Chanzo cha Uhai

Chanzo cha Uhai

Ukisema unaenda kuoga inafahamika kua ni maji, lakini ukisema unaenda kuoga audio yenye yenye kutoa sauti ya maji unakua umeacha shaka

Ukiniambia kua kwani maji unavyoyaoga hayatoi sauti au mlio nikakuambia ndiyo yanatoa sauti, halafu wewe useme sasa kua umetumia audio yenye kelele za maji kuogea hivyo uko sawa na yule atakayetumia maji kuoga, kwasababu akioga yatatoa sauti kama yako iliyo kwenye redio yako

Hapo ukisema udongo wenye sauti hauna tofauti na huu mfinyanzi nao ujua mimi, huna tofauti na kuoga audio yenye kelele za maji


Sent using unknown device
Mfano wangu wa maji,umekomea kwenye maji tu,wala hukutakiwa kuleta mambo ya "audio" sababu unakosea zaidi.

Mfano wangu umejikita katika maneno yenye kujitosheleza na endapo ukiongeza maneno kwenye maneno yenye kujitosheleza utaonekana kituko.

Natilia mkazo tu,achilia mbali utofauti wa udongo ule na huu uliopo,lakini hakuna udongo usio toa sauti. Kuna wakati ukifikiria unatakiwa ufikirie hasa,ukikurupuka kama ufanyavyo wewe lazima ukosee.

Kuna maneno ya kutilia mkazo na kutofautisha mmoja kwa mwengine. Mfano nikisema "Walikuja vijana sita na Zurri akiwemo". Hapa haimaanishi kama Zurri sio mtu,bali katika lugha ni katika kuimakinisha taarifa,kuitofautish na kuiweka sawa taarifa.

Nipo ....
 
Mfano wangu wa maji,umekomea kwenye maji tu,wala hukutakiwa kuleta mambo ya "audio" sababu unakosea zaidi.

Mfano wangu umejikita katika maneno yenye kujitosheleza na endapo ukiongeza maneno kwenye maneno yenye kujitosheleza utaonekana kituko.

Natilia mkazo tu,achilia mbali utofauti wa udongo ule na huu uliopo,lakini hakuna udongo usio toa sauti. Kuna wakati ukifikiria unatakiwa ufikirie hasa,ukikurupuka kama ufanyavyo wewe lazima ukosee.

Kuna maneno ya kutilia mkazo na kutofautisha mmoja kwa mwengine. Mfano nikisema "Walikuja vijana sita na Zurri akiwemo". Hapa haimaanishi kama Zurri sio mtu,bali katika lugha ni katika kuimakinisha taarifa,kuitofautish na kuiweka sawa taarifa.

Nipo ....
Hata aya iliyosema udongo wenye sauti, ilikomea hapo hapo hukutakiwa kuongeza yako ya kusema udongo ukipigwa pigwa ndio unatoa sauti sababu unakosea zaidi

Sent using unknown device
 
Hata aya iliyosema udongo wenye sauti, ilikomea hapo hapo hukutakiwa kuongeza yako ya kusema udongo ukipigwa pigwa ndio unatoa sauti sababu unakosea zaidi

Sent using unknown device

Kuna la ziada la kuniambia ?

Tujikite kwenye mada ya mdau sasa. Mimi kazi yangu kwako imeisha.

Nipo ...
 
Habari wana- JF!
Karibu katika makala fupi kuhusu "Chanzo cha Uhai"

CHANZO CHA UHAI

Wanasayansi wengi wanaoamini mageuzi watakuambia kwamba uhai ulianza mabilioni ya miaka iliyopita kwenye ukingo wa kidimbwi cha kale kilichojaa maji wakati wa kupwa au katika sehemu za chini ya bahari. Wao huhisi kwamba katika maeneo yasiyojulikana kama hayo, kemikali zilijikusanya na kuwa vitu vinavyofanana na mapovu,vikafanyiza molekuli tata, na kuanza kujigawanya-gawanya. Wanaamini kwamba uhai wote duniani ulijitokeza wenyewe tu kutokana na chembe “sahili,” moja au zaidi.

Wanasayansi wengine wanaoheshimika ambao pia wanaunga mkono mageuzi hawakubaliani na wazo hilo. Wanakisia kwamba chembe za kwanza au angalau sehemu zake kuu zilikuja duniani kutoka anga la nje.

Licha ya jitihada zao nyingi, wanasayansi hawajaweza kuthibitisha kwamba uhai unaweza kutokea ghafla kutokana na molekuli zinazodhaniwa zilitokeza uhai. Katika mwaka wa 2008, Alexandre Meinesz, Profesa wa Biolijia, alizungumzia utata huo. Alisema kwamba kwa zaidi ya miaka 50 iliyopita, “hakuna uthibitisho wowote uliopatikana kupitia majaribio yaliyofanywa unaounga mkono nadharia ya kwamba uhai ulitokea ghafla Duniani kutokana na molekuli fulani, wala hakuna maendeleo ya kisayansi yanayoweza kuthibitisha hilo.”

