Lituye
JF-Expert Member
- Dec 27, 2015
- 1,864
- 5,695
Aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani ya nchi ndugu Kitwanga amelieleza gazeti la Majira leo tarehe 5 Julai kuwa wauza unga ndio walio muondoa katika nafasi yake ya uwaziri na taarifa zilizotolewa na ikulu ni uongo mtupu.
Hii sio kauli ya kawaida, ni nzito na ya kuogofya inatia Shaka pia kujua hao wauza unga wenye mamlaka makubwa namna hii ni akina nani? Kwa hiyo wamemshugulikia yeye ili biashara iendelee kushamiri hapa nchini?
Taarifa Kama hii ni fedheha kwa Mtukufu na mamlaka yake. Ingekuwa kama kule Marekani Kitwanga angeitwa na kuhojiwa na shirika la ujasusi la F.B.I ili atoe taarifa muhimu juu ya mtandao huo hatari unaoangamiza taifa wakati yeye kumbe anawajua vizuri.
Mimi naona Kitwanga anayo mengi ya moyoni toka huko Israel alikoenda kupata mafunuo ya kimungu.