Chanjo ya ugonjwa wa kisonono yapatikana

Chanjo ya ugonjwa wa kisonono yapatikana

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
8,274
Reaction score
25,322
_96883578_aab941fa-44ac-4cc3-87f7-27a9993d79b4.jpg

Wanasayansi nchini New Zealand wameonyesha kwa mara ya kwanza kwamba chanjo inaweza kutoa kinga dhidi ya ugonjwa wa kisonono.

Watafiti kutoka chuo kikuu cha Auckland wamegundua kuwa maambukizi ya ugonjwa huo wa zinaa yameshuka kwa takribani theluthi moja miongoni mwa watu ambao walipata chanjo dhidi ya homa ya manjano.

Watafiti hao wamefuatilia kutoka kwa vijana milioni moja waliopata chanjo hiyo pindi kulipotokea ugonjwa wa homa ya manjano nchini New Zealand.

Kisonono imekuwa taabu kutibika kwa sababu imezoea dawa za antibiotic.

Mwandishi wa BBC wa masuala ya afya anasema utafiti huu unaonyesha inawezekana kuwa na chanjo dhidi ya ugonjwa.

Chanzo:
BBC
 
Chanjo 'imepatikana'?!!!

A mere UTAFITI at initial clinical trials afu wewe unasema Chanjo 'imepatikana'!

Uandishi wa kikanjanja. Si ajabu nawewe ni 'employee' kwenye media house bongo.

-Kaveli-
 
Wenye visonono mkuje na huku kale ka tiba sasa kamepatikanaga bwaana soon kaswende nayo itapata tiba ya uhakika
 
Back
Top Bottom