CHASO Dar es Salaam: Taarifa kwa umma

Nimejipanga vilivyo. Naisubiri kwa hamu hiyo tarehe 1 Septemba ili kwa pamoja tuseme NO kwa Dikteta uchwara.
 
Mimi ningekuwa Magufuli ningeiba vijana chadema nianze kukitetea chama upya, Magufuli anachoka na kukata Tamaa na ndio maana anajikuta anatoa kauli halafu baadae wasaidizi wake wanasema utani kwa sababu hana msaada wa mawazo akienda kwa mwigulu ndio anakuta scarf ya bendera ya Taifa shingoni muda wote utadhani tai lakini hamna cha maana, akienda kwa nepi ndio huyo yuko kwenye matamasha ya kina wema, mkuu akimwambia vipi? Akikurupuka huko kafungia gazeti, akija kwa february ndio anakuta jamaa kaacha wizara yake yuko kwenye dili za sukari, akienda kwa maghembe ndio unakuta yuko huko nyasa anasifia chakula, akienda kwa mwijage akimuuliza vipi viwanda mwijage anakurupuka na kumwambia leo nimepokea ujumbe wa wawekezaji mzee akiangalia hamna hata dalili ya kiwanda cha dawa ya kunguni kuanzishwa, akija huku vijana wa UVCCM ambao walitakiwa kuwa chachu ndio wananyanganyana hela za kuuza mashamba iringa
 
Na ninyi mmepaniki...tulieni bwana. Tueleze ninyi CHASO ni akina nani...mnatambulika kama nani ndani ya katiba yenu ama ya chama. Mnanguvu gani kikatiba ya kuhakikisha mawazo yenu yanafanyiwa kazi?

Kwa kifupi...hamkutulia wakati wa kuandaa tamko lenu. Na kama mko 'serious' mlitakiwa kuendelea na mikakati badala ya kuangaika na 'bait' ya wapinzani wenu. Au mmeshtuka 'kiberiti' cha gesi?
 
.....

CHASO tunatoa wito kwa wasomi wote nchi nzima kuungana siku ya tarehe 1/9/2016 kupinga ubakwaji huu wa DEMOKRASIA na uvunjaji wa KATIBA ya Nchi unaofanywa na Rais Magufuli na vibaraka wake wote huku wakivitumia vyombo vya dola.

.......
CHASO , chanzo cha fikra bora.

MUNGU IBARIKI TANZANIA
MUNGU IBARIKI CHADEMA.

....
Katiba hiyo hiyo ndiyo hasa inatoa na maelekezo ya nini cha kufanya juu ya rais kuvunja katiba. Je. mmejishughulisha kujua ni maelekezo gani ya katiba ya nchi yanayotoa haki ya kumshughulikia rais anapovunja katiba? Je. Sheria ya vyama vya siasa inazungumza nini juu ya uwezo na taratibu wanazoweza kutumia vyama vya siasa kumshughulikia rais anayevunja katiba? Nina hakika CHASO kama chanzo cha fikra bora mtanipatia majibu mazuri na yanayoeleweka kwa watanzania wote.
 
Hawa CHASO nao wana niudhi sasa... Wao UVCCM wakiropoka na wao mbio kujibu. Kuna ulazima gani wa kuwaweka hao wehu kwenye maandiko yao.
 
Hii habari imeandaliwa na sekeretari au umoja
Mtoa taarifa kamiliaha barua yako kwa jina muhuli pamoja na walioshiriki vinginevyo ni habari ya kuandaliwa na sekretari
Huu ni uandishi wa kijana wa CCM

Uki reffer andiko la kisomi na Makini la CHASO hapo juu na ukafanya Comparison na ulichoandika hapa, utaona tofauti kubwa sana kati ya Vijana wa CHADEMA na CCM.
 
Mimi ningekuwa Magufuli ningeiba vijana chadema nianze kukitetea chama upya, Magufuli anachoka na kukata Tamaa na ndio maana anajikuta anatoa kauli halafu baadae wasaidizi wake wanasema utani kwa sababu hana msaada wa mawazo akienda kwa mwigulu ndio anakuta scarf ya bendera ya Taifa shingoni muda wote utadhani tai lakini hamna cha maana, akienda kwa nepi ndio huyo yuko kwenye matamasha ya kina wema, mkuu akimwambia vipi? Akikurupuka huko kafungia gazeti, akija kwa february ndio anakuta jamaa kaacha wizara yake yuko kwenye dili za sukari, akienda kwa maghembe ndio unakuta yuko huko nyasa anasifia chakula, akienda kwa mwijage akimuuliza vipi viwanda mwijage anakurupuka na kumwambia leo nimepokea ujumbe wa wawekezaji mzee akiangalia hamna hata dalili ya kiwanda cha dawa ya kunguni kuanzishwa, akija huku vijana wa UVCCM ambao walitakiwa kuwa chachu ndio wananyanganyana hela za kuuza mashamba iringa
Mkuu vijana wa CDM wameniambia nikwambie kuwa wao hawawezi kwenda kuwa sehem ya kuhujumu nchi. Wameniambia nikwambie akili zao sio za kushikizwa kwa hiyo hawawezi kwenda ccm. Wameniomba nikwambie usiwadalalie kwa Magu maana hawatamuelewa hata kidogo.Aanze kwanza kuheshimu Katiba ya Nchi.
Ni hayo tu.
 
hawa vijana tuwape hii kazi.
233c4d24c4ebf6396b203636f911b59f.jpg

swissme
 
Uongozi wa CHASO mkoa wa Dar es salaam Leo jumatatu ya tarehe 22/8/2016,unapenda kutoa kauli na msimamo wetu juu ya mambo yafuatayo.

