#COVID19 Chanjo ya covid-19 kutua hivi karibuni

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,001
9,866
Serikali imesema ipo katika hatua za mwisho za mazungumzo kwa ajili ya kupata chanjo ya ugonjwa wa covid- 19 kwa ajili ya wananchi.

Kwa mujibu wa Wizara ya Afya, mazungumzo hayo na kampuni ya Global Alliance for Vaccines (Gavi) yanakaribia kuzaa matunda, ambapo Sudan Kusini iliyopata Uhuru wake mwaka 2011 itapata mamilioni ya chanjo hiyo.

Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Afya ya Kinga katika wizara hiyo, John Rumunu aliwaambia waandishi wa habari wiki iliyopita kuwa, serikali inajiandaa kupokea shehena ya chanjo ya covid- 19 kutoka Gavi.

Mpango wa utoaji wa chanjo ya ugonjwa huo duniani utasaidia kulipa gharama za mwanzo wakati huu yakifanya majaribio ya chanjo hiyo inayotarajiwa kuanza Januari mwaka huu.

“Serikali imeiomba Gavi kusaidia kulipia mzigo wa kwanza utakaofika siku chache zijazo,” alisema.

Rumunu alisema serikali imethibitisha kuwapo wagonjwa wa covid- 19 wapatao 5,210 kwa sasa na waliopona ni zaidi ya 3,131 na vifo hadi kufikia jana ni 63.

Taarifa ya idara hiyo iliyo ilisema ni haki ya Sudan Kusini kutoa chanjo kwa watu wake kama zinavyofanya nchi nyingine duniani.
 
Uingereza hata leo unashambuliwa na ongezeko la wagonjwa wa Covid 19 na huku wanaanza kutoa chanjo c waanzie wenyewe huko kwn lazima waanzie huku, sisapoti hii kitu na ninaomba serikali ya Tz isikubali hii kitu, Mungu atusaidie sana.
 
Wenzetu hilo australia wamechanjwa covid-19, wamejikuta wote Wana HIV + Hiyo chanjo waanze kina kabudi kwanza sisi tuwe wa mwisho
Ile ilikuwa hitilafu katika vipimo (false-positive). Hata upande wa COVID-19 kuna false-positives na false-negatives pia.
 
===
Madhara ya chanjo haya hapa!

 
Serekali yetu iwe makini sana na hii chanjo ipo documentary moja imekatazwa kabisa duniani juu ya ugonjwa bunifu kwa ajili ya ku depopulate raia tubaki na imani yetu hii hii kwamba hatuna hiyo kitu and we are safe kutakuwa na ubaya gani? [tujifukize tu kiasili] ingawaje tutakapoikataa moja kwa moja huenda tukapata misukosuko ya hapa na pale kwa sababu tutakuwa tunakwamisha njama za makusudi za watu fulani
 
Uingereza hata leo unashambuliwa na ongezeko la wagonjwa wa Covid 19 na huku wanaanza kutoa chanjo c waanzie wenyewe huko kwn lazima waanzie huku, sisapoti hii kitu na ninaomba serikali ya Tz isikubali hii kitu, Mungu atusaidie sana.
Juzi hapa nilishitushwa sana na habari kutoka Kenya iliyo dai eti taasisi ya KEMRONI ikishirikiana na taasisi ya Oxford inayo jishughurisha na utafiti ,majaribio na utengenezaji wa chanjo ya COVID-19 eti wamegunduwa kuna strain mpya ya COVID-19 ambayo haipo popote Duniani zaidi ya Kenya!

Kinacho tisha zaidi wanasema strain hiyo mpya imegundulika Jimbo la TAVETA, sasa statements hizo zina lengo gani tukitilia maanani kwamba Taveta hipo mpakani mwa Kenya na Tanzania!!

Hawa watafiti kutoka Uingereza Chuo kikuu cha Oxford, kwa nini wana shahuku sana ya kufanyia majaribio ya chanjo zao Barani Africa specifically Kenya, Nigeria na South Afrika na sio kwao Uingereza, tuliambiwa kwamba huko Uingereza majaribio yalifanyika kwa kuwachanja sokwe mtu na si binadamu - kibaya zaidi taasisi ya Oxford inafadhiliwa na Bill/Melisa Gates foundation, Soros, Rockerfeller foundation, Buffet na Rothschild's family - genge la jamaa hawa ni hatari sana kwa ustawi wa binadamu Duniani, wana malengo ya kishetani kabisa.

Binafsi naona itakapo bidi Taifa letu kuanzisha zoezi la kuchanja Raia wake ni vyema Serikali yetu ikinunua chanjo za COVID-19 kutoka Uchina na Urusi ambako tuna uhakika hawana ajenda za siri za kupunguza idadi za wanadamu kwenye third World Nation.

Vile vile suala la Kenya kudai eti kuna aina mpya ya corona huko TAVETA, hapo naona Serikali yetu ifatilie taarifa hizi kwa karibu sana ili wajiridhishe ukweli huko wapi, hisije zikawa ni mbinu za Kenya kuwatisha watalii wasije hifadhi ya Ngorongoro na Serengeti ambazo zipo mpakani na Kenya au isije ikiwa na mbinu za taasisi ya Oxford kupandikiza aina mpya za corona zenye uwezo mkubwa wa kuwamaliza Waafrika baada ya kuona kwamba strain ya kwanza haiku waathili sana Waafrika ukilinganisha na wazungu, haya mambo siyo ya kuchukulia poa hata kidogo.
 
Back
Top Bottom