Chanzo cha upepo

Cascos

New Member
Oct 13, 2012
0
198
Habarini wana jamvi,

Nimekuwa nikifikiria hili jambo kwa muda lakini nimekosa jibu la kunifanya niamini nnachosikia, nikaona sio mbaya ku share nanyi jamvini huenda kuna mtu ana uelewa wa haya mambo.

Hivi chanzo cha upepo ni nini?!
 
Una maanisha movement ya hewa angani kutoka sehemu moja kwenda nyingine
 
Upepo ni hewa inayojongea kutoka katika sehemu/eneo lenye makndamizo mkubwa wa hewa kuelekea kwenye sehemu yenye mkandamizo mdogo wa hewa.

Hewa hujumuisha, oksijen , hewa ya ukaa, naitrojen n.k

Kuna kitu kinaitwa Pressure Gradient ambacho Mara nyingi husababishwa na tofauti ya Temperature katika eneo moja na jingine hali ambayo husababisha Sehemu moja kuwa na mgandamizo mkubwa kushinda eneo jingine.

Sehemu yenye high temperature inakuwa na low pressure wakati eneo yenye low temperature huwa na high pressure.
 
Kwahiyo upepo unasababishwa na nini?!
 
Ngoja nikumbuke Geography yangu ya form two niliyofundishwa na Mrs. Mbwiluga.

Dunia ni sayari mojawapo iliyopendelewa sana kwa kuwa na tabaka nene la hewa. Katika tabaka hili ndiyo wamo akina Hydrogen, Oksijeni, Nitrogen na wengineo. Kwa hali hiyo, na kulingana na mwl. wangu kipenzi wa Jiografia Mrs. Mbwiluga, HEWA IPO TU KATIKA USO NA ANGA LA DUNIA INAELEA.

Katika hali ya kawaida hewa hii inapaswa kuwa tuliii imetulia (kama chumbani mwako ikiwa hujachochea feni au kiyoyozi) lakini mara nyingi haiwi hivyo kwa sababu dunia yetu ni hai: kuna majira, mawimbi ya bahari, hali ya hewa inayobadilika badilika mf. joto kupanda na kushuka, mgandamizo wa hewa (pressure) kubadilika badilika na kutofautiana kutoka sehemu moja kwenda nyingine n.k. Chanzo cha yote haya ni nishati inayotokana na jua.

Kulingana na Mrs. Mbwiluga, hali ya uwepo wa joto tofauti kutoka sehemu moja kwenda nyingine (mf. bahari vs nchi kavu, milima vs mabonde, msituni vs jangwani, kanda tofauti za hali joto) husababisha pia tofauti katika mgandamizo wa hewa. Tofauti hii katika mgandamizo wa hewa ndiyo husababisha mjongeo wa hewa kutoka eneo moja kwenda sehemu nyingine. Mjongeo huu wa hewa unapotokea ndiyo tunaita upepo; na kwa kawaida upepo huvuma kutoka sehemu yenye mgandamizo mkubwa wa hewa kwenda kwenye sehemu yenye mgandamizo mdogo; na kutegemea na hali ya hewa ya siku hiyo pamoja na natural barriers kama milima, spidi yake inaweza kutofautiana kutoka eneo moja hadi jingine.

Kwa kifupi hivyo ndivyo Mrs. Mbwiluga alivyonifundisha Jiografia form two kuhusu uwepo wa upepo katika sayari yetu hii nzuri iitwayo dunia japo tunaiharibu kwa kasi ya kutisha. Thanks sana mwalimu wangu mpendwa wa Jiografia Mrs. Mbwiluga. Nitakukumbuka na kukuenzi daima!
 
Upepo ni ule msukumo wa hewa kutoka sehemu moja kwenda nyingine

Aidha msukumo huo unaweza kuwa kwa ajili ya ukinzani baina ya kitu kinacho jongea, kama ndege, gar au boti.

Upepo unaweza sababishwa na mjengeo wa hewa kutoka mkandamizo mkali kwenda mgandamizo mdogo wa hewa...

Mwisho pia hizo pepo zinatofautiana kuna zile za kusi, kaskazi nk.matumizi yake ni kusafirisha kama kule baharini.madhara yake ndo kama hayo ya catrina, matheu nk.

