Chapel of all Saints in the Kutná Czech | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chapel of all Saints in the Kutná Czech

Discussion in 'International Forum' started by X-PASTER, Apr 30, 2009.

 1. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #1
  Apr 30, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  The simple chapel exterior

  Stepping inside will give you a bit of a creepy feeling especially seeing the piles of bones, Czech wood carver František Rint, with the skeletal art work and arrangement particularly the elaborate Schwarzenberg coat-of-arms.

  [​IMG] 1.jpg
  This church is small but 1000 years old. This church differentiates others as it is not decorated by wood, stone, marble or any other artificial materials but with Muslims' bones!!!!

  [​IMG] 2.jpg
  The story starts when the Pope Hanry set his journey to Qudus during the holy war in the year 1218 he ordered crusaders to bring the bones of people were killed in the war in order to decorate the church.

  3.jpg
  In the year 1318 they redecorated the Church with new bones of around 300,000. In 1870 Sculptors reconstructed the decoration with 40,000 bones to look the church more attractive and beautiful.

  [​IMG] 4.jpg

  At present this church is one of the famous church in the world not for its ancientness but for its decoration with the bones of people.
  [​IMG] 5.jpg

  6.jpg


  [ame="http://www.youtube.com/watch?v=1dDr7EN_SR4"]YouTube - Kutná Hora bone church[/ame]


  This direct association with the holy land led to the graveyard becoming a sought after burial site among the aristocracy of Central Europe. At the time of the thirty years’ war in the 17th century, the number of burials outgrew the space available, the older remains began to be exhumed and stored in the chapel, and it’s estimated that the chapel now contains the bones of up to 40,000 people.
   
  Last edited: Apr 30, 2009
 2. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #2
  Apr 30, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  What is it? Put your abstract together na sema nini unataka kusema au tangaza.
   
 3. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #3
  Apr 30, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Eeeh! pole pole mwalimu... mbona jazba... Mbona hiyo ni moja ya sanaa tu... wenyewe wanaita mapambo ya kisanii wewe unakurupuka... wapi na wapi kaka!
   
 4. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #4
  Apr 30, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Wenyewe akina nani? Mbona unakwepesha maneno? Sema kiuwazi ni nini unataka kutangaza au sema.
   
 5. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #5
  Apr 30, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  wenye kanisa lao kijiji cha Kutná hukoooo Czech, au na wewe ni mlei ktk hili kanisa!?
   
 6. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #6
  Apr 30, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  X-Paster,

  Asante kwa kunirudisha Czeck tena. Kutokana na maelezo yako naona kabisa hujawahi kufika Czech na hawa watu huwafahamu. Mie nilibahatika kukaa pale Praha miaka hiyoo na sikuwa mbali sana na daraja la Charles ambalo inasemekana walijenga kwa kutumia Mayai kama Bonding materials. Czeck ni nchi nzuri sana kufika kama mtalii. Wale watu ni wagumu sana kuwaelewa harakaharaka na labda mtu mwenyeji kusaidie, vinginevyo utaelewa kivyako.

  Nikiwa pale nilibahatika kufika katika jumba alilokuwa anakaa mtawala wa Czeck aitwaye "Archduke Franz Ferdinand of Austria". Ukitaka maelezo soma Wikipedia. Huyu alienda Sarayevo na kufika huko Waserbia wakamuuwa na hiyo ikawa ni SABABU ya kuanzisha vita ya kwanza ya dunia. Ukifika kwenye jumba lake liitwalo Konopiste chateau =gonga hapa(Život v Cizine), utaona kuwa huyu bwana katika maisha yake aliuwa ndege na wanyama zaidi ya laki tatu. Na baadhi ya vichwa vya ndege na wanyama vimebandikwa ukutani.

  Waczeck hawaamini dini kabisa. Ndiyo maana makanisa mengi huko yamebadilishwa kuwa vitu vya kushangaza sana si kama wewe tu Muislam ila hata Wakristo. Na hii ni tabia yao. Dini mwanzo waliletewa na Wa-austria na baadaye wakafanya mapinduzi na kuwafukuza wadini wote na moja ya kanisa lililofukuzwa ni Moravian Church (mimi ni member) ambalo lilianzia Moravia Czeck na ikabidi wahamie Ujeruman hadi leo hii.
  Kuna Makanisa mengi sana ambayo yamegeuzwa kuwa vivutio vya utalii na ukisikia mambo yaliyofanyika sehemu hiyo basi huna hamu. Mwenye niliona Makanisa mengi tu na utashangaa hamna waumini siku za jumapili ila Watalii na makamera yao. Na hii nchi ina watalii wengi saana. Inasemekana kuwa asilimia 80 ya watu wanaoishi Capital City Praha, wanafanya kazi kwenye sekta ya utalii. Jamaa ni mfano wa kuigwa.

