Chatu mkubwa azua taharuki Isyesye-Mbeya

Chatu mkubwa azua taharuki Isyesye-Mbeya

Ikaria

Member
Joined
Jul 17, 2019
Posts
93
Reaction score
238
Wananchi wa kata ya Isyese sokoni katika mkoa wa Mbeya wamekumbwa na taharuki baada ya sanduku lenye chatu mkubwa kupatikana katika eneo la wazi.

Chatu huyo amechukuliwa na na maafisa wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kwa ajili ya kuhifadhiwa.

20210311_175628.jpg
 
Unapigapicha kwa woga, mbona taharuki hatuzioni, acha kutengeneza taharuki ambayo haipo.
 
Hivi huyo nyoka haliwi kweli maana huko kusini kwa kula mivitu ya ajabu ajabu hawajambo
 
Mbeya kuna Matukio ya Kidwanzi! Mara Sanduku la Maiti litelekezwe! Leo sanduku la Chatu ukiingia ndani saaana ni Ulozi hakuna namna
 
Vikundi vingi vya utamaduni wanawatumia hao kucheza..maybe wameshindwa kumuhudumia maana nasikia wanakula balaaaa....wamekuja kumtelekeza badala ya kumuua...
 
Wananchi wa kata ya Isyese sokoni katika mkoa wa Mbeya wamekumbwa na taharuki baada ya sanduku lenye chatu mkubwa kupatikana katika eneo la wazi.

Chatu huyo amechukuliwa na na maafisa wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kwa ajili ya kuhifadhiwa.

View attachment 1722913
Nimecheka sana asubuhi wakati napita kuelekea kazini ikabidi nisimame nami nishuhidie hilo dubwana. Wahuni walidhani ni mali imetelekezwa, walichukua trunker na kwenda kuvunja kufuri zilizokuwa zimefunga hilo trunker baada ya kuliona hilo dude wakarudishia na kulirudisha hilo trunker palepale barabarani walipolikuta.
Huyu nyoka yaonekana ameletwa na mtu aliyekuwa akimfuga kwasababu uwanda ule wote hauna nyoka wakubwa Aina ya chatu.
 
Back
Top Bottom