Chanzo ni wavulana na sio wanaume.

Chanzo ni wavulana na sio wanaume.

madeinmusoma

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2014
Posts
326
Reaction score
391
-Maisha ya mahusiano ni magumu Sana kuliko hata maisha ya ndoa Boys wengi huwa wanachelewa sana kufanya maamuzi sahihi katika wakati sahihi na kuwakosa watu muhimu kwenye ndoa zao.

-Brother ukichelewa Kwa msichana anayekupenda kwa dhati utalia na utatoa machozi ya damu ukishachelewa tu moyo wa wanawake huwa unatoka na ukitoka kuurudisha inatakiwa usubiri sana mpaka miujiza ya Mungu imurudie.

-Ukiona Dada ametendwa na mwanaume Itafika kipindi katika maisha yake ambapo atagundua kuwa haukutakiwa kuwa sehemu ya maisha yake. Ni kipindi ambacho atapata moyo wa ujasiri wa kutokukusubiri na kukunyenyekea tena. Hatakusubiri tena umpigie simu au kuchukua simu yake na kukupigia.

-Hatakaa tena kusubiri ufafanuzi wako wa uongo na excuses zako za uongo kwa sababu atagundua kuwa haustahili muda wake hata kidogo. Ndio atalia sana kwa kuwa alikupenda toka moyoni, alijihakikishiakuwa wewe ndio mtarajiwa kwake na ndio baby wako namba moja. Atabeba hisia zake zilizojeruhiwa mbali na wewe.

-Kidogo kidogo ataanza kusahau na kuishi maisha yake japo kwa tabu mno. Atakuja kumpata mtu anayempenda. Atamfanya asahau maumivu yote ya huko nyuma uliyompa. Ikifika kipindi hiko tafadhali, usimfuate na kuanza kuleta usumbufu eti unataka mrudiane. Ulipewa nafasi ukaichezea basi atleast muache na mwenzako afurahie maisha upande mwingine.

-Ambalo hukujua ni kwamba kisichomuua mtu, siku zote humkomaza kiaskari. Kuna wadada wajenda wengi sana wahanga wa mahusiano kaka ukichelewa jikatae mapema kuliko kwenda kuongeza maumuzi yake. Yaweza kuwa tatizo lake ni kukupenda wewe na wewe ukajua unapendwa ukaringa Kama Mange Kimambi.

-Haya yote yanaweza kusababishwa na njia ambayo sio sahihi ambayo watu waliingia kwenye mahusiano yaweza kuwa mwanamke alikulupuka kuingia kwenye mapenzi na wewe ukajua lazima utakuwa boss na ukiwa boss kwenye mapenzi imekula kwako. Kuna mfano wa kweli ulitokea kwa rafiki yangu wa karibu.

-Mfano wake ni kwamba Yocma alimpenda sana Hilda na alitamani awe mpenzi wake ila alitafuta kila mbinu za kumpata. Yocma alipata mawasiliano ya Hilda na wakawa wanawasiliana baadae Hilda alimuelewa Sana yocma akahic ni mwanaume bora kwenye maisha yake.

-Kwa kuwa wadada ni waoga kumwambia mwanaume ila Hilda alionesha hisia zake kwa yocma. Ila yocma naye alijifanya kuvunga Kwanzaa ili asionekane mtu mbaya kwa Hilda maana alikuwa anampenda sana baadae uzalendo ukamshinda Hilda akamwambia yocma anampenda na anahitaji kuwa naye kwenye maisha yake.

-Yocma alikubali kwa moyo mmoja kwa sababu naye lilikuwa lengo lake kumbe yocma ameingia akiwa na makandokando mengi alimchukulia poa Hilda ikawa inapita hata siku mbili tatu bila mawasiliano na et ni wapenzi baadae Hilda ikabidi amwambie yocma mapenzi yao yaishie hapo tena kwa kusema alimpenda sana ila yy alimchukulia poa tu..

-Baadae yocma akawa analia ikitaka warudiane na hilda kumbe yocma alikuwa amechelewa na moyo wa Hilda haupo tena kwa yocma .Huu ni mfano wa kwel unavyoonyesha boys mlivyo wakatili kwenye mahusiano

-Kaka angu, rfk yangu Kuwa na Busara hata kidogo ukipendwa pendeka basi, thamini hisia za mwenzako. Mapenzi yanauma sana unakuta janaume linapendwa kwa dhati lenyewe liko serious Kama mgambo wa jiji.

-Mapenzi hayako hivyo thamini upendo wa mtu Kama humpendi mwambia mwanzoni wakati hajahamisha mabegi ya moyo wake kuja kwenye moyo wako. Badilika kaka, badilika ndg yangu badilika sasa wanawake wameumbwa kupenda ila upendo ukitoka hata ulete vifaru vya jeshi hautarudi.



Repost
@yossima
 
Hii barua imenishinda kuisoma, alieisoma anipe summary tafadhari..[emoji120][emoji120]
 
Back
Top Bottom