Siku zote uhai hutokana na uhai ambao tayari upo. Watafiti wamegundua kwamba ili chembe iendelee kuwa hai, angalau aina tatu tofauti za molekuli tata lazima zifanye kazi pamoja - DNA au deoksiribonyuklia asidi, RNA( ribonucleic acid), na protini. Leo, ni wanasayansi wachache wanaoweza kudai kwamba chembe kamili iliyo hai iliyojitokeza yenyewe kutokana na mchanganyiko wa kemikali zisizo hai.

Wanasayansi wengi huhisi kwamba huenda uhai ulijitokeza wenyewe kwa sababu ya jaribio fulani lililofanywa kwa mara ya kwanza mwaka 1953. Mwaka huo Stanley L. Miller aliweza kutengeneza asidi - amino, kemikali za msingi zinazofanyiza protini,kwa kupitisha nguvu za umeme ndani ya mchanganyiko wa gesi zilizodhaniwa kuwa zingewakilisha anga la Dunia. Toka wakati huo, asidi - amino zimepatikana pia katika vimondo. Ugunduzi huu haumaanishi kwamba kemikali za msingi za uhai zinaweza kujitokeza zenyewe.

Robert Shapiro, aliyekuwa profesa wa kemia katika Chuo Kikuu cha New York, anasema, “ Baadhi ya waandishi wameamini kwamba kemikali za msingi za uhai zinaweza kutengenezwa kwa urahisi kwa kutumia majaribio kama yale ya Miller na kwamba zinapatikana katika vimondo. Hata hivyo sivyo ilivyo.” * 1

Fikiria molekuli ya RNA. Imefanyizwa na molekuli ndogo zinazoitwa nukliotidi. Nukliotidi ni aina tofauti ya molekuli na ni tata zaidi kidogo kuliko asidi - amino. Shapiro anasema kwamba “ hakuna nukliotidi za aina yoyote zinazoripotiwa kuwa zilitokana na majaribio yanayohusu umeme wala katika uchunguzi wa vimondo. Pia anasema kwamba uwezekano wa molekuli kujifanyiza bila mpangilio maalum na kujikusanya toka kemikali nyingi za msingi “ ni mdogo sana hivi kwamba hata kama ungetokea mahali popote katika ulimwengu unaonekana ungeonwa bahati.

Mtafiti Hubert P. Yockey, anayeunga mkono fundisho la mageuzi ana maelezo zaidi. Anasema: “Haiwezekani kwamba chanzo cha uhai ni ‘protini tu.’”* 2 RNA inahitajika kutengeneza protini, hata hivyo, protini zinahusika katika utengenezaji wa RNA.

Je, kuna uwezekano wowote kwamba protini na molekuli ya RNA kutokea mahali pamoja kwa wakati uleule na kufanyiza uhai unaoweza kutokeza chembe ambazo zinaweza kuzaa na kuendeleza uhai?

Yaelekea uwezekano wa jambo hilo kujitokeza lenyewe, kukiwa na mchanganyiko usio na mpangilio maalumu wa protini na RNA, ni mdogo sana, anasema Dkt. Carol Creland ; mshiriki wa NASA ( National Aeronautics and Space Administration's Astrobilogy Institute).








1* Profesa Shapiro haamini kwamba uhai ulitokana na Muumba. Anaamini kuwa uhai ulijitokeza wenyewe kwa njia fulani ambayo bado haijaeleweka. Mwaka wa 2009 wanasayansi katika Chuo Kikuu cha Manchester, Uingereza,waliripoti kwamba wametengeneza nukliotidi katika maabara yao. Hata hivyo, Shapiro anasema kwamba viambatano vyao “bila shaka havifikii viwango vyangu vinavyokubalika vya kutengeneza RNA.”

2* Dkt. Cleland haamini masimulizi kuhusu uumbaji wa Mungu . Anaamini kwamba uhai ulijitokeza wenyewe katika njia fulani ambayo bado haijaeleweka vizuri.

UKWELI KUHUSU UCHUNGUZI WA KISAYANSI NA UHAI (UUMBAJI)


Ukweli wa mambo: Utafiti wote wa kisayansi umeonyesha kwamba uhai hauwezi kujitokeza wenyewe kutokana na kitu kisicho hai.

Swali : Kuna msingi gani wa kisayansi unaowafanya watu waseme kwamba chembe ya kwanza ilitokana na kemikali zisizo hai?

Ukweli wa mambo: Wanasayansi wamebuni katika maabara, hali za kimazingira ambazo wanaamini zilikuwako mapema katika historia ya dunia.Katika majaribio hayo, wanasayansi fulani wametengeneza baadhi ya molekuli zinazopatikana katika viumbe hai.

Swali: Ikiwa kemikali katika jaribio hilo zinawakilisha mazingira ya awali ya dunia na molekuli inayotokezwa inawakilisha chembe za msingi za uhai, mwanasayansi aliyefanya jaribio hilo anawakilisha nani au nini? Je, anawakilisha matukio yaliyojitokeza kiholela au mtu fulani mwenye akili?

