Chanjo yaua watoto morogoro | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chanjo yaua watoto morogoro

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mgirima, Aug 29, 2008.

 1. m

  mgirima Member

  #1
  Aug 29, 2008
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inaelezwa kuna watoto wa shule wamefariki na wengine kuzimia kufuatia zoezi la chanjo linaloendelea. Mwenye habari kamili atoe.
   
 2. M

  Mnyoofu Senior Member

  #2
  Aug 29, 2008
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 155
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Ni kweli, nipo dar lakini nimepigiwa simu kutoka kwa Masista wa Kolegina pale Kihonda Morogoro, kuna dada yangu pale amenisihi niwajulishe ndugu wote wa karibu kuwa mpaka saa 5 asubuhi inasemekana watoto 4 wa shule ya msingi ya Mji mpya na Mwenbe songo, zote ni za serikali wamefariki. Akaendelea kusema kuwa wote waliochoma hali zao ni mbaya sana.

  Nimepiga simu tena kwa jamaa zangu wa Wang'ula wanasema hali ni mbaya sana.

  Habari za kuaminika toka kwa jamaa yangu ambaye ni polisi -FFU pale morogoro amesema kuna vurugu kubwa sana zinaendelea, wazazi wamevamia mashule wanapiga wafanyakazi wa afya, na wamemwaga dawa za chanjo zote. Polisi imewalazimu kutumia mabomu ya machozi kutuliza ghasia hizi.

  Nimewajulisha uongozi wa juu wizara ya afya kufuatilia jambo hili na nimewashauri jamaa zangu wote wasiruhusu watoto wao wasipate chanjo hii mpaka uchunguzi ufanyike, Tafadhali eneza ujumbe huu kwa wote!
   
 3. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #3
  Aug 29, 2008
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Jamani hebu wasilianeni na Amina Said au news reporter yeyote wa Moro atupe zaidi. nimepagawa. Yaani nilitaka nipeleke mtoto wangu under five kwa matone na dawa za minyoo. Lakini nikajiuliza maswali mawili matatu kuwa kwani vitamini A inatokana na nini? Majibu nikapata kuwa wanangu wanakula mboga na matunda kila siku halafu every 6 months nawapa zentel syrup ya minyoo. Then why should I worry kuhusu minyoo na vitamini A. Halafu hiyo Surua ndo sielewi jamani. Kama kweli vifo vimetokea tuandamane jamani. Watu waelimishwe zaidi kuhusu ulaji wa vyakula bora na routine check ups za minyoo kwa watoto. Sielewi kwa nini mtoto anapewa chanjo ya surua then tunakuja kuambiwa turudie tena. Mbona mimi about 36 years ago, when I was 5 years ndipo nilidungwa chanjo ya kuzuia surua na hadi leo haijanipata? Au chanjo nazo ni feki kama zilivyo contract feki. Na nina imani chanjo hizo ni made in India. Wahindi watatumaliza!! Intentionally wanataka kuhamia wote TZ!!! Kama hatutakuwa makini nchi tunawapa Wahindi na wawekezaji uchwara, hasa Makaburu!!!
   
 4. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #4
  Aug 29, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Hivi tunaweza kufanya angalau kitu kimoja tu kwa usahihi wa asilimia 100?
   
 5. BabaH

  BabaH JF-Expert Member

  #5
  Aug 29, 2008
  Joined: Jan 25, 2008
  Messages: 703
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Haya bwana
  Hii ndio Tanzania, hapa sasa sijui mtatuambia nini tena?
  Haya bwana
   
 6. Mzeeba

  Mzeeba Senior Member

  #6
  Aug 29, 2008
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 145
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wazee hili jambo ni kubwa sana sana. Maana kwa habari toka morogoro ni kwamba chanjo hii imetolewa kwa watoto wote walio chini ya umri wa miaka 10. Hii ni mara ya pili kwa hizi chanjo kuwa na matatizo. Nadhani mtakumbuka ile iliyofanyika dar. Baya zaidi walikuwa wanatoa chanjo tofauti kwa wakati mmoja. Yaani ya surua, minyoo, pepopunda, TB na Matone ya vitamini A.

  Hizi chanjo huwa zinatolewa tofauti lakini kwa nini sasa sitolewe siku mmoja?

  Na nani amewapa waalimu nguvu za kuruhu watoto wachanjwe bila ruhusa toka kw wazazi wao?

