Changamoto za harusi

Changamoto za harusi

Kimbori

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2012
Posts
6,464
Reaction score
5,133
Kuna changamoto kibao zinazowakumba wachumba wanakotangaza nia ya kufunga ndoa, na kufanya harusi.
Naomba tujullishane magumu yaliyokupata, au kumpata mtu yeyote.
Hii itasaidia kuwaandaa wachumba kisaikolojia ili kuyakabili makwazo.
Karibu!
 
wanawake wanapenda harusi ya 1 day kuliko maisha ya ndoa ya 40 yrs.. maana wedding day ni kupendeza na raha tu huku maisha ya ndoa ni shida na raha miaka yote..

so wao wanaipenda siku ya raha tu...

all in all ndoa nzuri sana hasa wote muwe mmetunza hekalu la Mungu.. muwe ma bikira
 
Chanangamoto ni nyingi baadhi ni familia kutokuridhika na kabila,, elimu, kazi ya muhusika au muonekano wa mmoja wapo.. Cha msingi kabla hamjafika kwa wazazi kutambulishana ni vema mkijiridhisha nyie wenyewe wahusika.. Binafsi naamini hakuna uchumba usio na changamoto km utabahatika kutokukutana nazo kwenye uchumba basi utakutana nazo kwenye ndoa.. Uchumba na ndoa ni makubaliano baina ya watu wawili ambao ndio msingi hasa... Wengine hawapaswi kuingilia ndoa yenu isipokuwa wanapaswa kuwa shauri tu.. Hakuna mkamilifu isipokuwa na hili utakuwa na lile.. Yapo yanayorekebishika na mengine hayarekebishiki.. Usitegemee kumbadilisha mtu akiwa ndani ya ndoa km wa chumba wa naona Kuna udhaifu ni heri kuvunjwa uchumba mapema kuliko kuruhusu ndoa ukiamini eti at a badili ka.. Tabia ni ngozi.. All in all sikikizeni mioyo yenu inasemaje hakuna mchungaji wala shehe ktk hili
 
Moyo umelia paaa!, inamaana nimuache.....Naona anatabia ya "KICHECHE WA UVUNGUNI". Anajifanya kushinda kanisani, nimepata neno lako........Limeanza kunipa msongo wa mawazo alafu kama lina ukweli hivi......usipoziba ufa utajenga ukuta ndilo litakalofuata kwangu
 
Umeoa/ umeolewa na masikini,, wana tabia mbaya, wana viburi na hawashauriki, .....
Kuna mmoja aliwahi kumchagulia kijana wake binti wa kabila fulani, kabla ukuadi haujakamilika, yule binti akatofautiana na mama. Baada ya muda kijana akamleta binti wa kabila hilo na mwenye kiwango cha rlimu na kutoka familia ya kawaida. Huyo mchumba alisakamwa mpaka akakonda.
Kuna ndugu hufika hatua ya kutotoa mchango, japo ndoa ilifungwa.
 
Hii posti imenilenga sana mimi, nipo kwenye maandalizi ya harusi naona km utumbo unagusana na maini,
 
Siku yenyewe mademu wana-bleed kwa sababu ya woga, halafu usishangae umeingia ukumbini kabla hujapata chakula cha mchana sababu ya kukimbizana asubuhi mpaka muda wa kanisani/msikitini.
 
wanafiki watajitokeza na maneno kibao kuonyesha ulifanya chaguo baya! kujifanya wanawajua ninyi sana ili muachane
 