Ukweli wa mambo: Ili chembe iendelee kuwa hai, lazima protini na molekuli ya RNA zishirikiane.Wanasayansi wamekiri kwamba haiwezekani kuwa molekuli ya RNA ilijitokeza yenyewe. Uwezekano
wa hata protini moja kujitokeza yenyewe ni mdogo sana. Haiwezekani kamwe kwamba molekuli ya RNA na protini zingeweza kujitokeza zenyewe mahali palepale, wakati uleule na ziweze kushirikiana.

Swali: Ni nini kinachohitaji imani zaidi—kuamini kwamba chembe pamoja na mamilioni ya sehemu zake zinazoshirikiana kwa ustadi wa hali ya juu zilijitokeza zenyewe au kwamba chembe zilibuniwa
na Muumba mwenye akili?

Unajua katika jambo huwa linanishangaza kwa hawa wanasayansi ni hili,kama wao wamekuta dunia ipo tayari na viumbe vipo,hivi walishindwa hata kuwauliza au kutafuta taarifa zozote za kale zinazoelezea uumbaji ?

Sasa kama hivyo ndivyo,wao wanasayansi wanaujuaje ukweli ? Ina maana wanaujua ukweli kwa nadharia bunifu kisha majaribio kisha hitimisho au ? Kama hii ndio misingi yao ya kuupata ukweli ni upi ukamilifu wa misingi yao ?
 
Kwenye huu ulimwengu kuna vitu vilivyoumbwa kweli na vingine vilikuwepo kiasili au vimeumbwa kiasili

Vitu vilivyoumbwa kweli ni kama 7% tu ya ya ulimwengu, 93% ni pure conscious but formless energy namaanisha source/ source of energy au infinity source. Hapa ndipo wengi tunachanganyikiwa

Kwakuwa vitu vilivyoumbwa vina sehemu katika ulimwengu na matrix, uwepo (uhai) ni kipengele cha infinity source

Infinity source hufanya vitu vionekane (materialize) katika hali ya 3D na resultant effect ni polarity by default.The fusion and fission ya hiyo polarity na alchemistry ya opposing component ndio husababisha huu uhai wa muda (maisha)


Kwa hiyo (uhai) ni awamu au muhula wa muda wa kuwepo katika hii dunia

Ulimwengu wa matrix ukoje ? Kama ukitoa na mifano utakuwa umefanya jambo jema sana.
 
Kuna la ziada la kuniambia ?

Tujikite kwenye mada ya mdau sasa. Mimi kazi yangu kwako imeisha.

Nipo ...
Kazi gani? Yakupindisha kuraan?

Kuraan imesema udongo wenye kutoa sauti we unasema ukiogonga gonga, kwaiyo unaisahihisha ilipokosea?

Sent using unknown device
 
Our DNA was engineered by the supreme beings that occupy a wide range of conciousness katika plane of realm kubwa zaidi na ndo mana wanatufundisha namna ya kuimanipulate hata hiyo DNA yetu kisha kufanya hata mambo ya human cloning kwa kutumia recombinat au recession za DNA fragments zetu wenyewe...

Hapa bila shaka unawazungumzia Aliens sio ?

Unaweza kutuambia hao jamaa chanzo chao ni nini ? Au hawana chanzo ?

Nipo ....
 
Ningeulizwa kwenye mtihani hili swali la chanzo cha uhai ni nini ningejibu simpo tuu "pumzi"...
 
ATHARI YA KUJIFUNZA SAYANSI KABLA YA IMANI; TUSUBIRI WAKATI WA MAUTI YANATUKUTA TUTAELEWA ZAIDI CHANZO CHA UHAI WETU
 
Basi kwa taalumu uliyotumia hata wewe ni mwehu,

Leo hii anae amini mungu muweza wa yote na mwenye upendo kushindwa kudhibiti kifo anachukulia jambo hilo la kawaida sana, halafu wanasayansi ambao hawana uwezo wote kushindwa kuzuia kifo analichukulia kwa standard za juu

Hivi huu upuuzi ni lini utaisha

Sent using unknown device

UNA KIRANGA WEWE
 
Ngoja tunufaike kidogo ktk hili darasa.yule aliyetupa huo UHAI anasema
1. AMETUKUKA ambaye mkononi mwake umo Ufalme wote; na Yeye ni Mwenye uweza juu ya kila kitu.


2. Ambaye ameumba mauti na uhai ili kukujaribuni ni nani miongoni mwenu mwenye vitendo vizuri zaidi. Na Yeye ni Mwenye nguvu na Mwenye msamaha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na icho kitu ni lazime kiwe kimeumbwa na mwenye akiri zaidi ambae amekitengeneza
KAMA WEWE BINADAMU UNAUWEZO WA KUTENGENEZA GARI, NDEGE, VYOTE UMEVIUNDA KWA UWEZO WAKO.. BASI JUA KUNA MWENYE AKILI ZAID AMBAE AMEKUTENGENEZA NA AKAKUWEKA KWA AJILI FLANI.. .. HAKUNA KITU ETI..... BINADAMU AMEJIUMBA MWENYEWE...

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using unknown device
 
Back
Top Bottom