Cheka aingia orodha ya mabondia bora IBF | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Cheka aingia orodha ya mabondia bora IBF

Discussion in 'Sports' started by engmtolera, Aug 14, 2012.

 1. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #1
  Aug 14, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Imani Makongoro
  BINGWA wa ngumi za kulipwa, Francis ‘SMG’ Cheka ameingia katika orodha ya mabondia bora 15 duniani wanaotambuliwa na Chama cha Masumbwi cha IBF.

  Cheka bingwa wa taji hilo Afrika ameingia kwenye orodha hiyo kufuatia viwango vya ubora vya dunia vya IBF vilivyotolewa hivi karibuni.

  Kwa viwango hivyo, bingwa huyo wa Afrika wa uzani wa super middle ana nafasi ya kuwania Ubingwa wa Dunia wa IBF dhidi ya mabingwa kutoka nchi mbalimbali ulimwenguni.

  Kwa mujibu wa Rais wa Chama cha Ndondi cha PST, Emmanuel Mlundwa, Cheka anaweza kuwania taji hilo dhidi ya Benjamin Simon na Henry Weberwa wa Ujerumani.

  "Mabondia wengine wanaoweza kucheza na Cheka kuwania ubingwa huo ni Maxim Vlasov wa Russia, Marco Periban wa Mexico na Ezequiel Maderna wa Argentina," alitaja Mlundwa.

  Wengine ni Paul Smith wa United Kingdom, Junior Talipeau na Serge Yannick (Australia), Nikola Sjekloca na Alexander Johnson (United States), Roman Shkarupa (United Kingdom), Luis Garcia (Ireland), Rudy Markussen (Denmark) na Fulgencio Zuniga wa Colombia.

  GAZETI MWANANCHI


   
Loading...