Chanzo cha Uhai

Chanzo cha Uhai

Basi kwa taalumu uliyotumia hata wewe ni mwehu,

Leo hii anae amini mungu muweza wa yote na mwenye upendo kushindwa kudhibiti kifo anachukulia jambo hilo la kawaida sana, halafu wanasayansi ambao hawana uwezo wote kushindwa kuzuia kifo analichukulia kwa standard za juu

Hivi huu upuuzi ni lini utaisha

Sent using unknown device
Kama katka maisha haya tu tumemtumaini Kristo, sisi tu maskini kuliko watu wote,

Lakini sasa Kristo amefufuka katka wafu, limbuko lao WALIOLALA.

Maana kwa kuwa MAUTI Ililetwa na mtu , kadhalika na kiyama ya wafu ililetwa na MTU..

Kwa kuwa kama katka ADAMU Wote wanakufa, kadhalika na katka Kristo wote WATAHUISHWA.

Lakin kila mmoja mahali pake; limbuko Ni Kristo; baadaye walio wake Kristo, atakapokuja.

Hapo ndipo mwisho, atakapompa Mungu Baba ufalme wake; atakapobatilisha utawala wote, na mamlaka yote, na nguvu.

Maana sharti amiliki yeye, hata awaweke maadui wake wote chini yamiguu yake.

ADUI WA MWISHO ATAKAYEBATILISHWA NI MAUTI.
1Kornt 15:19-26;

Nb: Zingatia palipo na herufi kubwa

Sent from my VFD 200 using JamiiForums mobile app
 
Ushuzi huu peleka kanisani, nipe jibu la swali langu

Sent using unknown device
 
Pumbavu sana hawa wanasayansi wajinga kweli kweli siwapendi ata kidogo , badala ya kujitahidi kuzuia watu tusife wanahangaika na vitu vya kijinga Hivi ;! Mara paap wakatuletea magurunet ili tuuane vzr wapumbavu sana siwapendi, .

Kama kuna mwanasayansi hapa mwambieni simpendi ,

Unrounded;

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuwatukana wanasayansi ni kujitukana mwenyewe.

Kumbuka kwamba kila mwanadamu ni mwanasayansi
 
Habari wana- JF!
Karibu katika makala fupi kuhusu "Chanzo cha Uhai"

CHANZO CHA UHAI

Wanasayansi wengi wanaoamini mageuzi watakuambia kwamba uhai ulianza mabilioni ya miaka iliyopita kwenye ukingo wa kidimbwi cha kale kilichojaa maji wakati wa kupwa au katika sehemu za chini ya bahari. Wao huhisi kwamba katika maeneo yasiyojulikana kama hayo, kemikali zilijikusanya na kuwa vitu vinavyofanana na mapovu,vikafanyiza molekuli tata, na kuanza kujigawanya-gawanya. Wanaamini kwamba uhai wote duniani ulijitokeza wenyewe tu kutokana na chembe “sahili,” moja au zaidi.

Wanasayansi wengine wanaoheshimika ambao pia wanaunga mkono mageuzi hawakubaliani na wazo hilo. Wanakisia kwamba chembe za kwanza au angalau sehemu zake kuu zilikuja duniani kutoka anga la nje.

Licha ya jitihada zao nyingi, wanasayansi hawajaweza kuthibitisha kwamba uhai unaweza kutokea ghafla kutokana na molekuli zinazodhaniwa zilitokeza uhai. Katika mwaka wa 2008, Alexandre Meinesz, Profesa wa Biolijia, alizungumzia utata huo. Alisema kwamba kwa zaidi ya miaka 50 iliyopita, “hakuna uthibitisho wowote uliopatikana kupitia majaribio yaliyofanywa unaounga mkono nadharia ya kwamba uhai ulitokea ghafla Duniani kutokana na molekuli fulani, wala hakuna maendeleo ya kisayansi yanayoweza kuthibitisha hilo.”

Siku zote uhai hutokana na uhai ambao tayari upo. Watafiti wamegundua kwamba ili chembe iendelee kuwa hai, angalau aina tatu tofauti za molekuli tata lazima zifanye kazi pamoja - DNA au deoksiribonyuklia asidi, RNA( ribonucleic acid), na protini. Leo, ni wanasayansi wachache wanaoweza kudai kwamba chembe kamili iliyo hai iliyojitokeza yenyewe kutokana na mchanganyiko wa kemikali zisizo hai.

