Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 17,026
- 20,511
Majaji katika mahakama maalum ya Umoja wa Mataifa mjini The Hague wametupilia mbali rufaa ya Kiongozi wa zamani wa Liberia Charles Taylor na kuendelea na adhabu ya kifungo cha miaka 50 jela. Taylor alikuwa amekata rufaa kupinga hukumu dhidi yake ambapo anatuhumiwa kuwasaidia waasi wa Sierra Leone ili apewe almasi. Mahakama hiyo ni maalum kwa ajili ya kushughulikia kesi za Sierra Leone. Jaji wa mahakama ya rufaa George King amesema vitendo vya Taylor na mienendo yake sio tu viliwaumiza waathiriwa na jamaa zao bali pia vilichochea mzozo uliokuwa kitisho kwa amani ya kimataifa na usalama katika kanda ya magharibi mwa Afrika.Uamuzi huo wa mahakama ya rufaa unafikisha ukingoni kesi hiyo dhidi ya Taylor ambayo imedumu kwa miaka saba.
Mtazamo wangu:
Hii ni salamu tosha kwa viongozi wa ccm na wale wote wanaoendeleza uhalifu dhidi ya binadamu na kukandamiza wa haki za Watanzania!
Mtazamo wangu:
Hii ni salamu tosha kwa viongozi wa ccm na wale wote wanaoendeleza uhalifu dhidi ya binadamu na kukandamiza wa haki za Watanzania!