Mkuu Polisi,
Haya ni matunda ya viraka na ukurupukaji wa wana siasa kila wanapoona kwamba sasa ni wakati wa kufanya mabadiliko fulani au kwa shinikizo kutoka nje au kwa manufaa ya Chama Tawala.
Pamoja na ukimya wa Katiba kwenye swala la eneo la kufanyia kazi la wabunge wa Viti Maalum, lakini simple logic iko wazi kutokana na utaratibu wa CCM wa kuwachagua wabunge wa Viti Maalum.
Wabunge wa Viti Maalum kupitia CCM wamegawanyika kwenye makundi yafuatayo:
1. Wawakilishi wa Mikoa - hupigiwa kura na wajumbe wa Mkutano wa UWT Mkoa
2. Wawakilishi wa UVCCM - hupigiwa kura na wajumbe Mkutano wa UVCCM wa Taifa
3. Wawakilishi wa walemavu - sijui wanavyopatikana
4. Wawakilishi wa Taasisi za Elimu ya Juu - sijui wanavyopatikana
5. Wawakilishi wa NGOs - niliona walipigiwa kura wa UWT Mkoa wa Dar
Note: Mchakato wa wabunge wa UVCCM, mpambano unaanzia ngazi ya mkoa then wanaenda ngazi ya Taifa.
Mary Chatanda alipigiwa kura na UWT mkoa wa Tanga, na hivyo kimantiki anatakiwa kuwatumikia wapiga kura wake ambao wako mkoa wa Tanga. Matatizo ya akina Mama wa Mkoa wa Arusha hayafanani na matatizo ya akina mama wa Tanga au Manyara. Hatujui aliahidi nini alipokuwa anaomba kura kwa wapiga kura wake ambao wako Mkoa wa Tanga. Je, atashughulikiaje matatizo ya akina mama wa Tanga na ili hali haingii kwenye vikao vya baraza la madiwaji wa Jiji la Tanga? Kwanini alazimishe kuwatumikia akina mama wa Arusha ambao hawakumpigia kura wakati wa uchaguzi?
Pamoja na kwamba Katiba iko kimya, kitendo cha Mary Chatanda kupewa nafasi ya Viti ya Maalum kwa kupigiwa kura na akina mama wa mkoa wa Tanga, maana yake ni kwamba anawakilisha matatizo ya akina mama wa Tanga kuanzia kwenye kata, wilaya, mkoa na hatimaye Taifa.
Mary Chatanda anatakiwa kwenda kuwatumikia akina mama wa Tanga kwa kuwatetea kwenye vikao vya baraza la madiwani huko Tanga. Angekuwa ni mwakilishi wa UVCCM, Walemavu au Taasisi za Elimu ya Juu au NGOs, angekuwa na haki, maana majimbo/maeneo yao ya kazi yamesambaa nchi nzima.
Hoja yangu hapa ni kwamba, Kama Chatanda alipigiwa kura na akina mama wa mkoa wa Tanga, maana yake ni kwamba anawajibika kwa akina mama wa CCM (UWT) mkoa wa Tanga, hapo ndipo ilipo primary responsibility yake.
manne hivi ya Wabunge wa Viti Maalum, wapo wanaowakilisha Akina Mama wewe ulemavu, wapo wanawakilisha NGOs na wapo wanaowakilisha Taasisi za Elimu ya Juu, wapo wanao