Hii posti imenilenga sana mimi, nipo kwenye maandalizi ya harusi naona km utumbo unagusana na maini,
Pole kwanini una hofu... Jipe moyo kwakua tayari mpo kwenye maandalizi ila huwa nahofia sana... Kijana umesoma kwa mda mrefu.. Umetafuta kazi au maisha kwa Muda mrefu sana.. Unatakiwa uishi na ndoa yenye amani kwani ndoa ndio safari ya mwisho yenye mlolongo mrefu sana ambao kifo tu ndio kiwatenganishe... Huwa naumia sana kuona mke au mume anakuwa mwiba kwa mwenzake.. Wapo Vijana wengi baada ya kuoa huingia kwenye ulevi wakiamini huko hupoteza mawazo na mda ili wakifika nyumbani walale.. Jamani tutambue kuwa ktk ndoa tumekutana ukubwani kila mtu kakulia na kulelewa ktk mazingira yake tabia zake nk.. Hivo mnapokutana ni vema kila mmoja akawa mwalimu wa mwenzake kwa kila jema analoliona linafaa kujenga ndoa na familia kwa ujumla.. Tukubali kukosoana kwa nia njema tu.. Tukubali kumfundisha a kwa nia njema tu... Tukumbuke maisha mengine tumejifunza kupitia wazazi wetu walivokuwa wakiishi.. Nasi tukaadapti tukijua ndivo Unatakiwa kuwa.... Elimu zaidi inahitajika kwa wanandoa.. Tusi tegemea kuona wazazi walivokuwa wanatukanana mbele ya watoto wao eti watoto wao wanapooa au kuolewa waliepuke hivo never.... Tusi tegemea wazazi wa likuwa wanalewa au mama anamchepuko mpk mtoto anajua halafu utegemee bint akiolewa ataliepuka Hilo never.... Mungu awasaidie Vijana wote wake kwa waume wote wawe na utayari toka moyon kwa Kuingia kwenye ndoa na si maigizo... Wawe na utayari wa kujifunza na kutunza ndoa zao... Kubwa ni Kila mtu kumkubali Mwenzake jinsi alivo... Tusionae eti kwakua mmepeana mimba au nimelazimishwa au mama angu amempenda eti anamuonekano mzuri nk... Mkishaingia kwenye ndoa kila mtu hutegemea familia yaani watoto uwapo Mungu atabariki hili... Je wakipatikana halafu ukangundua kuwa huyu sie.. Nani alee watoto wako... Wakati upo Hai!! Ndoa zinachanagamitao ila mkizielewa na kila mtu akamjua mwenzio kuwa nini hapendi nini a napenda... Mtaenda sawa.. La msingi ni kujua kuwa hamtaishi maisha ya honeymoon kila siku ipo siku mtakwaruzana ila isiwe sababu... Ni vema mkayamaliza ili amani iendelee nyumbani... Kila la heri wote mnaotegemea Kuingia huku. Karibu sana msiogope.. Kumbukeni kuelezana mapema nini hapendi nini unapenda mweleze mwenzio tabia ambazo hutakuwa tayari kuzivumilia... Ili km anazo basi aanze kuzikwepa kabla... Tatizo tunaogopana kuwa je nilimwambia akichukia heri achukie achukue maamuzi kuliko kuishi na mwiba...
 
wanawake wanapenda harusi ya 1 day kuliko maisha ya ndoa ya 40 yrs.. maana wedding day ni kupendeza na raha tu huku maisha ya ndoa ni shida na raha miaka yote..

so wao wanaipenda siku ya raha tu...

all in all ndoa nzuri sana hasa wote muwe mmetunza hekalu la Mungu.. muwe ma bikira
kweli mkuu maana mtu yupo radhi kuolewa na yoyote kisa harusi
 
Uzi mtamu sana huu...wengine hata tunaogopa kuingia hata kuingia kwnye mahusiano...Ila hapa kuna vya kujifunza!
 
Harusi....ule mzunguko wa kufuatilia michango bhana,bado wiki moja,nusu ya bajeti bado kukamilika,mwingine unampigia hapokei,yule uliyemtegemea sana atakupa kiasi cha kutosha anakupa kiduchu,kule mtunza hazina kama humuelewi flani unahisi kapiga panga....kizungumkuti.
 
Umeongea ukweli aisee yaani kunakuwa kutoaminiana sana
 
Back
Top Bottom