Chanzo cha Uhai

Witted Jc

Member
Dec 28, 2018
58
116
Habari wana- JF!
Karibu katika makala fupi kuhusu "Chanzo cha Uhai"

CHANZO CHA UHAI

Wanasayansi wengi wanaoamini mageuzi watakuambia kwamba uhai ulianza mabilioni ya miaka iliyopita kwenye ukingo wa kidimbwi cha kale kilichojaa maji wakati wa kupwa au katika sehemu za chini ya bahari. Wao huhisi kwamba katika maeneo yasiyojulikana kama hayo, kemikali zilijikusanya na kuwa vitu vinavyofanana na mapovu,vikafanyiza molekuli tata, na kuanza kujigawanya-gawanya. Wanaamini kwamba uhai wote duniani ulijitokeza wenyewe tu kutokana na chembe “sahili,” moja au zaidi.

Wanasayansi wengine wanaoheshimika ambao pia wanaunga mkono mageuzi hawakubaliani na wazo hilo. Wanakisia kwamba chembe za kwanza au angalau sehemu zake kuu zilikuja duniani kutoka anga la nje.

Licha ya jitihada zao nyingi, wanasayansi hawajaweza kuthibitisha kwamba uhai unaweza kutokea ghafla kutokana na molekuli zinazodhaniwa zilitokeza uhai. Katika mwaka wa 2008, Alexandre Meinesz, Profesa wa Biolijia, alizungumzia utata huo. Alisema kwamba kwa zaidi ya miaka 50 iliyopita, “hakuna uthibitisho wowote uliopatikana kupitia majaribio yaliyofanywa unaounga mkono nadharia ya kwamba uhai ulitokea ghafla Duniani kutokana na molekuli fulani, wala hakuna maendeleo ya kisayansi yanayoweza kuthibitisha hilo.”

Siku zote uhai hutokana na uhai ambao tayari upo. Watafiti wamegundua kwamba ili chembe iendelee kuwa hai, angalau aina tatu tofauti za molekuli tata lazima zifanye kazi pamoja - DNA au deoksiribonyuklia asidi, RNA( ribonucleic acid), na protini. Leo, ni wanasayansi wachache wanaoweza kudai kwamba chembe kamili iliyo hai iliyojitokeza yenyewe kutokana na mchanganyiko wa kemikali zisizo hai.

Wanasayansi wengi huhisi kwamba huenda uhai ulijitokeza wenyewe kwa sababu ya jaribio fulani lililofanywa kwa mara ya kwanza mwaka 1953. Mwaka huo Stanley L. Miller aliweza kutengeneza asidi - amino, kemikali za msingi zinazofanyiza protini,kwa kupitisha nguvu za umeme ndani ya mchanganyiko wa gesi zilizodhaniwa kuwa zingewakilisha anga la Dunia. Toka wakati huo, asidi - amino zimepatikana pia katika vimondo. Ugunduzi huu haumaanishi kwamba kemikali za msingi za uhai zinaweza kujitokeza zenyewe.

Robert Shapiro, aliyekuwa profesa wa kemia katika Chuo Kikuu cha New York, anasema, “ Baadhi ya waandishi wameamini kwamba kemikali za msingi za uhai zinaweza kutengenezwa kwa urahisi kwa kutumia majaribio kama yale ya Miller na kwamba zinapatikana katika vimondo. Hata hivyo sivyo ilivyo.” * 1

Fikiria molekuli ya RNA. Imefanyizwa na molekuli ndogo zinazoitwa nukliotidi. Nukliotidi ni aina tofauti ya molekuli na ni tata zaidi kidogo kuliko asidi - amino. Shapiro anasema kwamba “ hakuna nukliotidi za aina yoyote zinazoripotiwa kuwa zilitokana na majaribio yanayohusu umeme wala katika uchunguzi wa vimondo. Pia anasema kwamba uwezekano wa molekuli kujifanyiza bila mpangilio maalum na kujikusanya toka kemikali nyingi za msingi “ ni mdogo sana hivi kwamba hata kama ungetokea mahali popote katika ulimwengu unaonekana ungeonwa bahati.

