WABUNGE na madiwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), jana walisusa kushiriki uchaguzi wa Jumuiya za Serikali za Mitaa Tanzania (ALAT) katika Mkoa wa Arusha.
Walifikia hatua hiyo wakipinga uwepo wa Mbunge wa Viti maalumu kupitia Jumuiya ya Wanawake (UWT) wa Mkoa wa Tanga, Mery Chatanda katika mkutano huo.
Mbunge wa Jimbo la Karatu, Mchungaji Israel Natse ambaye alitaka ufafanuzi wa Chatanda kuwepo katika kikao hicho, kwa kuwa kanuni za Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) wabunge wanaopaswa kuhudhuria kikao hicho, ni wa Mkoa wa Arusha tu na sio vinginevyo.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa muda wa mkutano huo, Ismail Katamboi ambaye ni Diwani wa kata ya Kisongo, katika Halmashauri ya Arusha, alisema Chatanda ni mjumbe halali wa kikao hicho na kutaka shughuli za kikao hicho kuendelea.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Karatu, Lazaro Massay alisimama na kumtaka Katamboi kueleza kama Chatanda ni Mbunge wa Arusha ama Tanga.
Lakini Katamboi hakutaka kujibu swali hilo kama alivyotaka Massay bali alisisitiza kuwa Chatanga ni mjumbe halali wa mkutano huo wa Alat na hakutoa ufafanuzi zaidi.
Baada ya jibu hilo, Diwani Julius ole Sekayane (CCM) ambaye alimwakilisha Meya wa Jiji la Arusha, alisimama na kuwataka wajumbe kuendelea mkutano kwa kuwa Chatanda ni mjumbe halali katika mkutano huo na anayedai kuwa sio halali amekosea.
Baada ya malumbano hayo, wabunge wa Chadema, Natse wa Karatu na Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema na madiwani wote wa Chadema waliondoka ndani ya ukumbi wakisema hawako tayari kushiriki uchaguzi huo.
Natse akizungumza nje ya ukumbi, alisema Chatanda sio mjumbe halali na pili wao wanaungana na wenzao kusema kuwa hawamtambui Meya wa Jiji la Arusha Gaudence Lyimo kwani hakuchaguliwa kufuata kanuni za Tamisemi.
Mkutano huo wa Alat Mkoa wa Arusha hushirikisha wabunge wote wa mkoa, wenyeviti wa halmashauri za wilaya, wakurugenzi wa halmashauri zote na madiwani wawili waliochaguliwa na baraza la madiwani la wilaya husika.
Mkutano huo ulikuwa wa kumchagua Mwenyekiti wa Alat mkoa wa Arusha, mweka hazina, kamati ya utendaji na mbunge mwakilishi wa mkoa katika mkutano mkuu wa Alat Taifa.
Kibaya kwa wengi ni kibaya kwa wote"sio kila kibaya kwako basi ni kibaya kwa mwengine"
Kibaya kwa wengi ni kibaya kwa wote
Keil,
Je ni sawa kwa CHADEMA ambayo ina wabunge viti maalum 30 nchi nzima kuwapangia 2 halmashauri ya Arusha au 2 halmashauri ya Hai? Wametumia vigezo gani kuwapangia hizo halmashauri?
.
Mi nahisi nina tatizo na comment za wanaume hasa hapa JF,hivi hilo la kumnyonya matiti hadi yaishe,halafu anyonyeshe vipi au alichokosea yeye ni adhabu pia kwa mwanae.............whats the point?kuna sehemu nyingine za mwanamke ukiziongelea hivi ni udhalilishaji????wala sitaki matusi,nilishasema inawezekana nina tatizo,mwenye uwezo anisaidie si kunitukana.........
Keil,
Kama huyo mama anafaa kuwakilisha mkoa wa Tanga, je wabunge wa CHADEMA ambao hawakutumia utaratibu wa mkoa wanafaa kuwakilisha makundi gani?
Je ni sawa kwa CHADEMA ambayo ina wabunge viti maalum 30 nchi nzima kuwapangia 2 halmashauri ya Arusha au 2 halmashauri ya Hai? Wametumia vigezo gani kuwapangia hizo halmashauri?
Katiba iko wazi sana, hakuna wabunge viti maalum wanaowakilisha mikoa. Hata ukienda kwenye katiba ya CCM hakuna kitu kama hicho. Wabunge wanaotajwa ni wale wa majimbo na wale wanaoishi kwenye mkoa husika.
Je huyo mama angegombea kupitia kundi la Waremavu ndani ya CCM mungesema akawakilishe walemavu tu? Je angegombea kwenye kundi la vyuo vikuu, mungesema akawakilishi vyuo vikuu tu?
Nakubaliana na wewe kama huyu mama aligombea Tanga ndani ya CCM ina maana yuko karibu na huo mkoa au anaishi huko. Kikawaida hata mimi ningetegemea huyo mama atimize haki yake kama diwani huko Tanga. Lakini hapa kuna complications zingine, huyu mama alikuwa katibu CCM mkoa kabla ya Uchaguzi na anaendelea na kazi hiyo huko huko Arusha. Sheria inamruhusu kuchagua halmashauri ya kutumikia, mnataka achague mkoa ambao itabidi asafiri km karibu 500 kwenda kuhudhuria vikao, why?
CHADEMA ambao hawana utaratibu wa mikoa wana haki ya kuchagua wanakotaka, ila hawa CCM kwasababu wana utaratibu wa mikoa basi wabanwe kwenye mikoa yao. Sheria haiendi hivyo mkuu, ni wote wanaruhusiwa au hakuna anayeruhusiwa.
Pia Mamuya nafikiri sio mbunge. Alichaguliwa kugombea lakini hakupata kwasababu alikuwa chini kwenye list.