tonicimmobility
JF-Expert Member
- Jun 17, 2025
- 493
- 1,038
Mkufunzi kutoka Chuo cha Uhifadhi Wanyamapori cha Afrika, Mweka, Tito Lanoy, amesema wamefanikiwa kumwondoa nyoka aina ya chatu, ambaye alikutwa kwenye shamba la mfugaji akiwa amekamata kondoo na kummeza.
Tukio hilo limetokea leo, Agosti 14, 2025, eneo ni Dolly estate, Usa river, Arusha.
Soma pia: Fisi waua kondoo 21 Simiyu
“Chatu akisha shiba hukaaa mahali au karibu na mahali alikopata mawindo yake, ili kusubiri chakula kiyeyuke tumboni.
“Inakuwa vigumu kwake kutambaa wakati tumbo limeshiba. Hutumia wiki kadhaa mbili hadi nne, kwa chakula kuyeyuka tumboni kulingana na hali ya hewa,” amesema.
Amesema wakati wa baridi nyoka hawali kwa sababu miili yao haina uwezo wa kutengeneza joto, ili kuyeyusha chakula.