Mtafiti Hubert P. Yockey, anayeunga mkono fundisho la mageuzi ana maelezo zaidi. Anasema: “Haiwezekani kwamba chanzo cha uhai ni ‘protini tu.’”* 2 RNA inahitajika kutengeneza protini, hata hivyo, protini zinahusika katika utengenezaji wa RNA.

Je, kuna uwezekano wowote kwamba protini na molekuli ya RNA kutokea mahali pamoja kwa wakati uleule na kufanyiza uhai unaoweza kutokeza chembe ambazo zinaweza kuzaa na kuendeleza uhai?

Yaelekea uwezekano wa jambo hilo kujitokeza lenyewe, kukiwa na mchanganyiko usio na mpangilio maalumu wa protini na RNA, ni mdogo sana, anasema Dkt. Carol Creland ; mshiriki wa NASA ( National Aeronautics and Space Administration's Astrobilogy Institute).

1* Profesa Shapiro haamini kwamba uhai ulitokana na Muumba. Anaamini kuwa uhai ulijitokeza wenyewe kwa njia fulani ambayo bado haijaeleweka. Mwaka wa 2009 wanasayansi katika Chuo Kikuu cha Manchester, Uingereza,waliripoti kwamba wametengeneza nukliotidi katika maabara yao. Hata hivyo, Shapiro anasema kwamba viambatano vyao “bila shaka havifikii viwango vyangu vinavyokubalika vya kutengeneza RNA.”

2* Dkt. Cleland haamini masimulizi kuhusu uumbaji wa Mungu . Anaamini kwamba uhai ulijitokeza wenyewe katika njia fulani ambayo bado haijaeleweka vizuri.

UKWELI KUHUSU UCHUNGUZI WA KISAYANSI NA UHAI (UUMBAJI)

Ukweli wa mambo: Utafiti wote wa kisayansi umeonyesha kwamba uhai hauwezi kujitokeza wenyewe kutokana na kitu kisicho hai.

Swali : Kuna msingi gani wa kisayansi unaowafanya watu waseme kwamba chembe ya kwanza ilitokana na kemikali zisizo hai?

Ukweli wa mambo: Wanasayansi wamebuni katika maabara, hali za kimazingira ambazo wanaamini zilikuwako mapema katika historia ya dunia.Katika majaribio hayo, wanasayansi fulani wametengeneza baadhi ya molekuli zinazopatikana katika viumbe hai.

Swali: Ikiwa kemikali katika jaribio hilo zinawakilisha mazingira ya awali ya dunia na molekuli inayotokezwa inawakilisha chembe za msingi za uhai, mwanasayansi aliyefanya jaribio hilo anawakilisha nani au nini? Je, anawakilisha matukio yaliyojitokeza kiholela au mtu fulani mwenye akili?

Ukweli wa mambo: Ili chembe iendelee kuwa hai, lazima protini na molekuli ya RNA zishirikiane.Wanasayansi wamekiri kwamba haiwezekani kuwa molekuli ya RNA ilijitokeza yenyewe. Uwezekano
wa hata protini moja kujitokeza yenyewe ni mdogo sana. Haiwezekani kamwe kwamba molekuli ya RNA na protini zingeweza kujitokeza zenyewe mahali palepale, wakati uleule na ziweze kushirikiana.

Swali: Ni nini kinachohitaji imani zaidi—kuamini kwamba chembe pamoja na mamilioni ya sehemu zake zinazoshirikiana kwa ustadi wa hali ya juu zilijitokeza zenyewe au kwamba chembe zilibuniwa
na Muumba mwenye akili?
 
Mungu aliumba ulimwengu hizi zengine mbwembwe na kuonekana watu wajuaji Sana kukata imani za kuletewa wakati wao wanasoma elimu na syllabus walizoziandaa watu ili waendelee kusoma story zao na gunduzi zao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu naomba nikanushe kuhusu usemi huo unaosema kuwa ,ili uhai uwepo ni lazima DNA na RNA ziwepo kwa pamoja...No No No..big noooo...