  JF Doctor hebu tupe madhara ya kuchanganya chanjo zote hizi kwa wakati mmoja?

  Kwa walio karibu hii ni Morogoro tu au ilikuwa chanjo ya nchi nzima?

  Halafu tunasema eti Tanzania ina uongozi, Utoke wapi?

  Huu uzembe mpaka watoto watanzania wanakufa bila sababu za msingi na yenyewe tutaambiwa waziri kajiuzuluu?

  Hii inauma sana sana
   
 7. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #7
  Aug 29, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Bado nakuna kichwa sipati jibu hizo dawa lazima tujue kwanza ni Made in wapi?China au Tanzania au USA au India tunaomba mlio karibu na viboksi mtupe majibu......
   
 8. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #8
  Aug 29, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Nasikia hata Sumbawanga hii imetokea leo watoto wanaanguka anguka ovyo hebu tafuteni dot....kisha muunganishe.
   
 9. P

  Paullih Member

  #9
  Aug 29, 2008
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 85
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  mhn! labda ni zile dawa za kutoa kwenye chupa kubwa na kumimina kwenye vichupa vidogo vidogo. isijekuwa huyo aliyepewa maagizo ya kumimina akamimina sumu kimakosa na kupewa watoa chanzo. Iliwahi kutokea katika shule moja ya sekondari huko malangali iringa. wanafunzi wengi walipoteza roho zao. hapa ufanyike uchunguzi wa kina na chanjo hii isitishwe nchi nzima.
   
 10. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #10
  Aug 29, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Nasikia hakuna aliyekufa, isipokuwa wamepatwa na madhara kama kuishiwa nguvu na baadhi walipoteza fahamu
   
 11. B

  Baba Ubaya Senior Member

  #11
  Aug 29, 2008
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 127
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mlio karibu fatilieni mtupe data zaidi ni hatari
   
 12. Kwetunikwetu

  Kwetunikwetu JF-Expert Member

  #12
  Aug 29, 2008
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 1,544
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Ni kweli watoto wengi wamezimia mara baada ya kupata hiyo chanzo, mmoja ndio nimesikia amefariki. Nimepita maeneo ya hospitali kuu ya mkoa jioni hii kuna umati mkubwa wa watu wakisubiri kuona maendeleo ya tiba ya watoto wao ambao wamelazwa baada ya kuzidiwa na dawa hiyo ya chanjo
   
 13. M

  Midas Touch Member

  #13
  Aug 29, 2008
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 74
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 15
  Mimi nimekuwa Morogoro for the last 4 days. Hii habari ni kweli kabisa ila real figures hazijapatikana officially. Nasikia hata polisi wamepigwa na watu wenye hasira kali. Vijiwe vyote na kona zote habari hii imetawala.
  My question is: Huu ni mradi wa watu fulani mafisadi waliotoa deadly fake immunization drugs? Watoto wengi wamelewa na kuzimia. INAUMA KWELI!
   
 14. M

  Masatu JF-Expert Member

  #14
  Aug 29, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Be organised kabla hamja kurukupa get ur facts correct. Hii habari ni nzito na inahusu taifa ku speculate watoto wamekufa ilhali hamna uhakika sio jambo zuri kabisa
   
 15. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #15
  Aug 29, 2008
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Kuwe na vifo au hakuna langu kubwa ni juu ya Wizara ya Afya. Kuna nini mpaka utoe dawa za aina hii kwa pamoja kiasi kikubwa hivi. Tuna outbreak yoyote inayolazimisha tiba ya aina hii?

  Na tena eti chanjo zinarudiwa. Kwa sababu ipi. Au ndo kuhalisha ufisadi wa matumizi mabaya ya pesa maana nasikia Wizara yetu ndo yenyewe kwa dili na makampuni ya madawa na hasa ya India.

  Bila kunishawishi kisayansi sina sababu ya kumushawishi ndugu kuchanjwa mara ya pili, tatu n.k.
   
 16. Muacici

  Muacici JF-Expert Member

  #16
  Aug 29, 2008
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 208
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Ni kweli Mpita njia mimi ni mkazi wa Morogoro na watoto wangu walipata hiyo chanjo ni uvumi hakuna yeyote aliyekufa katika hizo shule zilizotajwa. Hapa Chamwino nikweli wazazi walikasirika baada ya kusikia hizo porojo wakaleta ugomvi hadi FFU wakaja kutuliza ghasia hiyo.

