Master Legendary
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 579
- 887
Nimewasikiliza hawa jamaa naona kama kuna kuchanganyikiwa flani hivi au wana hasira za kutoka CHADEMA kiasi cha kupoteza Dira na kutumia Mikutano yao waliyoiandaa kwa Gharama kubwa kuisakama CHADEMA badala ya CCM, siyo kwamba wanarudia kosa walilofanya ACT?
Lengo la Chama chochote cha Siasa ni kushika Dola inakuwaje sasa wao wanaishambulia CHADEMA ambayo haina Dola na kuacha Chama kilichoshika Dola?Hii si itathibitisha sasa kwamba wanafanya kazi ya Bosi?
Nimemsikiliza Salum Mwalimu analalamika anadai hela zake CHADEMA, yeye si alikuwa Kiongozi Mkubwa tu alipotoka na walisema Sekretariet yote wanaingia CHAUMMA sasa kama hawakuwajibika kiasi cha watu kutolipwa katika kipindi chao wanamlaumu nani?
Analia sana CHADEMA waingie kwenye Uchaguzi, kama yeye anaona Mazingira ni rafiki na atashinda kwanini asinadi sera zake akaingia ulingoni kuliko kulazimisha wanaoona mazingira hayaruhusu waingie.
Anyway hoja kubwa ni ndani ya muda huu mfupi ni wapi zimepatikana Fedha nyingi hivi za kufadhili Mikutano ya CHAUMMA kwa kujenga Majukwaa ya Gharama, Misafara ya Magari, helikopta,Pikipiki nk.
Kuna mtu anaona ninachoona hapa?Au niendelee tu na mtori?