikia kumefanyika uvamizi nyumbani kwake, kiasi cha kumfanya akimbia na kujificha.
Ilimshangaza!
“Uvamizi umetokeaje na….” Hakumalizia swali lake, jamaa upande wa pili aliingilia..
“Sijui kilichotokea, lakini kiufupi nimevamiwa na hapa muda wowote watanifikia.. Wanaonekana kuijua vema nyumba yangu” Jamaa aliongea kwa hofu huku dhahiri, akisikika akitetemeka kiasi cha kufanya taya zake zigongane.
“Hapo ulipo unaweza kutoka na ukakimbia?” Miguu ya kuku alimuuliza, huku haraka akichomoka chumbani kwake, akiwa amevaa boksa tu na wala hakujali.
“Naweza na sipo mbali na gari langu”
“Good! Ingia kwenye hilo gari na uondoke hapo haraka sana, lakini usikate simu yako, funga vioo vizuri na ukimbize gari kama umetoka kuiba benki”
“Sawa!” Jamaa alijibu na kukaa kimya. Upande wa pili Miguu ya kuku aliendelea kusikia harakati za yule bwana, akifuata maelekezo aliyompa.
Wakati simu yake ikiwa sikioni, miguu yake ilikuwa inapishana kwa kasi kuelekea kwenye chumba chake cha siri.
Sekunde chache baadae, alikuwa anatungua funguo za gari lake na kuanza kurejea sebuleni kwake.
Wakati wote huo, bado hakuwa amevaa nguo zake na alikuwa amesitiriwa na boksa pekee lakini, mwili wake wote ulikuwa wazi bila nguo.
Alipofika sebuleni akaitua simu yake kwenye sofa, kisha akachukua kompyuta yake iliyokuwa kwenye sofa jingine na kuiwasha.
Ilipowaka, alibonyeza hapa na pale na kisha akaingiza namba za simu yake na namba za yule mtu aliyempigia.
Sekunde chache baadae, aliweza kuona mahali ilipokuwa simu iliyompigia, kupitia ramani ndani ya simu yake.
“Wameniungia kwa nyuma, wako kasi sana….” Jamaa aliongea kwa hofu huku akiwa anatetemeka. Sauti yake ilimfikia vema Miguu ya kuku, kupitia simu yake.
“Vuta pumzi mara tatu na uziachie mara moja, kisha endesha gari bila kutazama viona nyuma” Alimwambia huku yeye akielekea nje.
“Wako kasi sana na wameanza kunishambulia kwa risasi..” Jamaa alilalamika tena.
“Unatumia gari gani?” Miguu ya kuku aliuliza huku akiingia kwenye gari lake na kuliwasha.
“Natumia Vx V8!”
“ Wao umeona wanatumia gari za aina gani?”
“Nahisi ni V8 zile!”
“Sasa tulia na usukani, waachie manyoya. Hawawezi kukupata na vigari vyao!”
“Natetemeka tatizo!”
“Fanya nilivyokwambia, ondoa hofu, nipo njiani”
“Nielekee wapi? Wako nyuma kwa kasi sana aisee!”
Miguu ya kuku aliwaza kidogo, kisha alimiiliza huku akiangalia kwenye simu yake ambayo aliunganisha ili aweze kuona aliyempigia alikuwa sehemu gani.
“Umefika sehemu gani sasa hivi?”
“Niko Moroko, Kinondoni!”
“Basi, elekea Koko”
“Whaat!!”
“Usishangae, elekea Koko beach kisha nisubiri hapo”
“Utatoka Tegeta saa ngapi hadi ufike huku mzee, huoni nitauawa hapohapo Koko!?”
“Leo nililala kwenye nyumba yangu ya Magomeni, ninahakika nitafika kabla hawajakuua!”
“Com'oon Zukii!”
“Sasa utafuata maagizo yangu au nirudi kulala?”
“No! Nitafuata! Nitafuata!”
“Good! Sasa endesha na usiangalie wanaokufuata na usizime simu yako!”
“Lakini hujanambia nikifika huko nifanye nini!”
“Zamisha gari kwenye maji!”
“Eeh!!?”
“Ndiyo! Nenda uingize gari baharini hadi injini yake izime yenyewe”
“Nitakufa Zuki!”
“Hautakufa, ukikaribia kufika washa kiyoyozi hadi mwisho, kisha funga vioo vyote na ukanyage mafuta hadi mwisho ili iwahi kupotelea majini”
“Nitakufa bwana!”
“Unaniamini au huniami?”
“Nakuamini!”
“Fanya niliyokuelekeza. Hutakufa kwa sababu itakuchukua dakika kumi na tano kuanza kupoteza hewa ukiwa ndani ya gari lililoko majini na itakuchukua dakika ishirini zaidi, gari kuingiza maji baada ya vioo kuzidiwa uwezo. Hivyo basi, fanya ninayokuelekeza ila kikubwa, usizime simu yako na ukiizima kweli utakufa, maana sitaweza kukuona ulipo” Miguu ya kuku aliongea huku akiweka simu pembeni na kuongeza mwendo wa gari lake.