Hakuna kitu kama hicho duniani na Ulimwenguni (kote)

Ni kwamba DNA ndo inayoprocess na kubeba au kuhifadhi codes( mwongozo) wote wa namna uhai wa kiumbe utakavyokuwa...

RNA ni kweli inahitajika kutengeneza protein lakini lazima ipate mwongozo toka kwa DNA..( kupitia RNA ndogi inayotengenezwa toka kwenye kipande cha DNA)

So DNA inaanza kutengeneza kwanza aina ya kwanza kabisa ya RNA inayoitwa Meseger RNA( mRNA) ambayo huwa inatengenezwa kwa kipisi kidogo cha DNA kinachojiachia kisha kutoka nje ya Nucleus na kwenda huko kwenye cytoplasm ambapo ndo kuna hizo RIBOSOMES ambazo zipo za aina mbili,kuna Larger subunit na smaller subunit lakini katika hizo Ribosomes kuna aina mbili tena ya RNA ambazo huwa zimeshatengenezwa ,nazo ni Transfer RNA ( tRNA) pamoja na Ribosomal RNA( rRNA) ambapo hiyo Ribosomal RNA kazi yake ni kutengeneza aina flani ya protein ambapo mfumo wake unakuwa umeletwa kwenye ujumbe na mesenger RNA( codon) ,kisha kufanyiwa activation na bwana Transer RNA ambapo kazi yake ni kumechisha aina au specific codon za mesenger RNA na zile anti codon zinazoletwa na Transfer RNA ...process hii itaendelea kufanyika mpaka pale urefu husika wa protein inayohitajika umekamilika kisha process nzima inajiachia kupitia terminating codon zilizopo kwenye mesenger RNA.

Mkuu DNA ndo kila kitu mzee..asikudanganye mtu RNA inasimama peke yake.??..

Yani DNA inaweza kumtengeneza bwana RNA kupitia process yake ya TRANSCRIPTION PROCESS, ili huyo RNA aje kutengeneza specific amino acids( proteins) Kupitia njia ya TRANSLATION PROCESS ili proteins za kutosha zipatikane kwa ajili ya kutengeneza organ au kitu flani katika mwili wa kiumbe husika..

Vile vile DNA mwenyewe anaweza undergo self replication kupitia process yake inayoitwa TRANSCRIPTION PROCESS ....

Kwa hiyo DNA ndo inabeba codes za kutengeneza kila kitu mzee ...

Naona somo la molecular analysis la DNA na RNA hujaligusa vizuri....kasome vizuri urudi hapa mkuu tutaeleweshana vizuri..

Waache au kama kuna ka upotoshaji kwa watu na hao maprofessor hukuwanukuu vizuri au ulielewa vibaya...na kama una source ya taarifa zao ziweke wazi tuzichambue hapa ki molecular zaidi ili tuone wapi RNA anasimama peke yake bila kutengenezwa na DNA....

Ndo mana katika molecular analysis hatuna analysis ya RNA, ila tuna analysis ya DNA, manake ndo kitu ambacho codes zote zimeifadhiwa mule ndani...

Ndo mana hata Viral replication anatumia DNA ya host cell na sio RNA yake make VIRUS hawana DNA ila wana RNA ,so wakiingia kwenye cell ya host cell wanaicomand DNA husika ifanya RNA replication ...

Nimekuwekea hapa chini uweze kuona ni kwa jinsi gani DNA inamtengeneza RNA kabla ya kuanza kufanya ujinga wowote anaotaka...

RNA ni mfanyakazi wa DNA ,ni kama kijakazi wa big sound mwenyewe(DNA...)

Narudia tena, soma molecular vizuri na uielewe vizuri...

DNA ndo kila kitu ...

Our DNA was engineered by the supreme beings that occupy a wide range of conciousness katika plane of realm kubwa zaidi na ndo mana wanatufundisha namna ya kuimanipulate hata hiyo DNA yetu kisha kufanya hata mambo ya human cloning kwa kutumia recombinat au recession za DNA fragments zetu wenyewe...