Wanasayansi wengi huhisi kwamba huenda uhai ulijitokeza wenyewe kwa sababu ya jaribio fulani lililofanywa kwa mara ya kwanza mwaka 1953. Mwaka huo Stanley L. Miller aliweza kutengeneza asidi - amino, kemikali za msingi zinazofanyiza protini,kwa kupitisha nguvu za umeme ndani ya mchanganyiko wa gesi zilizodhaniwa kuwa zingewakilisha anga la Dunia. Toka wakati huo, asidi - amino zimepatikana pia katika vimondo. Ugunduzi huu haumaanishi kwamba kemikali za msingi za uhai zinaweza kujitokeza zenyewe.

Robert Shapiro, aliyekuwa profesa wa kemia katika Chuo Kikuu cha New York, anasema, “ Baadhi ya waandishi wameamini kwamba kemikali za msingi za uhai zinaweza kutengenezwa kwa urahisi kwa kutumia majaribio kama yale ya Miller na kwamba zinapatikana katika vimondo. Hata hivyo sivyo ilivyo.” * 1

Fikiria molekuli ya RNA. Imefanyizwa na molekuli ndogo zinazoitwa nukliotidi. Nukliotidi ni aina tofauti ya molekuli na ni tata zaidi kidogo kuliko asidi - amino. Shapiro anasema kwamba “ hakuna nukliotidi za aina yoyote zinazoripotiwa kuwa zilitokana na majaribio yanayohusu umeme wala katika uchunguzi wa vimondo. Pia anasema kwamba uwezekano wa molekuli kujifanyiza bila mpangilio maalum na kujikusanya toka kemikali nyingi za msingi “ ni mdogo sana hivi kwamba hata kama ungetokea mahali popote katika ulimwengu unaonekana ungeonwa bahati.

Mtafiti Hubert P. Yockey, anayeunga mkono fundisho la mageuzi ana maelezo zaidi. Anasema: “Haiwezekani kwamba chanzo cha uhai ni ‘protini tu.’”* 2 RNA inahitajika kutengeneza protini, hata hivyo, protini zinahusika katika utengenezaji wa RNA.

Je, kuna uwezekano wowote kwamba protini na molekuli ya RNA kutokea mahali pamoja kwa wakati uleule na kufanyiza uhai unaoweza kutokeza chembe ambazo zinaweza kuzaa na kuendeleza uhai?

Yaelekea uwezekano wa jambo hilo kujitokeza lenyewe, kukiwa na mchanganyiko usio na mpangilio maalumu wa protini na RNA, ni mdogo sana, anasema Dkt. Carol Creland ; mshiriki wa NASA ( National Aeronautics and Space Administration's Astrobilogy Institute).

1* Profesa Shapiro haamini kwamba uhai ulitokana na Muumba. Anaamini kuwa uhai ulijitokeza wenyewe kwa njia fulani ambayo bado haijaeleweka. Mwaka wa 2009 wanasayansi katika Chuo Kikuu cha Manchester, Uingereza,waliripoti kwamba wametengeneza nukliotidi katika maabara yao. Hata hivyo, Shapiro anasema kwamba viambatano vyao “bila shaka havifikii viwango vyangu vinavyokubalika vya kutengeneza RNA.”

2* Dkt. Cleland haamini masimulizi kuhusu uumbaji wa Mungu . Anaamini kwamba uhai ulijitokeza wenyewe katika njia fulani ambayo bado haijaeleweka vizuri.

UKWELI KUHUSU UCHUNGUZI WA KISAYANSI NA UHAI (UUMBAJI)

Ukweli wa mambo: Utafiti wote wa kisayansi umeonyesha kwamba uhai hauwezi kujitokeza wenyewe kutokana na kitu kisicho hai.

Swali : Kuna msingi gani wa kisayansi unaowafanya watu waseme kwamba chembe ya kwanza ilitokana na kemikali zisizo hai?

Ukweli wa mambo: Wanasayansi wamebuni katika maabara, hali za kimazingira ambazo wanaamini zilikuwako mapema katika historia ya dunia.Katika majaribio hayo, wanasayansi fulani wametengeneza baadhi ya molekuli zinazopatikana katika viumbe hai.