1.Tamko la UVCCM kuhusu kufanya mikutano na maandamano nchi nzima kumpongeza rais kwa utendaji wake,CHASO tunaona tamko la UVCCM kama kichekesho na ndoto zisizoweza kutimia kwa sababu CCM hawana vijana wa kufanya maandamano nchi nzima na hawana historia hiyo,na hii inasababishwa na CCM kutokua na nguvu ya ushawishi kwa vijana hivo kiufupi maandamano hayo hayajawai kuwepo na hayawezi kuepo.

Pia CHASO tunalishangaa genge hili lisilokua na ushawishi wala uungwaji mkono toka kwa vijana kuanza kudandia hoja na mipango ya CHADEMA ya kufanya maandamano na mikutano ya hadhara nchi nzima,Hii ni hatari sana kwao maana wasishangae watakapopigwa bakora mitaani kutokana na hali ngumu ya maisha kwa watanzania,hivyo "wasiwajaribu watanzania maana hawatakubali kujaribiwa"

2.Ushiriki wa Wana CHASO katika operation UKUTA kuanzia September 1.

Sheria ya vyama vya siasa Na.5 ya 1992.KANUNI ZA MAADILI YA VYAMA VYA SIASA ZA MWAKA 2007.

Sehemu ya pili.

Haki ya chama.
Lakini pia sehemu ya tatu, 5.wajibu wa chama (e) na (f).CHASO kwa sheria hiyo tunapenda kuendelea na msimamo wetu wa kuunga mkono operation hii kwa nguvu zetu zote na hatutarudi nyuma katika movement hii,tutaidai haki hii hadharani bila kificho,na uongozi unawasihi wanachaso popote mlipo kufika katika ofisi za chama zilizopo karibu na kutoa ushirikiano.

CHASO tunatoa wito kwa wasomi wote nchi nzima kuungana siku ya tarehe 1/9/2016 kupinga ubakwaji huu wa DEMOKRASIA na uvunjaji wa KATIBA ya Nchi unaofanywa na Rais Magufuli na vibaraka wake wote huku wakivitumia vyombo vya dola.

Tunawataka UVCCM kuzungumzia hali ngumu ya maisha kwa sasa mitaani,Wanafunzi kutopewa hela za mafunzo kwa vitendo mpaka sasa,Bei ya Sukari kuwa juu,Biashara kudorora kutokana hali ngumu ya maisha,Wamachinga na Bodaboda kuendelea kuteseka ndani ya nchi yao,Serikali kushindwa kuajiri wala kutengeneza vyanzo vya ajira.
Tunawataka UVCCM kutuonesha ni KIWANDA gani mpaka leo imekwisha zinduliwa na Mh. Rais kama ilivyo kipaumbele chake.

Mwisho.
Tunawapongeza Watanzania wote wenye mapenzi mema na nchi yetu bila kujali itikadi zao, dini wala ukanda kwa kuendelea kuunga mkono Operation UKUTA kwa mustakabali mwema wa nchi yetu.

Tunatoa wito kwa vyombo vyetu vya Dola kuona umuhimu wa Operation UKUTA,wao wanajua umuhimu wa kuheshimu utawala wa Katiba na Sheria,pia wameapa kuilinda KATIBA ya nchi. Tunaomba vyombo vya Dola kutoa ushirikiano ili kufanikisha Operation UKUTA.

AHSANTENI

CHASO , chanzo cha fikra bora.

MUNGU IBARIKI TANZANIA
MUNGU IBARIKI CHADEMA.

TUKUTANE SEPTEMBER 1, 2016#UKUTA

Mere kicks of a dying horse (in articulo mortis) at the point of death
upload_2016-8-23_15-46-6.png
 
huu uzi ni muhimu kuusave kwa manufaa ya kizazi kijacho waje waone chama makini kilivyokuwa na hazina ya vijana.
 
CHASO wamepikwa wakaandaliwa kuwa viongozi wanajuwa shida za wananchi sio hao vijana wa UVCCM wanasoma tamko huku wakitetemekea kujikomba kwa dikteta uchwara anarudisha nchi nyuma miaka hamsini
 
CHASO wamepikwa wakaandaliwa kuwa viongozi wanajuwa shida za wananchi sio hao vijana wa UVCCM wanasoma tamko huku wakitetemekea kujikomba kwa dikteta uchwara anarudisha nchi nyuma miaka hamsini
Umenena vema mkuu. Vijana hawa huwa wapo smart sana. Magufuli aache kuwakandamiza kisa wapo upinzani. Hawa wanaweza kuja na mawazo mazuri sana ya kujenga nchi.
 
ktk uwandish vijana wa tz nawapongeza bt katika mapambano ya uso kwa uso watu watajifungia vyumban mwao
 
Back
Top Bottom