Changamoto ya mtoto kulia sana usiku

Changamoto ya mtoto kulia sana usiku

Ndugu poleni na mjukumu ya kutwa nzima.

Wapendwa hii sasa imenizidi nguvu siku ya tatu sasa sijafanya kazi yoyote. Mwanangu na umri wa mwaka na miezi 4 kuikweli huyu mtoto sijajua shida nini hasa nimejaribu kwa madaktari bingwa wa watoto sijabahatikaa kuona tofauti yoyote nimejaribu kuingia kwenye maombi napo bado sijaona tofauti changamoto zinazo mkabili ni kulia sana usiku na kukohoa hadi kutapika usiku

Hii ikifika mida ya saa 4 mtoto anashtuka na kuanza kulia sana namkumbatia anaendelea kulala hapiti mda anashtuka analia hadi kunakucha nimwendo huo hua analala nashtuka na kulia ila ikifika saa 10 anaanza kukohoa sana kana kwamba kuna kitu kimemkaba hadi anatapika ndio anakaa sawa.

2. Hatambai wala hatembei
ndugu zangu nampenda sana mwanangu cha ajabu kila napo anapotaka kutambaaa anaanza kuumwa .

3. Hali ugali bila maji
mwanangu hawezi kula ugali bila maji yaani hawezi kuumeza bila maji hata uwe mlaini vipi.

kunywa uji au juisi hataki hata viwe vitam kiasi gani.

NIMEHANGAIKA SANA JUU YA HUYU MTOTO LAKINI SIJAPATA MABADILIKO.

Sasa ani saa 3 mtoto anaanza kulia hadi kunakucha
NAOMBENI MSAADA WENU NDUGU ZANGU
Pole sana!

Ameweza kutqmka maneno ya kitoto (babbling)?
nashauri uende hospital kubwa afanye MRI,Ct Scan

Inaweza kua ni tatizo la Usonji ( Autisim) wahi mapema
 
Tafuta BONISAN au GRIP WATER utakuja kunishukuru.
 
Pole sanavkwa changamoto unazopitia.
Hayo maswali yanaweza kuksaidia kutafta chanzo kiutalamu
1 .KWanza mtoto wa mwaka 1 anatakiwa awe na kilo angalau 10 na kuendelea.wako ana ngp?
2 . Mwaka 1 na miezi. 4 na hajaanza kutambaa hapo tunasema kachelewa kwenye stage ya ukuuaji tena sana(delayed millestone). Sahvi anawez kufany nn upand wa ukuuaji? Ashawahi kuugua utapiamulo?

(Kama bado ypo legelege kwenye mikono au miguu au upande mmja wa mwili ni dhaifu ndo hio ishu ya utindio wa ubongo/celebral palsy inaibuka)

3 . Hio kukohoa na kutapika. Nawez kusem inawezekan kua n hali ya utumbo haujakaa sawa kumeng'enya chakula vzri ila kuna watoto uzaliw na changamoto z utumbo kujikunja. Choo anapata? Ulimnyonyesha miez 6 ya mwanzo bila kumpa chochte?

4 . Kwako mama, Kipindi cha ujauzito wake kuugua? Ulimzaa ana kilo ngapi? Ulijifungulia hospitali au nyumbani? Chanjo amepata ipasavyo?
5 . Ulijifungua kwa njia y kawaida au operation? Mtoto alichelea kulia baada y kutoka tumboni? Kwenye kitovu hajawahi shida kam kupata usaha. Ashawahi kua na manjano?
ILA kama hayo yote yapo vzri mtaalamu ausike ktafta chanzo maana sio kawaida.
Nimuhimu akafanya EEG, huenda mtoto ana kifafa au matatizo mengine ya ubongo
 
Back
Top Bottom