cheka seke seke la kitaa

Bin wamakamo

Member
Dec 12, 2021
77
92
Seke seke la kitaa
Na bindondora
************

"Yule jamaa katoka sauz ni mgeni kabisa hapa tz , sasa nasikieni karudi na mapuri ya bange kibao"
"Sasa sie tunavuta bangi? Akazungumza kwa zarau mwana kijiwe mmoja aliyeketi mwisho kabisa mwa benchi.
"Wewe mwehu kumbe maada gani za kuleta kijiweni mapuri na bangi yake siye yanatuhusu nini? Akawaka tena
"Sikieni sasa mie ninawazo" akasisitiza baada ya kuona aeleweki.

Kijiwe chote kimya kikuu kika tawala kusikia wazo.

"Mahesabu ya haraka haraka yule jamaa hawezi kukosa jiwe moja pale alipo" akameza fundo la mate.
"Eeh sasa kama ana iyo millioni moja sie tufanyaje" akajibu kipuuzi yule aliyekaa mwisho kabisa mwa benchi akazidi kumuandama mtoa wazo.

"Sikia sasa na wewe munaonaje tukajifanya sie polisi."
"Polisi bila kitambulisho bila fom nawe izo bangi unazosema ushaanza kuzivuta", akadakia kijana mwengine aliyevaa shati la daimondi baba lao aliyekaa katikati mwa benchi.

"Wewe polisi wa sikuizi sio mpaka wavae form," akajitetea.
"Yule tunakwenda kumtingisha ela anazo yule muhindi," akaongea kinyonge baada ya kuona wazo lake alikupokelewa vyema.

Katika benchi walikaa watu watatu wa kwanza alikuwa mtu mzima kiasi, aliye vaa shati la daimond baba lao na wa mwisho wao umri wao ulifanana awakuachana sana pamoja na aliye leta wazo.

Wa kwanza katika benchi yeye alitulia tulii kama mpiga chabo.

"Sema ilo mbona kama dili mujue," akazungumza kwa mkulupuko, sasa na kumfanya aliyetoa wazo amakinike kumtazama, kisha kusitisha zamila ya kukaa katika benchi.

"Huyu mshua anakaa wapi", akauliza kibabe.
"Ni hapo tu mtaa wa kati kwani mbali basi", akajibu mtoa wazo.
Kisha yule mtu mzima kiasi akaduwaa sekunde kazaa kisha kama kunakitu alikifikilia na kuinua kichwa akasema.

"Sikia ilo dili ujue mwanangu ngoja nikachukue zanaa tondoke dakika sifuri tu hapo yeye si muhindi ngoja tukamchezeshe picha la kivetnam", kisha akainuka nakuondoka na dakika kazaa akarudi na makoti matatu na mabuti na kuwagawia wenzake, hakuna aliyeweka pingamizi tena safari ikaanza.

"Sasa niite afande nani? "Propera" akasimama kisha akaongea yule mtu mzima kiasi na wote wakabaki kumtumbulia macho, "semeni ndio afande ".
Aka amrisha na wote wakajibu "ndio afandeeee".

"Wewe na wewe na wewe munisikilize" akaongea akiwanyoshea kidole cha shahada mmoja mmoja huku kichwa akikipeleka chini juu".
"Tukifika pale mie ndo afande mkuu sawa".
"Naitwa afande nani? "Propera", wakajibu.

Hawakukawia hatimae wakafika kisha propera akagonga mlango "ngoo ngoo ngoo".

"naniii?.
Upande wa ndani ukahoji.

"wewe njoo ufungue mlango" akajilazimisha kuongea kiafande afande.
"nije fungue lango sijui iko nani?
Muhindi upande wa pili akahoji kwa zarau.
"Afande kutoka kituo cha kati toka nje tunashida na wewe".
akafoka kwa gazabu propera baada ya kuona maswali yamezidi kisha akanong'ona.

" kama nilivyowambia akifungua tu mlango munaingia kwa fujo sawa? Wakaitikia kwa vichwa.
"Akiwa mbishi mbishi muna mkandamiza makonzi ya pua".

Akanong'ona tena kisha akaziba jicho moja nakutazama katika upenyo wa funguo kisha akanong'ona". Kuweni stend baii anakuja".

"Iko shida nini fande", akazungumza muhindi kwa woga.

"Oya atuhitaji maswali utafungua mwenyewe au ukanunue kitasa kipya " akafoka propera kisha akaugonga mlango kwa nguvu.

"Nakuja fande", akahamaki muhindi wenge likamtawala.

Mlango ukafunguliwa kisha wale vijana wakaingia kwa fujo kama walivyo ambiwa na kisha wakapekua kuwa kila sehemu wakafanikiwa kulipata lile roba lilifungashwa bangi.

Yule muhindi macho yakamtoka pima.

"yaani unatoka na mibange na kutuletea hapa tanzania unataka kuharibu nguvu kazi ya taifa letu".
Akang'aka propera kisha sura aka ikusanya utazani aliihitaji kuitia mfukoni, muhindi jasho lilimtoka kisawa sawa alitetemeka utani izirahel mtoa roho alikuwa mbele yake.

"Fande iko taka tuonge", akajitetea yule muhindi.

"Muonge nini unataka kumpa kamanda rushwa wewe".
Akaongea aliye vaa shati la daimond baba lao akifatisha kibao kilicho tua vyema katika kiwaza cha yule muhindi, rangi iliimuiva sura ilishaanza kuwa nyekundu miguu ilimchezacheza utani ilitaka kuchomoka.
"situ....".
Funga bakuri lako".
Akadakia sasa mtoa wazo alitunisha mishipa ya shingo utazani dada wa kimara baluti amemkamata danga aliyekimbia kulipa hela. Kisha akasema huku macho ameyatumbua.

