Changamoto ya mikopo ya HELSB

Changamoto ya mikopo ya HELSB

CORAL

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2011
Posts
2,827
Reaction score
1,858
Ndugu walimu wenzangu na wanufaika wote waliosomeshwa kwa fedha ya serikali yaani BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU (HESLB). Juzi Jumatatu tarehe 28.12.2020 niliomba LOAN STATEMENT ya deni langu kutoka Bodi ya mikopo ili niweze kuclear deni baki ambalo kwa mujibu wa SALARY SLIP yangu ya 31.12.2020 Deni linasomeka Tsh. Mil 4.65

Aidha, cha kushangaza na kushtua jana HESLB wakanitumia kwa njia ya email statement ya deni langu ambapo Deni langu linasomeka nadaiwa Tsh. Mil 12.087 wakati kwenye Salary slip ya mwezi deni ni Tsh. Mil 4.65. Kiukweli nilichanganyikiwa nikawatumia ujumbe Bodi ya mikopo kuomba ufafanuzi wa hiki na leo Jumatano asbh nikajibiwa kuwa hakuna kilichokosewa kwenye statement waliyonitumia jana.

Baada ya kuona sielewi imelazimika nisafiri hadi Halmashauri kuonana na AFISA UTUMISHI ili aweze kunipa ufafanuzi wa jambo hili, nilipofika akampigia simu AFISA kutoka makao makuu ya HESLB ambaye ndo anashugulika na makato ya fedha zote kutoka kwa wanufaika wote nchini, alimpigia palepale mbele yangu na akaweka Loud speaker yule Afisa wa Bodi akaeleza mambo mengi sanaa kuhusiana na fedha hii.

Ambapo kiujumla amesema kwamba watumishi wote tunaokatwa kupitia mishahara yetu deni tunaloliona kwenye hizo salary kama linapungua sio deni halisi bali deni la halisi analodaiwa mnufaika wanalo wao Bodi kwenye mfumo wao ambao mfumo wao hauna mahusiano yyte na Mfumo wa Lawson, hivyo deni letu halisi huwa haliwi updated kwenye salary slip ndo maana tunaona kila mwezi linapungua ila kiuhalisia ni hapana.

Akaendelea kusema mtumishi yeyote akitaka ajue deni lake halisi analodaiwa basi aombe Loan Statement kutoka Bodi hapo ndo anaweza kujua deni lake halisi ambalo ni tofauti sanaaa na linaloonekana kwenye Salary slip zetu.

Akasema tena deni lililopo kwenye salary slip linapokwisha mtumishi anaweza akaona kama vile kamaliza deni, kumbe kuna deni kule bodi bado wanamdai. Hivyo akasema sasahv wapo kwenye mchakato wa kuandaa barua kuwatumia waajiri wote nchini madeni mapya ya wale wote ambao washakamilisha kulipa deni la kwenye salary slip ili makato yaendelee kama kawaida.

Mwisho Afisa huyo akamuomba Afisa Utumishi anipatie mimi namba ya huyo Afisa ili kama mahali nitakuwa sijamwelewa vzr niweze kumpigia wkt wwte kwa maelezo ya kina.

Hivyo ndug watumishi na walimu wenzangu ambao ni wahanga wa hili tusijipe matumaini ya kuclear hili deni tunaweza hata kustaafu nalo. Tupambaneni kutafuta hela ili watoto wetu tuwanusuru na kuongia kweny hili janga la Bodi ya mikopo ili tuwasomeshe kwa fedha zetu hata kwa kujibana maana inauma sanaaa.

Yeyote atakayehitaji namba ya simu ya huyu Afisa kutoka HESLB kwa ajili ya maelezo ya ziada anaweza kunitafuta inbox nikamtumia. Asante

BY. MWL MUSSA A. IDDY
NAMONGE SEKONDARI

(NIMEITOA WHATSAPP)
 
Tumwombe Rais wetu mpendwa,

Rais wa wanyonge.

asamehe madeni yote waliokopeshwa watanzania kupitia bodi ya mikopo.

Tanzania ni nchi tajiri na ina rasilimali nyingi,hizi fursa wanyonge wazifaidi kwa kusamehewa madeni kama sisi tunavyosamehewa na nchi wafadhili(china)
 
Loan board ni kama jini linalonyonya damu, mishahara yenyewe kiduchu halafu hapo hapo loan board wanakamua bila huruma yoyote hali wakijua hayo madeni hayana uhalisia wowote zaidi ya mwendelezo wa kupiga hela na kukusanya mapato kutunisha mfuko wa serikali pendwa. Kuna mzee mmoja jana nilimwona kaweka uso wa huruma kuomba kufutiwa madeni na Chi Shwan Whaaa, lakini wao kufuta madeni au kuwaondolea wanyonge kodi ni mtihani mkubwa.
 
Toka ni graduate sijawaingia kweny system na sijawahi walipa.

Na Nina biashara zangu kubwa poleni kwa mtakao ajiriwa.
Pole sana ndg Iddy...
Bodi ya mikopo yaani HESLB mimi naamini ni chombo kimeundwa kuwadidimiza watanzania kwenye lindi la umasikini.
.
Mimi binafsi nilienda bodi ya mikopo kuomba kujua nadaiwa kiasi gani wakasema jumla wananidai shilingi milioni 60.
.
Nilipambana nao sana zaidi ya miaka 2 bila mafanikio na mwisho nikaamua niachane nao waendelee kunikata ila nikiamini kuna siku nitawakimbia nikiachana na ajira rasmi.
.
Kwa ufupi HELSB hawana taarifa sahihi kuhusu nani wanamdai na anadaiwa nini, kikubwa nilichogundua wanajaribu kughushi taarifa za madenina kuwabambikia watanzania madeni ya ajabu.
.
Umenena vema,...tutafute pesa ili hata siku moja tusiruhusu watoto wetu kujiingiza kwenye madeni na hili zimwi linaitwa bodi ya mikopo
 
Tumwombe Rais wetu mpendwa,

Rais wa wanyonge.

asamehe madeni yote waliokopeshwa watanzania kupitia bodi ya mikopo.

Tanzania ni nchi tajiri na ina rasilimali nyingi,hizi fursa wanyonge wazifaidi kwa kusamehewa madeni kama sisi tunavyosamehewa na nchi wafadhili(china)
Huyo ndio ndio katufikisha hapa.
 
Back
Top Bottom