Lilikuwa ni jambo la hatari aliloamua kulifanya ili kuweza kuokoa maisha ya mtu aliyempigia simu usiku huo, lakini hakuwa na la kufanya zaidi ya hilo jambo.
“Hatari lakini salama!” Alijisemea huku akiongeza kasi kuelekea kinondoni.
“Nimekaribia kufika, jamaa na wao naona hawajakata tamaa!” Jamaa aliongea kwa kitetemeshi cha uoga.
“Washangaze hao jamaa!” Miguu ya kuku alimwambia huku akikunja kona kupita maeneo ya ubalozi wa Marekani, maeneo ambayo yalitawaliwa na ukimywa mkubwa, lakini yeye hakujali. Ilikuwa ni lazima awahi kufika kwenye fukwe za Koko ili atoe msaada kwa mtu aliyempigia simu.
Gari lake aliliendesha kwa kasi kubwa huku mara chache ikimlazimu kupunguza kasi, ili aweze kumudu kukunja kona. Kila mara macho yake yalikuwa yanatizama simu yake, ili kuweza kupima umbali aliobakiza kufika ufukweni.
Zikiwa zimesalia mita kadhaa ili afike sehemu alipokuwa mtu wake, masikio yake yalinasa sauti za risasi mfululizo. Haraka alizima taa za gari lake, kisha alipapasa kwenye kiti, kushoto kwake na kuibuka na bastola aliyoipenda kuliko bastola zote alizowahi kumiliki.
Ilikuwa ni bastola aina ya USA Colt M1911, bastola ambayo ilikuwa na uwezo anaouhitaji kwenye misukosuko ya aina yoyote ile.
Alipokwisha kuitwaa, alirudisha umakini kwenye kwenye gari, kisha alianza kupunguza kasi ya gari lake huku masikio yake yakizidi kusikia sauti za risasi zikirindima bila mpangilio.
Alisimamisha gari akiwa amebakiza mita mia moja tu, ili awafikie wale waliokuwa wakipiga risasi upande wa bahari.
Aliegesha gari kandoni mwa barabara, kisha aliinyakua simu yake na kushuka ndani ya gari huku bastola ikiwa mkononi, tayari kwa lolote.
Alianza kupiga hatua zake huku macho yake yakiwa makini, kutazama kioo cha simu yake. Lengo lake ajue uelekeo wa ilipokuwa simu iliyompigia.
Alijikuta akisimama baada ya kuona uelekeo wa simu aliyoiunganisha. Uelekeo ulisomeka ni mita zaidi ya mia mbili kutoka pale alipokuwa.
Aliinua macho yake na kutazama kule alikoona mtu wake atakuwepo. Makadirio yake yalionesha tayari mtu yule atakuwa amelitosa gari ndani ya maji, hivyo alikuwa anasubiri msaada wake.
“Kumekucha!” Alisema huku akijaribu kuiweka simu mfukoni.
“Heh!” Alishangaa baada ya mkono kukosa mfuko na alipojitazama, aligundua alikurupuka kitandani bila kuvaa nguo zaidi ya boksa aliyokuwa nayo.
Alitamani kujicheka, lakini wakati haukuruhusu. Alichoamua kufanya ni kupindua pindo la boksa yake na kuipachika simu yake ili aingie mapambanoni kabla ya dakika kumi na tano kuisha.
Wakati akikimbia kwa kuambaa na ufukwe, huku akili yake ikiwa kwa wale jamaa waliokuwa wamesimama na kishambulia baharini, bila kumuona waliemshambulia, masikio yake yaliendelea kumpa tahadhari ambayo tangu awali, hakuwa ameizingatia.
Alisimama na kufumba macho na kuyaruhusu masikio yake yasikie kile ambacho hakuwa amekizingatia.
Gafla alifumbua macho mithili ya mtu aliyeona kibwengo gizani, tayari alikuwa ameshatambua kile kilichosikilizwa na masikio yake.
Milio ya risasi!
Risasi zilikuwa zinatoka kwenye bunduki kubwa na za kisasa, bunduki ambazo hazikuwa zikipatikana hapa nchini na hata kama zilikuwepo, si rahisi kuingia mikononi mwa walugaluga.
“Automatic Riffleman!?” Alishangaa na kujiuliza bila majibu, lakini hakuwahi kutilia shaka uwezo wa masikio yake na utambuzi wa silaha.
“Huu ni mziki ambao unavuka kina!” Alijisemea huku akijaribu kuwaza njia mbadala ili kutokuingia kwenye mapambano ya risasi na watu wale, ambao walionekana kutumia silaha za kisasa zaidi na kwamwe isingelikuwa busara kutupiana risasi.
Alitazama kushoto kwake na kuiona barabara, kulia kwake kukiwa na kingo za maji. Alipotizama mbele aliona gari za wale watu ambao walikuwa bado wanarusha risasi.
Akawaza kufanya jambo!
ENDELEA KUWA NAMI