  Habari ya kweli ni kwamba watoto wengi dawa iliwazidi nguvu, na sababu kubwa ilikuwa lishe. Shule zilizopatwa na mkasa huo hazikusimamia vizuri watoto wakati wa kupata uji.
   
 17. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #17
  Aug 29, 2008
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Usiseme kukurupuka. Hili si taifa linalohitaji uangalifu ili uweze kuamua mambo. Unayoyasikia ni matokeo ya kutoamini busara za serikali. Hazipo!

  Kumbuka Vaccine ya polio na kampeni zilizoendeshwa bila sababu juzi hapa. Inafikia wakati hiyo Wizara inaamua tu kuendesha kampeni za kihuni ili ufisadi ufanikiwe.

  Niliwahi kusikia kuna wakati wanaamua kuagiza maji ndani ya vials na kuchanja watoto. Baadaye wenye huruma wakija tena wanaamua kuagiza chanjo halisi na kutangaza kurudia zoezi.
   
 18. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #18
  Aug 29, 2008
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Vaccine Development Practices
  Kuna kitu huwa general public haifahamishwi. Katika utafiti wa kitabibu hasa ukihusu uendelezaji wa madawa na chanjo kuna kitu wanakiiita "Guinea Pigs" Kabla ya kwenda kutumiwa kwa general public hu-sample either age fulani, au sex fulani, au watu wenye tabia fulani, na kuwadunga au kuwachanja chanjo hizo na kisha mara kufuatialia A to Z reactions, effects etc za kile walichompatia candidate wao. Na yawezekana kabisa wala sio chanjo kwa kitu walichokisema inawezekana kwa kitu kingine yaani hapa wana-Blind Fold participants wakiona vile inafaa au inahitajika.

  Outcomes
  Sasa kuna mawili ama bado iko kwenya phase hiyo ya "Vaccine Development Research Studies" au ndo hawakufanya vizuri katika phase hiyo awali ama sample size ilikuwa kidogo kuweza kutoa majibu hayo na kufanyia marekebisho nk. Kwaufupi hii ndo inaweza kuwa kisa chake.

  What to do
  Baada ya hapa watawachukua wale waloathirika na kuendelea na utafiti wa kina ili kujua athari kwa wengine ni nini chanzo ili kuweza kujua ni watu wepi hawapaswi kupata chanjo hiyo au kutengeneza njia ya kuwa-test watu kabla ya chanjo hiyo yaani "Sensitivity Test", watakao-react against hawatapata chanjo hiyo na wale watakaokuwapoa ndo watapata. Na inabidi hata hivyo kuendeleza tafiti ili kutengeneza chanjo nyingine kwa magonjwa yale yale ila mbadala kwa wasopatana na ile iliyowadhuru. It is very very expensive to develop any vaccine. It is tedious as well but all in all GOOD job kama wameathirika wachache kiasi hicho we can say a vaccine is effective to use to general public cause with side effects its 99.999999999999% OK for use only 0.00000000000001% not ok which is all vaccines works within or along the specified % frame.

  Kwa anayebisha kwa hoja atuelimishe zaidi badala ya kupotoka na kuogopa kuwahimiza watanzania kupata chanjo.

  Health Sector - Vaccine Development Team
  You have a lot to work out and make sure you are there or your trained manpower on the prescibed vaccine to help the public just incase when there is an issue of side effects and develop a contra-indication checklist
   
 19. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #19
  Aug 29, 2008
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145

  Tume
  Tutaunda tume mapema kuchunguza na kisha taarifa tutaiweka katika sefu ya waziri wizara ya afya. Au vipi masela?
   
 20. Mzeeba

  Mzeeba Senior Member

  #20
  Aug 29, 2008
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 145
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hatuhitaji Tume tena. Tunahitaji kuwaondoa hawa jamaa.

  Ndugu zangu hata mimi na mtoto mdogo morogoro ni kwamba tu leo walisahau kuhusu chanjo kwa hiyo hawakumpeleka, la sivyo tungekuwa tunaongea mengine labda. Tunaomba habari za uhakika zaidi maana kwa habari nilizonazo ukiacha watoto waliozimia ni kwamba wapo walio kufa. Lakini siwezi kudhibitisha hilo. Nadhani kamanda wa mkoa atatoa taarifa karibuni na tutajua ukweli.

  Hili ni kubwa sana, sana...
   
Loading...