  Ukorofi mwingine wa hawa jamaa ni kuongelea openly habari TABU kama sex. Kwa mfano siku moja nilisikia jamaa wakiongelea kuwa "Kulikuwa na onyesho la thieta ndani ya kanisa la zamani. Jamaa wanapeana maneno wee na mwisho wake dada mmoja anampa laana mwenzio kwamba 'nakuombea hadi unakufa, usije ukaliwa tigo'......." Sasa maneno kama haya ndani ya EX-Kanisa, kwa kweli utaishiwa nguvu.

  Hilo kanisa ni kweli lipo na lipo kwelie mji uliousema. Ila vituko vya ANTI DINI kwa Czeck vipo vingi sana. Wana majengo mengi sana ya miaka 700, 800, 1000 etc. Maisha ya Czeck kwa ujumla kwa watalii ni rahisi sana kulinganisha na nchi nyingine za EU. I wish Tanzania tungelienda kusomea kwa hawa jamaa jinsi ya ku-oparate katika utalii. Kama kuna safari ya masaa sita, ukinunua ticket basi unaanzia kwenye hiyo castle na hapo utaona watu kibaooooo, na mwishoni mnapelekwa kwenye kiwanda cha bia ambacho hawauzi bia zaidi ya kiwandani (Konopiste Chateau & Velké Popovice Brewery TOUR). Hiyo ni moja ya vivutio na vivutio hivyo vipo vingi sana na ni hela yako tu. Unalipa na kama waishi mjini basi next day wanakufuata nyumbani na mkirudi wanakurudisha hadi home. Very well organised.

  Hivyo X-Paster, jitahidi ufike huko siku moja. Ila wale wajinga hawamind dini yoyote. Uwe Muislam, Mkristo, Myahudi ect they dont give *****. Hapo hata Mrusi alitoka nje. Hapendwi mtu zaidi yao wenyewe. Hakuna cha kuiga vya watu kama sisi. Wale hata Nyimbo zote maarufu wanazibadili na kuziimba kwa Kiczeck. Majina yote yanabadislishwa. Sijui Obama wamemuitaje wajinga wale........ Kila la kheri.
   
 7. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #7
  Apr 30, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Umejuwaje kuwa sijafika huko Czeck!? Na bado mwenyewe unakubali kuwa
  nadhani hii taarifa yako inamfaa sana masimba. Maana yeye aliniuliza
  Nikamjibu kwa kifupi. Nashukuru ndugu umerahisisha kazi.
  thanx
   
 8. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #8
  Apr 30, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Hayo maandishi niliyoyawekea BOLD, yalinipa wasiwasi kama kweli ulifika. Na hata kama ulifika basi hukuelewa. Ndiyo maana nikakuambia kuwa makanisa mengi ya Czeck ni kivutio cha utalii. Sasa ungelijua hilo, ungeligundua kuwa kanisa hilo si wanakijiji ila linakuwa chini ya Czeck Republic au hata UNESCO/Czeck Republic.

  Hata ukiwa kwenye lile Castle (Prague Castle/Pražský hrad) alilokuwa akiishi Václav Havel (Ex-President), nyuma yake kuna kanisa kubwa sana. Na ukitumia Google unaweza hata kuliona na wameliweka katia 3D. Kanisa hilo wanaliita St. Vitus Cathedral (angalia Wikipedia), hili nalo halina wenyewe na wala misa ndani haifanyiki. Hapo kila siku iendayo kwa Mungu kuna watalii wengi sana wanaingia. Hata ukiangalia Google earth utaona kuwa kuna watu wengi sana na wamepiga picha nyingi sana.

  Anyway, uwe umefika au hujafika, si muhimu hapa. Nilitaka tu kuonyesha jinsi Waczeck walivyochangamka katika utalii kwamba hata vitu vya aibu na kusikitisha, wao wanakusanya pesa tu. Siyo kama sisi Tanzania, ufuska na ushoga upo kibao na watu wanaingiza hela kibao na serikali inajifanya hamna na hivyo haichukui kodi. Kama ulishafika, ni poa sana. Na kama bado na siku moja ukawa nchi za jirani, basi jitahidi kwenda hapo na nunua trip za kwenda kutembea sehemu na watakuuliza hata lugha na hapo mnapata kiongozi anayeongea Kiingereza. Mie nilikuwa nawatumia sana Martin tour ambao ukiwa pale mjini, wana vituo vingi tu vya kuuzia ticket.
  Again, asante kwa kutuma.
   
Loading...