Chanjo kutoka USA na EU

Baniani baya kiatu chake dawa.

Pamoja na ubaya wake mmarekani na EU lakini inapokuja kwenye masuala ya ubinadamu na haki za binadamu hawa jamaa wako far sana, Ni Nchi zinazoongoza kwa kutoa misaada hapa Duniani haswa Nchi za kiafrika na Asia, ni Nchi zinazoongoza kqa kupigania usawa wa kibinadamu kwa jamii kubwa ya Dunia ya tatu.

Tuseme kweli, Africa na viongozi wake bila Marekani na EU ni bara giza kabisa.

Yes, Mrusi ana mchango wake ila hauwezi hata siku moja kufikia mchango wa Marekani na EU.

Napenda Demokrasia so mtu yeyote ambaepambana kuleta usawa bora kwa jamii kwangu ndio mfano wa kuigwa.


Wengi wetu hatuna cha kujifunza toka Moscow ila tuna mengi ya kujifunza kutoka US na EU, hata wengi tuochangia huu mjadala hapa ukiambiwa kati ya kuishi London au Moscow asilimia 98 tutachagua London.


Thanks US na EU bila ninyi nadhan nisingekuwa natumia IOS, Android, Windows n.k.


Wengi wetu humu tumetolewa ujinga baada ya kupata western education.

KOICA na JICA pia asanteni kwa kidogo ambacho mnapambana kuisaidia Nchi yetu.


Kwa Msaada wa watu wa marekani, EU, Koica na Jica.


Kama ulishawahi kuona bango lolote kwa msaada wa watu wa Russia au North Korea nimekaa palee niitwe 🐒
 
Nakuunga mikono na miguu. Waafrika hawanaga shukurani mwenye msaada kwao(nchi za magharibi) ndiye anayedharauliwa ila yule asiyekuwa na msaada kwao ( Russia) ndiye wanayemsapoti.
 
Ubarikiwe mkuu, Bila USA na EU ungekuta tulishakufa kwa Ukimwi , Kifaduru, Chanjo Moja kwa mtoto ni laki 6.Maskini utapata wapi ? Matakore mengine hayana akili hapa . Kuna kipindi mwenda zake aliwekewa dizaini ya hizi chànjo za watoto mbona tulienda Namanga kuzitafuta .
 
base zao zipo africa ili kutusaidia kupambana na magaini ya kiislamu ili mataifa yetu yaishi kwaa amani na upendo.
swali lingine tafadhali.
Wewe kumkichwa chaji imeisha!
Magaidi yanatengenezwa na wao ili duniani kuwa na migogoro halafu waingie wakaibe,
Asilimia kubwa sehemu zote zenye magaidi kuna mali ama mafuta au hata madini au pia yaweza kuna masilahi yao binafsi.
 
Angalia hata kwenye bega lako kama huna alama ambayo umechanjwa ili usife halafu unakuja kumdharau Mmarekani .
Shida ilianzia kwenye USHOGA, kutuaminisha kwamba USHOGA ni kitu cha kawaida sasa wewe leo ugeuzwe SHOGA upo tayari mkuu upelekewe moto kwenye hio puru yako utakubari?
 
Somalia , Msumbuji , Mali , Nigeria,Niger Cameron. Migaidi ya kiislam yamejaaa sana
Ulishawahi kufanya hata tu research ndogo ukagundua nini tatizo na ulishajiuliza kwa nini Somalia waliondoka kwa kusingizia eti wameshindwa hivi Marekani anaweza akashindwa na Somalia?.
Zivujie basi Mkuu.
 
Anayedharau uwezo wa Marekani na Eu bloc kiuchumi na kijeshi apimwe akili.

Lakin pia anayedharau uwezo wa Urussi na China kiuchumi na kijeshi Apimwe mkojo..

Hizi Bloc 4 ziheshimishwe duniani

1. US
2. Russia
3.China
4.EU

Tatizo linaanzia hapo
Amezungumzia mambo ya misaada. Kwa vile unataka kuwatetea hao mabaradhuli ndio maana umekwepa issue ya misaada
 
Kaka huyo hayajui madudu ya marekan. marekani ni mashetani sio watu wale
 
Bila hao ulio wataja hapo juu hata hayo magonjwa yasinge kuwepo trus me
 
Hakuna msaada wa bure kijana. Fuatilia kilichowakimbiza Ufaransa kule Mali.
 
Mkuu unajua sana kufikiria . Mwambie mkuu chanjo zote ni misaada kutoka USA na EU , ukija kuangalia Africa bila Wazungu hamna kitu tutarudi kule kwa ujima mkuu.
 
Muache kula popo wa porini na kima , Sokwe mtu , nyani , hawa ndio wanaobeba virus .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…