Ni hayo kwa mujibu wa masomo yangu ya maarifa ya jamii darasa la saba c
 
MCHANGO WANGU (MADE SIMPLE)
Atmosphere (anga ama uso wa dunia) umejazwa na hewa (gas) ambayo ipo stationary kabisa (at room temperature) hewa hiyo ni Nitrogen, Oxygen na Noble gases (Hydrogen, hellium etc). Upepo ni hewa inayo tembea.
Naona wote mmejaribu kuelezea lakini sababu kubwa inayo sababisha kuwepo kwa upepo ni mwanga wa jua (Solar energy ) kivipi?
Jua linapopiga katika uso wa dunia linatengeneza joto kutokana na baadhi ya mionzi inayo sharabiwa ardhini na majini japo mingine inakuwa reflected. Kwa kawaida maji ya bahari huchelewa kupoteza joto haraka kuliko ardhini hivyo basi wakati wa usiku kufanya bahari kuwa na joto wakati ardhi huwa ni yabaridi hivyo kutokea kuwa upande wa ardhi huwa na mgandamizo mkubwa wa hewa (high pressure) hivyo hewa hutoka nchi kavu na kuelekea baharini ili kucover ile low pressure iliyopo kule.
Wakati wa mchana bahari inakuwa kwa kiasiflani imesha poa japo sasa inaanza kugain joto taratibu na ardhi inakuwa imepata joto kwa kiasi kikubwa kutokana na mionzi ya jua inayopiga ardhini. Hivyo hewa sasa katika mfumo wa upepo husafiri kutoka baharini ili kuja kupooza joto kali lilioko ardhini.
Kwahiyo kwa kifupi ni kuwa upepo ni hewa inayo tembea kutoka eneo lenye mgandamizo mkubwa (high pressure) kwenda kwenye eneo lenye mgandamizo mdogo (low pressure). Au kutoka sehemu yenye baridi kwenda kwenye sehemu yenye joto.
Ni kama vile gas inayowekwa kwenye mitungi mule ndani kunakuwa na high pressure na low temperature hivyo unapofungua koki utaruhusu gesi itoke automatically kwenda kwenye eneo lenye low pressure yaani nje ya mtungi.
Nadhani kwa kiasi fulani nimeeleweka. Ahsante
 
Umenikumbusha Jiografia darasa la sita mkuu: Upepo Mwanana wa nchi kavu na Upepo Mwanana wa Baharini...Nilisahau kulisema waziwazi hili katika comment yangu hapo juu (comment #15). Nadhani tumejaribu kueleza kwa lugha rahisi kabisa na inayoeleweka kuhusu upepo ndiyo maana hata waliokuwa wanaulizia huko nyuma wamepotea. Asante kwa elimu ya bure mkuu.
 
Upepo ni hewa inayojongea kutoka katika sehemu/eneo lenye makndamizo mkubwa wa hewa kuelekea kwenye sehemu yenye mkandamizo mdogo wa hewa.

Hewa hujumuisha, oksijen , hewa ya ukaa, naitrojen n.k

Kuna kitu kinaitwa Pressure Gradient ambacho Mara nyingi husababishwa na tofauti ya Temperature katika eneo moja na jingine hali ambayo husababisha Sehemu moja kuwa na mgandamizo mkubwa kushinda eneo jingine.

Sehemu yenye high temperature inakuwa na low pressure wakati eneo yenye low temperature huwa na high pressure.
Hivi pressure si directly proposional na temperature
 
Upepo ni hewa inayojongea kutoka katika sehemu/eneo lenye makndamizo mkubwa wa hewa kuelekea kwenye sehemu yenye mkandamizo mdogo wa hewa.

Hewa hujumuisha, oksijen , hewa ya ukaa, naitrojen n.k

Kuna kitu kinaitwa Pressure Gradient ambacho Mara nyingi husababishwa na tofauti ya Temperature katika eneo moja na jingine hali ambayo husababisha Sehemu moja kuwa na mgandamizo mkubwa kushinda eneo jingine.

Sehemu yenye high temperature inakuwa na low pressure wakati eneo yenye low temperature huwa na high pressure.
Unadhan umeelewa swali?
 
Back
Top Bottom