Hivi kama wameweza kutuonesha the total blueprint ya uhai wetu kwenye DNA pamoja na kuifanyia manuva yoyote, watashindwaje kuicreate....??

Soma maelezo hapa chini uone jinsi broo DNA anavyomtengeneza mwana mdogo RNA wako....
Screenshot_20190128-004907~2.jpeg
Screenshot_20190128-004934~2.jpeg
 
Waache au kama kuna ka upotoshaji kwa watu na hao maprofessor hukuwanukuu vizuri au ulielewa vibaya...na kama una source ya taarifa zao ziweke wazi tuzichambue hapa ki molecular zaidi ili tuone wapi RNA anasimama peke yake bila kutengenezwa na DNA....
Msamehe tu_nadhani ni copy & paste ya makala za mashahidi wa yehova

Sio kwamba imekosewa labda kawaelewa vibaya kutokana na aina ya uandishi wao wa mbwembwe kidogo na ugumu wa kuhariri Lugha sanifu
 
Kwenye huu ulimwengu kuna vitu vilivyoumbwa kweli na vingine vilikuwepo kiasili au vimeumbwa kiasili

Vitu vilivyoumbwa kweli ni kama 7% tu ya ya ulimwengu, 93% ni pure conscious but formless energy namaanisha source/ source of energy au infinity source. Hapa ndipo wengi tunachanganyikiwa

Kwakuwa vitu vilivyoumbwa vina sehemu katika ulimwengu na matrix, uwepo (uhai) ni kipengele cha infinity source

Infinity source hufanya vitu vionekane (materialize) katika hali ya 3D na resultant effect ni polarity by default.The fusion and fission ya hiyo polarity na alchemistry ya opposing component ndio husababisha huu uhai wa muda (maisha)

Kwa hiyo (uhai) ni awamu au muhula wa muda wa kuwepo katika hii dunia
 
Mwaga nondo mkuu
 
Pumbavu sana hawa wanasayansi wajinga kweli kweli siwapendi ata kidogo , badala ya kujitahidi kuzuia watu tusife wanahangaika na vitu vya kijinga Hivi ;! Mara paap wakatuletea magurunet ili tuuane vzr wapumbavu sana siwapendi, .

Kama kuna mwanasayansi hapa mwambieni simpendi ,

Unrounded;

Mwambie Mungu wako awaue hao unaowachukia
Anikajema ni munafiki mkubwa wewe
....
 
Pumbavu sana hawa wanasayansi wajinga kweli kweli siwapendi ata kidogo , badala ya kujitahidi kuzuia watu tusife wanahangaika na vitu vya kijinga Hivi ;! Mara paap wakatuletea magurunet ili tuuane vzr wapumbavu sana siwapendi, .

Kama kuna mwanasayansi hapa mwambieni simpendi ,

Unrounded;

Sent using Jamii Forums mobile app
Kisayansi kifo ni sehemu anayopitia kila kiumbe hai

Wewe mwenye mungu mbona ameshindwa kutufanya tusife

Sent using unknown device
 
Hata huyo mungu wako unayemwamini yeye pia ni mwanasayansi wa kiwango cha juu
Pumbavu sana hawa wanasayansi wajinga kweli kweli siwapendi ata kidogo , badala ya kujitahidi kuzuia watu tusife wanahangaika na vitu vya kijinga Hivi ;! Mara paap wakatuletea magurunet ili tuuane vzr wapumbavu sana siwapendi, .

Kama kuna mwanasayansi hapa mwambieni simpendi ,

Unrounded;

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe humjui Mungu, ndio maana huwez kulijibu hilo swali، sijataka uendelee kuhoji kuhusu Mungu ambaye hakuhusu, nazungumza kuhusu sayansi inayotuhusu na mnayojidai kuwa inatatua matatzo ya kiumbe na kuyachunguza? Kwann tunakufa?

Sisi tumeahidiwa maisha mengine baada ya kufa yatakuepo na huyo Mungu ambaye humtak
Mungu ni nani?? Leo hii unauliza swali hili wewe??

Wautoe kina nani?

Sent using unknown device

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom