Chechen za rais mtarajiwa v/s haki ya mtumishi(ceo tanesko) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chechen za rais mtarajiwa v/s haki ya mtumishi(ceo tanesko)

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by UGWADU, Mar 30, 2012.

 1. U

  UGWADU Member

  #1
  Mar 30, 2012
  Joined: Feb 24, 2012
  Messages: 78
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 25


  [h=2]Agizo la CEO wa TANESCO kutokuwa na Jenereta[/h]Ndugu Wanamabadiliko,

  Nimeona ni vema nitoe ufafanuzi kuhusu suala la Kamati yangu kuiagiza bodi ya TANESCO kuondoa stahili ya 'standby generator' kwenye mkataba wake wa Kazi.

  Rationale

  Shirika la Ugavi wa Umeme nchini lina jukumu la kuhakikisha kuwa nishati ya umeme inapatikana kwa wananchi wote. Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO ndiye Mtanzania aliyepewa jukumu hilo na Taifa. Iwapo mkurugenzi mkuu wa TANESCO anawekewa stahili katika mkataba wake kwamba 'atapewa standby generator itakayolipiwa na Shirika' maana yake ni kwamba mgawo au kukatikakatika kwa umeme ni jambo litakalokuwepo tu. Kwamba Shirika linalopasa kuhakikisha kwamba Umeme unapatikana muda wote, Bosi wake anapewa stahili ya 'Generator' umeme ukikatika. Bosi huyu atajuaje machungu ya kutokuwepo Umeme? Morally this is wrong. Fundamentally this is a contradiction to CEO's mandate.

  Jambo hili ni dogo sana lakini lina maana kubwa sana. Bodi ya Wakurugenzi ya TANESCO haikupaswa kuweka stahili hii.

  Kuhusu wengine, kamati ya POAC haina mamlaka ya watu wengine. Mawaziri wapo kwenye kamati ya Makamba, kwenye POAC wanaohusika ni Bodi na CEO basi. Wanaonitaka kuagiza kwingine wananipa jukumu lisilo langu.

  Hata hivyo kimsingi, Waziri wa Nishati hapaswi kuwa na Jenereta nyumbani kwake, iwe ya kulipiwa na Serikali au ya kujilipia mwenyewe. This is politics at higher level - Next level kabisa. Tukubali kubadilika ndugu zangu. Haya ni mambo madogo yenye maana kubwa sana.

  Kuhusiana na tanesco kutopewa fedha. Kamati imekuwa kali sana kwa serikali. Kamati ilimwita Katibu Mkuu kuhusu suala hilo. Kamati imeagiza kwamba suala hilo limalizwe haraka iwezekanavyo.

  Kamati ya POAC inajitahidi sana kuhakikisha Mashirika ya Umma yanatimiza wajibu. Tunaomba mtuunge mkono na pale ambapo mnaona tumekosea, msitubeze bali mtueleze tujirekebishe. Kejeli, kurushiana maneno na kujadili mambo juu hakutasaidia Taifa letu. Tushirikiane, tusaidiane, tukosoane ili tusonge mbele kujenga Taifa letu zuri sana.

  Zitto
  Sent via my BlackBerry from Vodacom - let your email find you!


  [HR][/HR]

  [h=2]Ufafanuzi huo umepata maoni kadhaa, Richard Mgamba, yeye anasema:-[/h]Wana-mabadiliko,

  Tuache kuwa watu wa kufikiri kama vile sisi siyo binadamu. CEO kuwa na generator nyumbani kwake ni issue hapa? Maana hata mkinyang'anya kwa mshahara wake atanunua mpya kesho yake.

  Juzi hapa mliunga mkono madaktari kupewa posho stahili, mazingira mazuri ya kazi na pa kuishi, lakini leo mnataka CEO wa Tanesco, mhimili wa Uchumi wenu asiwe na generator ili nayeye aonje machungu ya mgao.

  Kwa hiyo akionja fedha za Benki kesho yake zinatoka bure au mapato ya Tanesco ghafla la yanakuwa mabilioni toka mbinguni?

  Zitto anaongelea Morals hapa? Morals hizi zinakuwa na makengeza? Hii tabia ya heri wote tukose, ni ya ajabu na hatari sana.

  Tatizo la sasa ni Muhando na Generetor yake au Serikali na Tanesco yake?

  Kuna vyeo ambavyo huja na maslahi kibao, na watu wengi tu wanafaidi akiwemo mkuu wa TRA, BOT, na kwingineko, sasa kama swala ni hilo, then Zitto aache Makengeza. Nimesema hata mikopo isiyo na riba ya bure ya kununua mashangingi waache basi kweli wanayo morals.

  Morals gani hiyo wakati wabunge wamekopa mashangingi bure huku Rais akiahidi Bajaji kama ambulance za wagonjwa?

  Tatueni kero ya umeme acheni siasa za chuki na kuchimbana.


  [HR][/HR]  Source: Previous Posts - wavuti.comĀ 
   
 2. HISIA KALI

  HISIA KALI JF-Expert Member

  #2
  Mar 30, 2012
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 694
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  mimi naunga mkono kamati kwa uamuzi wake wa kuondoa hiyo stahili ya mkurugenzi wa tanesco pamoja na wafanyakazi wengine kuwa na generators zinazoendeshwa kwa fedha za tanesco kwenye nyumba zao kuishi. Morally this is right decision. Big up kamati.
   
 3. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #3
  Mar 30, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,524
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  uamuzi umegubikwa na jazba.
   
 4. m

  moshingi JF-Expert Member

  #4
  Mar 30, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 278
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pamoja na kwamba, morally you were right, but legally you were wrong as per principle of privity of contract.
  "A third party cannot acquire rights under a contract to which he is not a party."
  Kamati ya bunge siyo sehemu
  ya mkataba kati ya Mkurugenzi wa Tanesco na bodi ya Tanesco, hivyo kisheria hawana haki ya kuuingilia mkataba huo.
  Mnachoweza kukifanya ni kuiwajibisha political figure kwa kuruhusu mkataba wa aina hiyo.
   
Loading...