"Uwo mdomo utasabibisha makonzi yaoteshe nywele kwenye icho kiwalaza chako"

Muhindi alichachawa propera na wenzake walijua kuicheza vema ile nafasi ya uwafande.

******************
"Unahitaji kuongea?" propera akatupa swali kwa muhindi aliyekuwa bado ameshikilia kiwalaza chake kilicho tandikwa kofi uku akijitahidi kuirudisha sura katika hali ya mnyoko.
"Utaenda kuongelea kituoni mbebeni huyo" akaongea kwa makini propera bila kuhitaji jibu la swali lake utazani ni kweli alihitaji kumpeleka kituoni yule muhindi.

Baada ya amri wale vijana walibaki kwenye pumbazo wasifanye kile kilicho amrishwa kisha kila mmoja alimuelekezea macho propera, propera akakonyeza kusisitiza kile alicho sema kisha wale vijana wakamshika kwa nguvu kumnyanyua.
"hapana fande usi fanye ivyo".
Akahamaki sasa muhindi baada ya kihisi harufu ya jera inanukia loo angejua!

"Iko na millioni kumi fande weza tuonge mimi gawia yote nyie".
Akasisitiza sasa na kufanya wala vijana nguvu ya kumshika ikose kane, million kumi gawia watu wanne izo ndo hesabu zilizo jipiga vichwani, kati ya wale nani angeacha fursa kama hiyo wakati iyo elfu hamsini walibaki kuisikia kwenye matangazo ya kuchangia.

Propera aliduwa kwenye kupiga hesabu ya mgao pia, sasa alishusha pumzi taratibu.
"Iyo pesa ni ndogo sanaa kwa kesi yako ongeza".

Akafoka na kufanya wale vijana wahisi propera aliwaletea mzaha kwenye jambo lile millioni kumi ni pesa ndogo asalale yule aliyetoa wazo sasa alihisi propera aliendelea kupoteza mda na kusahau kwamba wao awakuwa askari kweli.

Akamuonesha ishara ya kumwita kisha akasogea propera baada ya muhindi kugoma kuongeza hela ,
yule aliyetoa wazo akanong'ona sikioni mwa propera.

"Mwambie atoe iyo pesa tunazidi kupoteza mda umesahau kuwa siye siyo askari" akaitikia kwa kichwa propera kumanisha kuwa alimuelewa hoja yake.

"Toa iyo pesa" akamuamlisha yule muhindi kwa kumkazia macho.

Muhindi sasa aliona amepata walau hafua maana kamasi zilisha anza kumtoka taratibu puani , shati lote lilikwisha loa chini ya shingo kwa nyuma upande wa juu wa mgongo, alitetemeka ata funguo za kufungulia droo ambayo aliweka pesa aikuisha kumdondoka.

"Watu kama hawa ukiwasweka rupango watu gombania gombania kama yao".

Akatisha kwa kugezea rafudhi ya muhindi yule aliyevaa shati la daimond baba lao ambalo alilifunika vyema katika koti.

"Changamka wewe hatuna muda wakupoteza kabla atujabadili maamuzi".
Akang'aka sasa propera baada kuona yule muhindi mapepe ayakumuisha huku akikipigiza mkononi kilungu alichopewa katika kundi la walinzi shirikishi.

Mhindi alifungua droo kisha akatoa zile pesa zilizopo katika brifu kesi na kumkabizi propera, akili zikamtuma kama akimbie vile na moyo aukuisha kumtunda kwa kasi, mtoa wazo hakuamini kile alichokiona, akili kama ilianza kumruka.

Pesa ambazo hata kwa miaka ishirini asingekuwa na mpango wa kuzipata, leo hizi hapa anaziona zina kalibia mkononi mwake. Mzee wa daimond baba lao alijipiga kifuani na kujilaumu na kujilani kwanini aliwekea kipingamizi safari ile yenye matunda tele na hivyo hivyo kwa mwenzake.

"Tumekupa onyo ukiludia tena hatutakuwa salama na wewe serikali imechachama sana kwenye maswala ya madawa ya kulevya ivyo kuwa makini kwa mara ya pili utaenda kunyea debe", kwa kusihi akaongea propera huku akimnyoshea kidole.

Yule aliyetoa wazo aliona sasa wazi na yeye kumaliza scpirt yake alivuta pua ya yule muhindi kisha akaisigina kulia na kushoto bila kusema neno akamuacha muhindi akiugulia maumivu, huyu wa daimond baba lao nae akutaka kubaki nyuma alimshika na kumkwida shati lake kisha akabana meno na kugusisha kichwa cha yule muhindi na chake akasugua ilivyotosha alimuacha muhindi akiwa kwenye hali ya kusubiri yule wa mwisho angemfanya nini?

Mara mlango ukagongwa "naniii? Akauliza kinizamu propera kisha masikio yakawa haaa kama mbwa asiyekujua, si nilisema kijiweni kulitanda kimya kikuu kumsikiliza mtoa wazo sasa mara hii kilikuwa kimyaa kikuuu haswa.

"Kuanzia sasa mpo chini ya ulinzi mimi ni askari kutoka kituo cha bamia si hitaji kuona mtu yeyote asijalibu kuleta vurugu maana siitaji nimpeleke mtu kituo akiwa ameshatangulia mbele za haki na mavi yake" ukafoka upande wa nje na kuminya kitasa nacho bila ajizi kikakubali amri.

Propera alihisi mzunguko wa damu uliongezeka japo ni mtu mzima kiasi lakini udogoni mwake hakuwai kuwa na matatizo ya kujikojolea kitandani lakini bila hiyana taratibu ulirowesha suruari na kupenya katika mabuti yake.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom