Check and Balance kwa Tanzania haipo, Spika anafanya kazi za Serikali

BLACK MOVEMENT

JF-Expert Member
Mar 11, 2020
2,720
6,527
Ni kitu cha hatari sana kukuta Spika wa Bunge eti anatembelewa na Wawekezaji. Hii inawezekana Tanzania pekee, hakuna nchi chini ya jua hata Somalia ambako spika wa Bunge anaweza kuwa too low kiwango hiki.

Hili la Spika kufanya kazi za Serikali lilianzia awamu ya Mwendazake ambako Ndugai aligeuka kuwa katibu mkuu mtendaji make kwenye Dhiara zote za Jiwe alikuwa lazima awepo.Sasa awamu hii naona kuna muendelezo tena kwa kasi sana. Spika wa Bunge anafanya kazi za Waziri mkuu.

Fikiria Wawekezaji wanaenda kuoanana na spika wa Bunge, na vipi hao wawekezajiikibainika kwa baadae kwamba kuna uhunu au ufisadi walifanya.Spika ataweze kuendesha kikao cha kuwajadili ilihali walimtembelea ofisini?

Kule Loliondo nako Spika anafanya sana kazi za Serikali yaani speed yake ya kuitetea Serikali ni kubwa kuliko ya Waziri Mkuu.
 
Keyword: Lobbying

Watu wanatafuta ushawishi, ili mambo yao yaende, has nothing to do na kuifanyia kazi serikali.

Ni kama aliepita baada ya kupata Mwaliko China akarudi na wimbo wa bandari ya Bagamoyo.
 
Back
Top Bottom