Swali: Ikiwa kemikali katika jaribio hilo zinawakilisha mazingira ya awali ya dunia na molekuli inayotokezwa inawakilisha chembe za msingi za uhai, mwanasayansi aliyefanya jaribio hilo anawakilisha nani au nini? Je, anawakilisha matukio yaliyojitokeza kiholela au mtu fulani mwenye akili?

Ukweli wa mambo: Ili chembe iendelee kuwa hai, lazima protini na molekuli ya RNA zishirikiane.Wanasayansi wamekiri kwamba haiwezekani kuwa molekuli ya RNA ilijitokeza yenyewe. Uwezekano
wa hata protini moja kujitokeza yenyewe ni mdogo sana. Haiwezekani kamwe kwamba molekuli ya RNA na protini zingeweza kujitokeza zenyewe mahali palepale, wakati uleule na ziweze kushirikiana.

Swali: Ni nini kinachohitaji imani zaidi—kuamini kwamba chembe pamoja na mamilioni ya sehemu zake zinazoshirikiana kwa ustadi wa hali ya juu zilijitokeza zenyewe au kwamba chembe zilibuniwa
na Muumba mwenye akili?

Kwani kati ya kifo na uhai kipi kilianza au kipi huanza ?
 
Wanasayansi wanaumiza vichwa kutafuta ukweli, alafu watu wa dini wanakuja na nadharia za kufikirika eti tumetokana na udongo, wengine eti udongo wenye kutoa sauti

Bora nikubaliane na wanasayansi kidogo fact yao inamake sense kuliko hii ya udongo

Sent using Jamii Forums mobile app

Ukiambiwa udongo unatoa sauti,kwa akili yako ndogo unafikiri unaongea nini ? Akili mmepewa bure,kwanini hamuitumii vyema na mkafikiri kwa usahihi.

Udongo ukipigwa pigwa au kupondwa pondwa hautoi sauti ?

Huwa nasema hivi,mwanadamu kutokujua mipaka yako ni ujinga wa kujitakia. Na mpaka mwisho wa dunia hakuna hakuna mwanasayansi atakae weza kuelezea uhai akapatia.
 
Hivi huoni unaisahihisha quraan kwamba imeongopa?? Mimi nimeweka kama ilivyoandikwa kwenye kuraan sijaongeza wala kupunguza nashangaa unavyobwata

Sasa udongo ukipondwa ukitoa sauti, utasema udongo unasauti?

Udongo gani ambao ukiupiga piga hautatoa sauti? Kama hakuna kulikua na maana gani kusema udongo wenye sauti wakati ikijulikana kua kila kitachopigwa kinatoa sauti?

Kuraan imetumia neno sauti ili kutofautisha na udongo ambao hauna sauti, halafu wewe unakana

Huoni kwamba unaipinga quraan mwenyewe kwa kutaka kubadili maneno yaliyomo ndani ukidai kua sivyo ilivyo kusudia?

Nakukumbusha kitu kimoja,hii tusiifanye huku ikwa mada,sababu kule kwenye mada husika mimi hili tulilimaliza.

Nakujibu hili,ili kuweka muhuri juu ya hili. Nakupa mfano huu. Sasa wapi nimekana ? Wapi nimesema kama udongo hautoi sauti ?
Tuliza akili uwe unasoma unaelewa sio unakurukupuka,pale nimekupa ufafanuzi tena kwa mfano ili uzingatie.

"Naenda kuoga" hivi kuna haja ya mimi kusema "Naenda kuoga maji ?"

Siwezi kuipinga Qur'aan na sina uwezo huo. Kama ulikosea kuilewa aya ile na ukashindwa kurejea kule ulikoitoa vipi utaepukana na makosa katika hili ?

Nipo ...
 
Ukisema unaenda kuoga inafahamika kua ni maji, lakini ukisema unaenda kuoga audio yenye yenye kutoa sauti ya maji unakua umeacha shaka

Ukiniambia kua kwani maji unavyoyaoga hayatoi sauti au mlio nikakuambia ndiyo yanatoa sauti, halafu wewe useme sasa kua umetumia audio yenye kelele za maji kuogea hivyo uko sawa na yule atakayetumia maji kuoga, kwasababu akioga yatatoa sauti kama yako iliyo kwenye redio yako

Hapo ukisema udongo wenye sauti hauna tofauti na huu mfinyanzi nao ujua mimi, huna tofauti na kuoga audio yenye kelele za maji

Sent using unknown device
 
Back
Top Bottom