Spain kuna majimbo makubwa 2 moja ya catalunya na nyingine Basque country ambayo yana mgogoro
Catalonia ilivamiwa na mfalme wa Spain na kuishikilia ardhi ile kimabavu na kuingiza Spain
Miaka ya nyuma Dictator Franco alipiga marufuku lugha ya kikatalunya kuzungumzwa ili kuvunja ukatalunya
Sasa kulingana na historia catalunya wanadai wao walikuwa huru ila Spain waliwachukua kimabavu na catalunya wana serikali yao ,rais kama vile Zanzibar
Na jitihada za kujikwamua ilianza toka miaka na miaka nyuma ndio maana klabu ya Barca miaka ya 1920's walikuwa wanatumika kama wanaharakati ila dictator Franco alipiga marufuku bendera za Catalonia kuingia nazo uwanjani..kujitenga kwao hawakuanza Leo ni miaka na miaka wamekuwa wanadai
Basque country zinapatikana athletic Bilbao, sociedad nao wanataka wajitenge na wana tamaduni na lugha yao ila case yao ipo tofauti na Catalonia